Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM


Huwezi kukerwa na matatizo ya watanzania halafu ukadhani utayatatua kwa kugombea kupitia CCM..Utagombea na ni rahisi kushinda ukipita kwenye vikao vyao vya mchujo lakini baada ya hapo utakuwa mtumwa tu wa kufuata vile system inataka.
Hata kama una uchungu na tanzania,ukipita either ufuate wanavyotaka(na wengi ndiyo wanakuwa hivyo) au ujifanye nunda wakupoteze kwenye chati uishie kukimbilia kwa kina Mrema.
Mimi mtu yeyote anayejifanya ataleta mabadiliko kwa kugombea kupitia CCM namuona mzushi tu.Bora ugombee upinzani unaweza ukanishawishi manake ukishinda namba ya wabunge wa upinzani itaongezeka labda unaweza kuondoa two thirds za CCM za kupitishia miswada mbofumbofu.
Mkuu samahani nimeona niandike hapa japo haifanani sana na hoja yako.
 
Duh, Siasa za Bongo wakuu zangu kiboko..Hivi kweli tunategemea Mwakyembe kufanikiwa kuliendeleza jimbo lake wakati mfumo wa Uongozi wenyewe unajionyesha wazi kuwa haiwezekani.
jmni eeeh mhazini wa tanzanet ana lipi jipya?......Jf bana sasa hivi mwakyembe anaonekana hajafanya la maana kyela .......

miaka kibao kakaa majuu kafan ya lipi bana la maana zaidi ya kuja kuandaa ma party tu kama wengine.......mie nina uhakika uwezo wake wa kuwasaidia wana kyela unaonekana hata kabla sio mbunge.......tunamsubiri na w.malecela jimbo la mtera.....
 
Nikweli George anagombea Kyela kwa kupitia CCM, na nime confirm hilo kutokana na mmoja wa washauri wake ambaye anaishi hapa USA na amekwenda Tanzania kuungana na yeye.

Labda niseme kitu kimoja, George hana CV ya kutisha kama ilivyopambwa hapa JF. Ana elimu ya juu ya maswala ya computer, masters degree ni common kwenye bunge la Tanzania. Make no mistake i don't attack the men qualifications, what i attack is the motivation behind his campaign.

Nikweli yeye ni mmoja wa watu wa mwanzo hapa JF, vile vile tulikuwa tunatumia Tanzanet tunaukubali mchango wako. However, mpaka sasa yeye kama mkazi wa Kyela ameifanyia nini KYELA? Kwa kutumia resource ndogo alizo nazo jee amawekeza vipi katika jimbo hilo?

Kugombea ni haki ya msingi na anayepinga hilo inabidi asome katiba upya. However, nikiwa kama Mtanzania nauliza hivi Jee GEORGE amesaidia nini KYELA ya leo? Mbunge Tanzania hana power ya kulazimisha serikali kuchannel resources katika jimbo lake. Mwakyembe ameitikisa serikali ya JK madhara yake ni kwamba serikali ya JK imegoma kuchannel resources kwenye jimbo lake.

Kwa maana hiyo George anataka kuingia bungeni ili awe MR Yes? Maana siku akisema NO atapa the same thing. Hili ndio Tatizo la Tanzania, hatuna patriotism, na ndio maana naona hapa kwenye JF tunapiga kelele za bure sababu tunajali sana favorism.

Convice me more kwamba George is not more of the same. Kama kuna mtu ana namba ya Mwakyembe naomba Tafadhali....
 

kweli kabisa... Baadhi yetu tulireport Richmond siku ya kwanza kabisa alipokuja JK USA kuhutubia UN.... Muda ule ndio Kina Muhamed Gire walipika jungu.
Tukubali au tukatae Mwakyembe ndio engineer wa kuwasukuma kina Lowassa kwenye dimbwi.
 
Kama kakanusha mwenyewe basi tumwache. Lakini magazeti yamemwekea maneno mdomoni? Au alikuwa anaangalia kina cha maji? Kama ana uchungu na Kyela afanye kwanza chochote wananchi waone kabla ya yeye kutaka ubunge.
 
Kweli wana kyela wasipo kuwa makini watafulia kwelikweli. Huyu jamaa siasa inaonekana ni mtupu kabisa.
 
Naona hapa tunaelekea kuendeleza utamaduni mmbaya kama ule wa kumchukulia kila anayepiga kelele kuhusu ufisadi hata kama ni tunawajua kuwa ni wezi, majambazi, mafisadi na manyang'au wakubwa kama mkombozi wakati tukijua fika kuwa huo ni usanii tu.

Sasa hapa napo nadhani tunataka kujenga utamaduni kuwa kama kuna 'mwenzetu' tunajuana naye mtandaoni na zaidi akiwa 'kigogo' basi huyo ni lazima atakuwa mkombozi wa madhila ya watanzania...This is wrong.........

Haya ya 'tumshindikize' mwenzetu sasa yatabadilika 'tumlinde' mwenzetu hapo baadaye.....then tunakuwa tunaruka uozo huu tunaogelea uvundo ule..

Vilevile mwenzenu ninatatizwa na huu utamaduni unaojengeka hapa kuwa ni sawa mtu kujiandia ndege kurudi nyumbani eti kuwasaidia watanzania kana kwamba mifano ya kina Kabourou na sasa Masha haitufunzi kuwa makini zaidi.

Tunapinga wafadhili weupe huku tukiwakumbatia wafadhili weusi (hapa hata Rostam na Mo nao wanaqualify) kama ambavyo tulipowaondoa wakoloni weupe tukapigania kuwajenga na kuwalinda wakoloni weusi...

omarilyas
 
Ni jambo jema kusikia kwamba yeye mwenyewe Mwakalinga anakataa kutohusika na kuitangaza nia ya kutaka kugombea ubunge huo wa kusadikika.

Kwa Kyela ilivyo, sidhani kama ni kazi nyepesi kwa sasa mtu kutoka Uingereza kugombea kiti hicho Ubungo mathalan, eti kaona uchungu sana kutoka Washington kwamba Manzese hawajaendelea, na kwa hiyo kwa kutumia taaluma yake ya kuendesha chain ya vyerehani mitaani Marekani ameshitukia kwamba aliyepo kwenye kiti hafanyi kitu, ila yeye atafanya.

Kyela is particularly too complex to look at it through a single eye and judge the possibility of you winning that bread. Wale jamaa wnashangilia sana mitaani na wanashabikia sana mtu hasa wakijua unao ulaji wa kuwapa, halafu wanakuacha kwenye mataa. Kuna makundi kweli Kyela, lakini huwezi kuyaunganisha kwa nguvu ya ulaya iliyo mikono mitupu.

Ukiiangalia Kyela wawezailinganisha na Bagamoyo, Ujiji n.k. Watakukaribisha sana kwa meno 32+ lakini wakati wa kura utashangaa kama Lyatonga kubebwa lakini kuambulia kura moja tu kwenye umati huohuo uliomshangilia na kumbeba na kusukuma gari lake kwa mijasho. Siasa za Bongo weacha tu bwana.

Bora kuamua kuuza maji kuliko kuwa mwanasiasa, maana kila mwenye kiu ni rafiki wa kweli wa maji ya muuza maji, lakini sio na mwenye kuyauza maji maji hayo. Angalia vilio vya bungeni kwa sasa, watu wameshaanza kujihami, tayari Sheh Hussein Yahaya katabiri wauzamaji pale bungeni kumwaga maji yao mwakani, watu hawajali, kila mtu anahangaika jinsi ya kuiona kesho yake na familia yake. Mwenye kukushawishi Mwakalinga usimwangalie kwa jicho zuri sana, anaishawishi mifuko yako ili imsaidie aione kesho bora, hana nia ya kweli kukusaidia wewe. Hapendwi mtu Bongo.

Leka
 
Msituletee wasanii hapa mbona mlifunga mjadala wake? hapa amefuata nini tena na mambo ya ubunge? hebu tupeni waasifu wake siyo oh mtaalaam wa komputa mara biashara kwani hizo ndizo sifa za ubunge? tuondoleeni kichefuchefu hapa.
 
Hawa ma mods waqchemfu sana wakati mwingine. Kila mtu anamjua huyo mtu kuwa ndio Mtanzania sasa wamefuta post yangu sijui kwa nini.

Nimekuelewa mkulu NN,you nailed it to death! i knew what was coming kutokana na comment za huyo mkulu.

BTW atapigwa kwa KO shauri yake! mark my words 2010 siyo mbali kiivyo.

Comments nyingi za kummaliza Dr.Harrison alizokuwa anazitoa hazikuwa objective,kumbe zilikuwa na malengo haya!!! ok nimeanza kuelewa sasa.

Asante sana NN kwa kuliweka hili wazi.
 
Acheni watu wajitokeze mapema hasa kwenye ngazi hii ya UBUNGE ili tuangalie namna ya kuwasaidia mashujaa wetu wa sasa warudi tena Bungeni. Nimemwona jana mama Shamsa Mwangunga akitamka rasmi kuwania Ubunge Jimbo la UBUNGO. Alikuwa kwenye kikao/semina ya KIDINI ambacho nadhani alikosea kukitumia kwa ajili hiyo.
Mnyika jiandae vizuri tu kama kweli CCM watampitisha huyu mama mdinimdini.
 
Huyo mwakalinga agombee tu lakini sisi wananchi wa Kyela bado tunaimani na mwakyembe na bado tunamwitaji. so elfu mbili na kumi sisi na mwakyembe tu. huyo mwakalinga hajui chochote kuhusu kyela. labda agombee ubalozi wa kijijini kwao.
MWAKYEMBE ATAZIDI KUPETA KYELA KWANI ANAJUA SHIDA ZA WAPIGA KURA WAKE. KAZI KWAKE HUYO MWAKALINGA
 

Hujui unachoongea , mwangunga hana udini wowote ni mtu poa sana yeye ni mwislamu lakini anajichanganya sehemu yoyote ile, kanisani anaingia kwani mumewe ni mkristo na watoto wake wote ni wakristo. acha kuongea kitu usichokijua.
 
kiuangalifu hata huyu bwn mwakalinga wa huko kyela duh msanii tu, sioni atafanya lolote, zaidi atadumisha biashara zake hapa tz tena hazitaendeshewa Mbeya itakuwa Dar, then mtu una masters hujafanyia kazi, unakuwa tuu ktk chama cha watz mh?nina wasiwasi mkubwa kuwa either msanii,(anajua kuongea sana) lakini matendo hayupo, inaonyesha wazi kwa mtu anehakiki kimakini!!
 
Du mjadala mtamu sana, wengine tunangoja muda mwafaka risasi zenyewe chache kwa hiyo inabidi kuzitumia kwa uangalifu sana.
 


Wamesema atagawa Laptop naona wengine hapa wameisha patiwa......!
 
hii sera ya laptop INANICHANGANYA AKILI!nahofia itakuwa ni 'one of the effects of jf'
 
Hujui unachoongea , mwangunga hana udini wowote ni mtu poa sana yeye ni mwislamu lakini anajichanganya sehemu yoyote ile, kanisani anaingia kwani mumewe ni mkristo na watoto wake wote ni wakristo. acha kuongea kitu usichokijua.
BN, kwa nini alilitumia jukwaa lile? Ulimsikia alichokisema C10?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…