Kwenye vilabu vya Simba na Yanga ni nani mwenye mamlaka ya kufukuza kocha au kuleta kocha mpya?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wakuu swali limejieleza vizuri sana , sasa naomba kufahamishwa mwenye mamlaka ya kuleta kocha na kutimua , na huwa wanatumia vigezo gani ?

Taarifa nyingi za kutimuliwa kwa makocha wa vilabu hivi tunazipata bila hata kusikia vikao vya uongozi wa vilabu husika , Baada ya Kishingo kuachia ngazi baadhi ya viongozi wa Simba akiwemo Mwina Kaduguda walipoulizwa walidai kwamba hawajui chochote , sasa kama hawa viongozi hawajui chochote ni nani anayefanya maamuzi ?
 
Kasome katiba ya Simba utaelewa na huta uliza uliza, acha uvivu, jipange na pena kujisomea .
 
Kasome katiba ya Simba utaelewa na huta uliza uliza, acha uvivu, jipange na pena kujisomea .
Hongera Simba kwa kufuata katiba , bila shaka ndio taasisi ya kwanza na ya mwisho kufanya hivyo nchini Tanzania , Vipi kuhusu Katiba ya Yanga
 
Simba na yanga ni timu mbili tofauti kabisa katika mfumo wa uendeshaji na utofauti huo ndo unaleta nani ana nguvu ya kumfukuza kocha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…