Pole Kichwa Ngumu....usitishike, kwikwi (hiccup) ni kitu cha kawaida kwa watoto wadogo, especially wachanga..ni kama 'reflexes' (sijui kiswahili chake samahani) zinazotokea sababu ya kutokomaa kwa viuongo vya ndani vya mtoto. Kwa hiyo mtoto anapokuwa na kukomaa, basi kwikwi zinapungua pia. Inaweza zikadumu kwa kuanzia dakika chache mpaka masaa kadhaa.
Kitabibu, hakuna tiba ya moja kwa moja ya kwikwi kwa mtoto...kuna vitu vingi watu huwa wanafanya (baadhi ndio ulivyofanya wewe) lakini huwa havisaidii. Lakini kujaribu kum'distract' mtoto wakati ana kwikwi kwa kumvutia na kitu kingine mfano chenye rangi za kuvutia au kinachotoa sauti flani hivi kupata attantion ya mtoto inaweza saidia.
NB: Mara nyingi mtoto anapopata kwikwi ni wazazi/walezi ndio wanaosumbuka...lakini si mtoto, kwani kwikwi haimsumbui mtoto!