Hivi CCM ilikuwepo wakati Watanganyika na baadae Watanzania walikpokuwa wanatolewa utumwani na pia wakati wa kujipatia uhuru?
Hivi CCM inajengwa na sera (tunazodai ni safi hata kama hatuzijui), majengo (waliyolazimishwa kuchangia watanzania na sasa yanauzwa kwa bei ya soko kwa watanzania haohao) na vikolombwezo vingine na sio wanachama wake? Je mienendo yao haihusiani na chama chao?
Hivi hili janga la ufisadi ndani ya CCM linahusu wale 'mafisadi' maarufu tu wa katika ngazi ya kitaifa ambao ni wazi CCM imekuwa na kigugumizi cha kudeal nao na sio kuanzia ngazi za mitaa, vitongoji, kata, wilaya na mikoa ambao kumejaa vigogo na vishoka watenda maovu?
Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo hujitokeza kichwani mwangu nisikiapo kuna watu bado wanajipa moyo kuwa CCM kama chama hakina tatizo lolote kama KADA nambari wani hapa anapojaribu kueleza...
Ukada kazi......
omarilyas
Huwezi kukerwa na matatizo ya watanzania halafu ukadhani utayatatua kwa kugombea kupitia CCM..Utagombea na ni rahisi kushinda ukipita kwenye vikao vyao vya mchujo lakini baada ya hapo utakuwa mtumwa tu wa kufuata vile system inataka.
Hata kama una uchungu na tanzania,ukipita either ufuate wanavyotaka(na wengi ndiyo wanakuwa hivyo) au ujifanye nunda wakupoteze kwenye chati uishie kukimbilia kwa kina Mrema.
Mimi mtu yeyote anayejifanya ataleta mabadiliko kwa kugombea kupitia CCM namuona mzushi tu.Bora ugombee upinzani unaweza ukanishawishi manake ukishinda namba ya wabunge wa upinzani itaongezeka labda unaweza kuondoa two thirds za CCM za kupitishia miswada mbofumbofu.
Mkuu samahani nimeona niandike hapa japo haifanani sana na hoja yako.