Nakumbuka wakati naongea na Mwakalinga alisema haya:
Sasa sitashangaa kama kaamua kugombea rasmi, yaelekea ndo maana hata SteveD hajatia neno katika topic hii, atakuwa alipata kanusho toka kwa Mwakalinga na anashtushwa na habari hizi!
- Si kweli kuwa nimekuja Tanzania rasmi kugombea Ubunge, ikiwa hivyo nitawafahamisha watu wazi bila kificho.
- Mwakyembe anajaribu kunimaliza hata kabla sijafikiria kupambana naye kwa kutumia gazeti la Majira. {Mwezi Machi aliwahi kunipigia simu akinieleza kuwa Mwakyembe (ambaye pia ni member wa JF) alikuwa akimsumbua sana kwenye PM na alidai kuwa anatumia gazeti la Majira kuendeleza propaganda dhidi yake.}
- Hata kama nikigombea Kyela kwani jimbo hilo Mwakyembe ana hati miliki nalo?
Kushitushwa wapi?
alichokanusha Mwakalinga ni kwamba wakati huo hakuwa Kyela bali Arusha na alichokanusha wakati huo ni kwamba kishaanza kampeni huko kelya vijijini .
Na alichofanya saizi ni kuonesha nia yake ya kuutaka kutumia haki yake kikatiba kama atakavyoitumia Mwakyembe.
Kwanini tunashindwa kutofautisha kitu hicho jamani? Yani mfano wewe uko hapo Dar harafu mimi nakuja nauvumi wa kwamba uko London ,nikikupigia simu kukuuliza uko wapi ukanijibu nipo Dar na wala siko London na sitegemei kuja ,harafu baada ya week kadhaa ukapata safari ya kwenda london eti nitashangaa? na kukuuliza kwanini upo london?
Mimi binafsi nitashangaa tu kama ungesema kamwe sitokaa nifike london maishani kwangu ama ndani ya miaka 2,5.