Mkuu
Tarime one, kwikwi inatokana na kujikunja ghafla kwa misuli inayotenganisha kifua na tumbo (diaphragm).
Kwilwi inaweza kusababishwa na :-
Kula haraka haraka na kubwia hewa kwa wingi na kujaza tumbo.
Ulaji uliopitiliza wa vyakula vyenye mafuta, viungo (spices),unywaji wa vinywaji vyenye gesi kama soda na bia ambavyo vintanua tumbo na kukera (irritate) diaphragm.
Magonjwa yanayoweza kukera diaphragm kama magonjwa ya ini na pneumonia, upasuaji wa tumbo
Magonjwa kama kiharusi, uvimbe kwenye ubongo na ugonjwa wa figo kutofanya kazi (renal failure)
Vile vile dawa kama diazepam (valium) na Lorazepam(ativan) zinaweza kusababisha kwikwi.
Matibabu ya kwilwi yanaweza kuanzia nyumbani kwa:-
Kunywa glass ya maji kwa kasi
Kushikilia pumzi kwa muda kuongeza hewa juvu mwilini
Kushtuliwa ghafla
Kusukutua kinywa
Kung'ata kipande cha limau