Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM


Kushitushwa wapi?
alichokanusha Mwakalinga ni kwamba wakati huo hakuwa Kyela bali Arusha na alichokanusha wakati huo ni kwamba kishaanza kampeni huko kelya vijijini .

Na alichofanya saizi ni kuonesha nia yake ya kuutaka kutumia haki yake kikatiba kama atakavyoitumia Mwakyembe.

Kwanini tunashindwa kutofautisha kitu hicho jamani? Yani mfano wewe uko hapo Dar harafu mimi nakuja nauvumi wa kwamba uko London ,nikikupigia simu kukuuliza uko wapi ukanijibu nipo Dar na wala siko London na sitegemei kuja ,harafu baada ya week kadhaa ukapata safari ya kwenda london eti nitashangaa? na kukuuliza kwanini upo london?

Mimi binafsi nitashangaa tu kama ungesema kamwe sitokaa nifike london maishani kwangu ama ndani ya miaka 2,5.
 
Pamoja na maoni mazuri ya Watanzania wenzangu katika thread hii, sijaona maoni ya mwana JF mmoja rafiki yangu anayekwenda kwa jina la MTANZANIA. Ningependa kujua maoni yake kuhusu Mwakalinga kugombea Ubunge mwakani katika jimbo la Kyela.
Mtanzania, pls popote ulipo tunaomba maoni yako, kwa sababu unazijua vema siasa za Kyela na Mbeya kwa ujumla, kama sie wengine.
 

Mkuu Idimi Mtanzania yupo busy sana.
 
mkuu msubiri SteveD yuko page ya 8 MS word anaandaa waraka kukujibu...btw mhazini wa tanzanet sidhani kama ana jipya.......




 

 
eeh basi mwakalL atakuwa msanii sanii tu.....hivi zile habari za majira ina maana wamezibuni? maana keshaanza kusema ati mwakeY analitumia majira kumchafua.....hivi kwani mwakaL msafi?
 
nasubiri comments za mtalaam wa siasa za Kyela, mkuu Mtanzania.
 

Max,heshima yako mkuu!

Kwa siasa za Kyela za sasa kurudi kugombea ubunge ni lzm ukubalike na"wenye wilaya",na hawa "wanyambala wawili kwa kweli watavurugana mno wilayani hapa!

Kuna wazawa Kyela wana nguvu sana ndani ya siasa za pale na ukiwakamata na kuwa upande wako kupata ubunge ni rahisi sana;kwa tafiti zangu rahisi inabidi uungwe mkono atleast na nusu ya watu hawa kama vile,Mzee Arthur Mwaitenda(aliyewahi kuwa DCI wa tz),Jeneral Mwamunyange(mkuu wa majeshi ya tz),Mzee Mwamunyange(aliyekuwa afisa mwandamizi wa jeshi la polisi-TZ),Francis Kifukwe,Mzee Mwanjala,Mzee Mwaikambo,Ally Mwaiposa,Askofu wa KKKT jimbo la Kyela-Ipyana na wengineo !

Mimi sina ubavu hata wa kuongea na wazee hawa waandamizi!
 
Nilitaka nimalize kusoma post zote ndipo nichangie, lakini hii ya Msauzi naona ni vema nikairekebisha kwanza. Mwaisaka sio mpambe wa Mwakyembe, huyo ni mlamba viatu wa Mwakalinga aka Mtanzania!!! Anaeleweka na kila mtu pale Kyela, anamsujudia Mwakalinga baada ya kuahidiwa ajira kwenye radio anayotaka kuanzisha!!!!

 
du nimekubali kuwa una data mzee. Hebu tupe wengine basi ambao hawangombei ili tupime basi kama form zinachukulika

......
umeanza tena matatizo yako? Angalia sana, ukifuata fuata watu utaishia kuumbuka maana data zote tunazo!

....
 

Mkulu Maxence, mimi ni mkazi wa kyela na kauli niliyoitoa ni ya kishabiki tu kama kauli za mashabiki wa yanga na simba. Mimi namshabikia Mwakyembe period kwasababu nzuri tu nilizonazo.

Napenda kuchangia katika maendeleo ya nchi yangu kwa namna nyingine na si hiyo ya kuwa kiongozi wa kuchaguliwa.

Nafikiri nimeweka record sawasawa.
 
......


....

Mwakyembe kisha weweseka .? Sasa kama yeye ni figure la taifa na amefanya mambo mengi si asubiri kampeni akawaambie hayo wananchi wa kelya kama wao hawayaoni.

tulichonacho ktk meza sasa ni kuwa Mwakalinga kisha onesha nia ya kuingia ktk kinyang'anyiro cha kupambana na mwakyembe kwa fikra chanya na si kupambana kwa mabavu na fikra hasi.
 

Ama ndiye? si unajua mwendo wa nyuma ya keyboard?
 
Wakuu Next Level, Kinyamana etc, ingieni kilingeni, tutawaunga mkono na mkienda kombo huko bungeni hatutasita kuwakosoa.

Ha!ha!ha!ha!ha! mkuu Max siasa za bongo lazima ujipange vizuri sana vinginevyo unaweza fulia weye pamoja na family yako aisee!

Kama nilivyosema awali hii mambo ya Dr. na Mwakalinga pamoja na siasa za Kyela kwa ujumla I like them....zinatoa changamoto na upinzani wa hali ya juu sana! Isipokuwa sipendi hii tabia ya kuchomekea siasa za visasi na visa kibao.....eti kama mmoja kamshinda mwenzie basi hakuna kutoa ushirikiano baada ya uchaguzi...tabia hii inapoteza hata maana ya siasa zenye uishindani tunazosifia huko Kyela. Kinachotakiwa kama mmoja kashinda basi aungwe mkono katika kuleta maendeleo jimboni sio kumwekea zengwe ashindwe kudeliver...hii inawacost wananchi wote!

Ukiangalia kwa haraka mazingira aliyonayo Dr. Kyela mi naweza sema ni vigumu kwa mbunge yeyote akiwa katika mzingira hayo kudeliver kwa kweli, amekuwa na wapinzani karibia kipindi chake chote ubunge so inakuwa vigumu sana kwake kuonyesha impact yake kule! Kwa mtindo huo, hata Mwakalinga akishinda wananchi wa Kyela hawatakaa waone maendeleo coz wale wa upande wa Dr. wanaweza kujoin forces kupinga jitihada zake!

Suala la muhimu ni kuendesha siasa ambazo zinatakuwa na maslahi kwa Kyela na Taifa kwa ujumla!

Mkuu Max don't worry wacha tujipange vizuri.....lakini kwa mimi 2010 ni mapema sana....but nakuhakikishia I am planning for this coming 2015 (earliest) but 2020 MUST!Ngoja mama yetu Makinda amalize muda wake in piece mkuu.....asije ondoka kwa pressure ...ha!ha!ha!
 
Kama ndani ya Kisima Cha Fikra sifa kuu za mgombea kuwa ndio hizi za kusadikika zisizo na mashiko,BASI TANZANIA YENYE NEEMA HAITAWEZEKANA!!!
 
kwa kigezo cha Mwakyembe sio Mwakalinga.
Na kama kigezo cha ubora wa hoja zako ndio kigezo cha washauri wa Mwakalinga basi tofauti ya Mwakalinga na Mwakyembe ni kama kichuguu na mlima kilimanjaro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…