Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Suala ni complex zaidi ya hivyo.Mpaka wa kusini wa Ziwa Nyasa na Msumbiji uliwekwa kupitia mikataba kati ya Uingereza na Ureno, ambayo iligawa mpaka wa ziwa katikati.
Hata hivyo, mpaka kati ya Tanzania na Malawi ulitokana na mkataba kati ya Uingereza na Ujerumani 1890 enzi hizo Tanganyika ikiwa koloni la Ujerumani, ambao uliweka ziwa lote chini ya himaya ya Uingereza (baadaye likarithiwa na Malawi).
Lakini sheria hizo ni za zamani, kwani kwa mujibu wa sheria za sasa za kimataifa, mipaka ya maziwa kwa kawaida hugawanywa katikati (kama ilivyofanyika kati ya Malawi na Msumbiji).
Malawi haitaki kukubali sheria za kisasa za kimataifa, badala yake inasisitiza kufuata sheria za zamani.
Soma andiko uone complexity.
The Nyerere Doctrine of State Succession inazipa nchi mpya wakati fulani baada ya uhuru kukataa mipaka yake ya kikoloni kama haijaridhika nayo, muda huo ukipita bila nchi hiyo kukataa mipaka yake hiyo, inachukuliwa kuwa nchi hiyo imeikubali mipaka hiyo.
Tanganyika haikuikataa mipaka ikiyokuwepo, licha ya kupewa nafasi ya kufanya hivyo.
Zaidi, Rais Nyerere na Waziri Mkuu Kawawa walishakubaki kwamba mpaka halali wa Tanzania na Malawi upo katika pwani ya mashariki ya ziwa Nyasa/Malawi.
Soma andiko hilo utaona mambo yote yameelezwa wazi.
NEGAN