wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,432
Nawashangaa sana wamalawi, yani karibia kila siku ajenda kuu za kimataifa lazima wagusie ziwa Malawi / Nyasa.
Mpaka wa kusini wa Ziwa Nyasa na Msumbiji uliwekwa kupitia mikataba kati ya Uingereza na Ureno, ambayo iligawa mpaka wa ziwa katikati.
Hata hivyo, mpaka kati ya Tanzania na Malawi ulitokana na mkataba kati ya Uingereza na Ujerumani 1890 enzi hizo Tanganyika ikiwa koloni la Ujerumani, ambao uliweka ziwa lote chini ya himaya ya Uingereza (baadaye likarithiwa na Malawi).
Lakini sheria hizo ni za zamani, kwani kwa mujibu wa sheria za sasa za kimataifa, mipaka ya maziwa kwa kawaida hugawanywa katikati (kama ilivyofanyika kati ya Malawi na Msumbiji).
Soma Pia: Serikali: Marufuku Kutumia Ramani ya Tanzania kutoka Google Kufundishia Wanafunzi, Inaonesha Ziwa Nyasa liko Malawi
Malawi haitaki kukubali sheria za kisasa za kimataifa, badala yake inasisitiza kufuata sheria za zamani.
Wao wanachoamini ziwa kuitwa Malawi ni lao, hapa kwetu kuna ziwa Tanganyika lakini tumegawana na Congo bila shida.
Yani inavyoonekana wao wanachotaka upande wa Tanzania tusitumie maji ya ziwa bila idhini yao, wavuvi wa upande wetu wasivue samaki, n.k.