Kwetu tunapohesabu wafu, wenzetu sasa wako kwenye kurejea maisha yao ya kawaida

Kwetu tunapohesabu wafu, wenzetu sasa wako kwenye kurejea maisha yao ya kawaida

Kuweka tangazo kama hilo haina maana wameweka idadi halisi ya maambukizi. Kwa kiongozi dikteta, hakuna cha kuamini kutoka kwake, kwani kila kitu kinaenda kwa vitisho na kutaka aonekane anayamudu mambo. Kwamba hakuna aliyekufa, ndio haiaminiki kabisa.
Kwa nini machapisho yako katika Kiingereza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu atusaidie

Mkuu Mungu hajaribiwi.

Kwenye yale maombi ya siku 3, wapo walithubutu kusema maambukizi na hata vifo vilikuwa vichache (wakati ule) eti kutokana na jitihada zao za kuomba. Sina hakika leo wanasema je au ndiyo hivyo tena wamesha acha kuomba.

Kwenye maombezi nadhani kama huyu hapa chini, wana akili kichwani siyo matope:

IMG_20200502_151623_320.jpg
 
Mass screening and testing huku kwetu wanasema ni gharama,
Kwa hali hii lazima tushuhudie mengi
 
Weka maoni yako unadhani nini kifanyike kwa sasa

Maoni ya nini kifanyike yamesgaelezwa mno. Kama utakuwa haujayaona basi labda kama ndiyo kwanza umerejea toka sayari nyingine.

Nini kifanyike hata kuongea na walikofanikiwa hatuwezi? Hivi majasusi wetu ni wa kupambana na kina Ben na kina Lissu tu?

Hivi huko hata mabalozi hakuna?

Ila kama kweli hujui nini kifanyike angalia japo humu:

Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums

Kwenu: Ummy, Taskforces, mabibi na mabwana katika mapambano ya dhati dhidi ya Corona - JamiiForums

Yako mengi mno kama haya hayatoshi sema tukuongezee.

Ajabu na kweli tumechagua kulinda uchumi ambao hata hivyo katika hali ya sasa haulindiki na hautalindika badala ya kulinda maisha ya watu kwanza.

Hatuna ambacho yeyote kwa hali ya sasa anaweza kujifunza kwetu. Tumekuwa kichekesho katika dunia iliyo staarabika:

IMG_20200424_182838_396.jpg


Hayupo mmoja katika hao ambao nchini kwake ana cha kutamanika kuhusiana na huu ugonjwa.
 
Nenda kaishi Rwanda [emoji1206] hakuna aliyekukataza brazaj


Sent using IPhone X

Dhana hiyo unayoongelea ni dhana mufilisi sana ambayo pia ishaongelewa sana.

Mkuu si wewe wala jiwe wala awaye yote mwenye hati miliki ya nchi hii. Hayupo mmoja awaye yote anayeweza kwa matakwa yake tu kudhani kuwa yeye ni mtanzania mno kuliko mwingine, kiasi cha kumwamrisha, kumtaka, kumshawishi au kumwomba mwingine kuondoka nchini.

Kwamba nchi fulani wanafanya vyema hilo ni jambo la kheri tu ndiyo maana ni jambo la afya mno kujifunza toka kwa wanaofanikiwa.

Jambo la msingi uwepo wa mavuvuzela ambayo yataunga mkono juhudi no matter what hiyo mbona inafahamika Mr. Vuvuzela?
 
Hizi nchi za kiafrika zina mambo mengi yanayofichwafichwa na watawala, hata taarifa zao sio za kuziamini sana, kenya naweza kuwaamini kiasi fulan ila hizi zenye mkono wa chuma kama uganda, burund, rwanda mmh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuweka tangazo kama hilo haina maana wameweka idadi halisi ya maambukizi. Kwa kiongozi dikteta, hakuna cha kuamini kutoka kwake, kwani kila kitu kinaenda kwa vitisho na kutaka aonekane anayamudu mambo. Kwamba hakuna aliyekufa, ndio haiaminiki kabisa.
Kwa nini machapisho yako katika Kiingereza?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulitaka yaandikwe kiswahili mkuu? Kwani wewe umeona hayo ni matangazo?

Kwa mawazo yako kwa vile kwetu tuna pukutika na kwingine ni hivyo hivyo?

Unadhani namba zinadanganya? Uthibitisho wa kisemwacho maisha yanaanza kurejea. Pia mikakati inaonekana. Mikakati huwa na progress reports. Mchanganuo wa hizo zinaweza kuashiria nani anasema ukweli na nani anasema urongo.

Hujawasikia WHO wanampigia kelele nani kuhusiana na uchakachuzi wa taarifa za maambukizi na vifo?

Acha sisi wanaojifukiza wamalize kwanza wiki yao ya nyungu kisha walete mrejesho.
 
Hizi nchi za kiafrika zina mambo mengi yanayofichwafichwa na watawala, hata taarifa zao sio za kuziamini sana, kenya naweza kuwaamnini ila hasa hizi zenye kila dalili ya mkono wa chuma kama uganda, burund, rwanda mmh

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtawasema sana. Ila WHO Rwanda anawakubali. Wao tofauti na wengine hao walikwenda total lockdown ya nchi nzima.

Uganda partial lockdown ya nchi nzima.

Kenya partial lockdown ya Nairobi na Mombasa tu.

Burundi hawa wamefunga mipaka tu.

Ni wazi kuwa ugonjwa huu unadhibitiwa kufuatia ukali wa hatua zinazochukuliwa.

Kutokana na ukweli huo, order ya mafanikio ni dhahiri itakuwa hivi:

Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na wa mwisho kabisa duniani atakuwa baba lao Tanzania. Huyu yeye bila aibu kaamua kutojishughulisha na kupambana na huu ugonjwa. Wa kufa afe wa kupona apone.

Kama haijatosha baba lao Tanzania akajipanga kuwaaminisha watu kuwa hapa ni kunawa nawa tu.

Yule mbunge au Anna Mgwira waliougua Corona walishindwa kunawa? Hao hata madaladala hawapandi na masokoni hawaendi. Sembuse mimi na wewe?
 
Mass screening and testing huku kwetu wanasema ni gharama,
Kwa hali hii lazima tushuhudie mengi

Maombi ya siku 3 walimaliza bila mrejesho.

Labda wanampango wa kuunganisha pamoja na wiki ya nyungu ndiyo watupe mrejesho wa jumla.
 
Dhana hiyo unayongelea ni dhana mufilisi sana ambayo pia ishaongelewa sana.

Mkuu si wewe wala jiwe wala awaye yote mwenye hati miliki ya nchi hii. Hayupo mno awaye yote anayeweza kwa matakwa yake tu kudhani kuwa yeye ni mtanzania mno kuliko mwingine, kiasi cha kumwamrisha, kumtaka, kumshawishi au kumwomba mwingine kuondoka nchini.

Kwamba nchi fulani wanafanya vyema hilo ni jambo la kheri tu ndiyo maana ni jambo la afya mno kujifunza toka kwa wanaofanikiwa.

Jambo la msingi uwepo wa mavuvuzela ambayo yataunga mkono juhudi no matter what huo mbona inafahamika Mr. Vuvuzela?

Unataka kuniambia kama jirani yako kila weekend anapeleka familia yake hotel ya 5 star kwenda kuenjoy na wewe utaiga kwa kuwa ni jambo zuri!?tuanzie kwako wewe unatoa mchango gani kwenye serikali?


Sent using IPhone X
 
Unataka kuniambia kama jirani yako kila weekend anapeleka familia yake hotel ya 5 star kwenda kuenjoy na wewe utaiga kwa kuwa ni jambo zuri!?tuanzie kwako wewe unatoa mchango gani kwenye serikali?


Sent using IPhone X

Mkuu hapa hakuna issue ya five star hotels. Hapa kuna suala la kufa au kuishi. Kwa mukthadha wa nchi:

'hapa pana suala la kufa au kuishi kwa kutumia raslimali zilizopo katika nchi husika". Hapa tena hamna cha nchi mjomba maana kila mtu ana pambana na lake.

Mfano mzuri ni kuwa kimepungua joka nyumbani. Una uamuzi wa kuliangamiza kuwahami wanao au kuwaakimbia wanao wawe wahanga wa joka hilo.

Achana na ndoto za hoteli za nyota tano jifunze kwa jirani zako wakakamavu wanao simama imara kuhami familia zao dhidi ya nyoka wavamizi kwa kutumia zana zozote walizo nazo karibu.

Kumbuka mkuu waungwana wanasema: "fimbo ya mbali haiui nyoka."

Kwa maana kamili ya kuwa tiba au chanjo ambayo haijagunduliwa kwa sasa haina msaada wowote!
 
Mpaka Sasa hakuna Alie ishinda Corona Ila Corona bado inaongoza na nikwambie tu wameamua kurudi kufanya kazi sababu ngoma bado ngumu
Wenzetu baada ya kuweka jitihada za dhati kuzuia ugonjwa wa Corona kusambaa, sasa wao wanapanga kurejea maisha ya kawaida. Wanazo takwimu zote muhimu. Sasa wanajua mashule lini yafunguliwe na lini warejee vipi kwenye maisha ya kawaida:

View attachment 1437362
View attachment 1437367

View attachment 1437365

Kwetu tuko hapa:

View attachment 1437370

Hatuna takwimu za watu tunaofuatilia wala waliomo quarantine.

Tupo tunasubiria kudra za mwenyezi Mungu na sasa wataalamu wa kufukiza nyungu nao ndiyo wamesha shika usukani kutuhubiria imani zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom