Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

Jamani wataalamu wa mambo ya afya, nimevumilia mpaka nimechoka sasa nazidi kuumia tu.

Kuanzia kwenye saa tisa usiku napiga kwikwi mpaka muda huu, ikitulia kidogo ni kama nusu saa inaanza tena. Hii inasababishwa na nini? na nifanyeje iweze kuacha kabisa?

Nisaidieni wanajamvi
 
Am not a dokta, ila mimi huziba pua zote na kunywa maji mafunda kama 9 hivi. The problem usually goes away.
 
Kwikwi husababishwa na nini?





Baada ya kusoma makala inayohusu kijana mmoja aliyesumbuliwa na kwikwi kwa zaidi ya miaka miwili na nusu, na baadaye kutibiwa tatizo hilo kwa kufanyiwa upasuaji wa ubongo na kutolewa tezi, nimeamua leo nizungumzie kwikwi.

Kwiki ni kitendo kisichozuilika ambacho hutokana na kusinyaa kwa kuta za kiwambo cha moyo au diaphragm. Kwa kawaida kwikwi ni

kitendo kinachojirudia rudia mara nyingi. Sauti ya 'hic' inayotokea wakati unapokuwa na kwikwi husababishwa na kidaka tonge

(epiglottis) ambacho hufunga haraka wakati hewa inapoingia kwenye koo. Kupiga kwikwi kwa kawaida hakuna maumivu lakini mara

nyingine husumbua hasa inapoendelea kwa muda mrefu. Kwikwi ya kawaida huweza kutulizwa kwa kunywa maji, lakini wakati mwingine kufanya hivyo hakusaidii.

Zifutazo ni sababu zinazoweza kukuletea kwikwi
1. Kula kwa haraka.
2. Kula chakula cha moto na kunywa maji baridi baada yake.
3. Kulia au kukasirika.
4. Kula chakula chenye viungo vingi au pilipili.
5. Kula chakula cha moto sana.
6. Kunywa pombe au soda kwa wingi.
7. Kukohoa sana.
8. Kucheka kupita kiasi.
9. Kufurahi sana, kusisimka au kupatwa na msituko.

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, vitu ambavyo vinakiletea karaha kiwambo cha moyo au diaphragm husababisha kwikwi. Kuna sababu nyingi ambazo husababisha jambo hilo na hizo tulizotaja hapo juu ni miongoni mwazo,ambapo matokeo yake ni humfanya mtu

apige kwikwi. Kwikwi kwa kawaida huisha baada ya dakika chache au hata sekunde. Lakini iwapo kwikwi itaendelea kwa masaa au kwa siku, huweza kuwa ni tatizo muhimu la kitiba na pengine hali kama hiyo inaweza ikawa inasababiswa na ugonjwa.

Kuna baadhi ya watu hupata kwikwi sana wakati wa ujauzito, baada ya kufanyiwa operesheni na hata watoto wachanga pia hupatwa na kwikwi mara kwa mara. Wajawazito hupata kwikwi sana mwishoni mwa miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito na mwanzoni mwa miezi

mitatu ya pili. Kwikwi hutokea wakati wa ujauzito ni kwa sababu wakati huo uwezo wa kuvuta hewa ndani ya mapafu na kutoa nje huongezeka kwa asilimia 30 hadi 40 ikilinganishwa na hali ya kawaida. Hakuna sababu inayojulikana inayosababisha kwikwi kwa watoto

wachanga, na wazazi wanashauriwa wasitiwe hofu na suala hilo. Hii ni katika hali ambayo kwikwi baada ya upasuaji husababishwa na nusu kaputi au anesthesia.
 
Dawa ya kutibu Kwikwi Chukua mua mweusi Kamua upate maji yake Uchanganye na asali safi ya nyukiunywe inshallah utapona. Tumia kisha uje unipe maendeleo ya Dawa yangu Give me a feedback mkuu.@Change_it
 
  • Thanks
Reactions: ral
mkuu Mtali Muwa Mweui nliokusudia ni huu mkuu ni dawa ya huo ugonjwa wa kwikwi kuna mtu mmoja nilimpa humu jamvini dawa hiyo alipona hebu angalia muwa wenyewe jinsi ulivyo tumia kisha uje unipe feedback.
32539403.jpg

Muwa mweusi ndio upi mkuu MziziMkavu???
 
Last edited by a moderator:
wadau habari za leo,naomba kupata ushaur wenu ni siku ya tatu sasa Mzee wangu anasumbuliwa na kwikwi,si mchana wala ucku yaan ni balaa,je kuna tiba mbadala yeyote?coz tumempeleka Ocean Road amepewa dawa lakin hatuon mabadiliko yeyote.msaada wapendwa!
 
Hii dawa ni ya zamani sana mama yangu alikua akinifanyia nikiwa mdogo.
Nilipokuwa na kwikwi alikua ananipigisha story mpya kabisa ambayo ni ya kustusha. Nikistuka tu kwikwi nayo ilikua inakata.
Sina hakika kama itamsaidia mzee wako.
Jaribu lakini

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hiccup?
If not persistance (that prolong for more than a day) drink a lot of water..if it is,see a doctor.
 
Naskía ukimpiga kofi mgongoni inakata, sina uhakika japo..
 
Mimi pia hukumbwa sana na hilo tatizo lakn lugha ya kitaalamu imetumika sana so nimeambulia patupu.
 
Ningependa kujua chanzo cha kwikwi na faida na madhara yake na inaashiria nini katika afya zetu, naomba kueleweshwa.
 
Mkuu Tarime one, kwikwi inatokana na kujikunja ghafla kwa misuli inayotenganisha kifua na tumbo (diaphragm).
Kwilwi inaweza kusababishwa na :-
Kula haraka haraka na kubwia hewa kwa wingi na kujaza tumbo.
Ulaji uliopitiliza wa vyakula vyenye mafuta, viungo (spices),unywaji wa vinywaji vyenye gesi kama soda na bia ambavyo vintanua tumbo na kukera (irritate) diaphragm.
Magonjwa yanayoweza kukera diaphragm kama magonjwa ya ini na pneumonia, upasuaji wa tumbo
Magonjwa kama kiharusi, uvimbe kwenye ubongo na ugonjwa wa figo kutofanya kazi (renal failure)
Vile vile dawa kama diazepam (valium) na Lorazepam(ativan) zinaweza kusababisha kwikwi.
Matibabu ya kwilwi yanaweza kuanzia nyumbani kwa:-
Kunywa glass ya maji kwa kasi
Kushikilia pumzi kwa muda kuongeza hewa juvu mwilini
Kushtuliwa ghafla
Kusukutua kinywa
Kung'ata kipande cha limau
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tarime one, kwikwi inatokana na kujikunja ghafla kwa misuli inayotenganisha kifua na tumbo (diaphragm).
Kwilwi inaweza kusababishwa na :-
Kula haraka haraka na kubwia hewa kwa wingi na kujaza tumbo.
Ulaji uliopitiliza wa vyakula vyenye mafuta, viungo (spices),unywaji wa vinywaji vyenye gesi kama soda na bia ambavyo vintanua tumbo na kukera (irritate) diaphragm.
Magonjwa yanayoweza kukera diaphragm kama magonjwa ya ini na pneumonia, upasuaji wa tumbo
Magonjwa kama kiharusi, uvimbe kwenye ubongo na ugonjwa wa figo kutofanya kazi (renal failure)
Vile vile dawa kama diazepam (valium) na Lorazepam(ativan) zinaweza kusababisha kwikwi.
Matibabu ya kwilwi yanaweza kuanzia nyumbani kwa:-
Kunywa glass ya maji kwa kasi
Kushikilia pumzi kwa muda kuongeza hewa juvu mwilini
Kushtuliwa ghafla
Kusukutua kinywa
Kung'ata kipande cha limau

shkran %
 
Last edited by a moderator:
Nilichosema mkuu ni kuwa moja ya side effects za valium ni kwikwi tafadhali onana na daktari wako akupe dawa zingine kama hiyo kwa sasa inakuletea kwikwi za mara kwa mara
 
Back
Top Bottom