Wakuu,
Naomba kwa wale ambao mna mtetea au ni wapambe wa Mwakalinga, muache hasira na andikeni hoja. Jino kwa jino wote tutageuka kuwa na ngeu.
Hilo ndilo ombi la Mwakalinga mwenyewe. Kwa mfano kuna sehemu nimeona mtu kaandika Mwakalinga atamwaga laptop kila shule. Jamani, Mwakalinga hajasema hivyo na naamini hata siku moja hawezi kusema hivyo maana huwa haahidi mambo asiyoweza kuyafanya.
Tubaki kwenye hoja.
Kule Kyela watu wameelemika na kufarijika, tusiwachanganye na kuwaangusha kwa habari ambazo sio kweli. Mtu anaweza akaja hapa JF akasoma na akafikiri ni kweli mwakalinga ameahidi hivyo; baadaye akiona hakuna laptop akaanza kusema jamaa alidanganya.
Wewe si ndiyo Mwakalinga mwenyewe? Wewe Bwana hueleweki. Mara useme hivi mara vile. Nakuomba kama kweli umekuja kwa wana kyela kwa nia njema ya maendeleo ujibu maswali yafuatayo:
1.Ni kweli ulifika kyela?
2.Umetangaza kwa wana kyela kwamba utagombea ubunge next year?
3.Ni kweli ulienda Monduli kabla ya kwenda kyela?
4.Wewe ni kibaraka wa Lowassa na washirika wake?
5.Kama ndiyo unadhani ni njia sahihi ya kupatia ubunge kyela?
6.Kama siyo, unajua watu wanakuhusisha na Lowassa na kundi lake?
7.Unajua madhara ya kisiasa ya kuhusishwa na kundi la akina Lowassa?(nachelea kuwaita mafisadi)
8.Ulifuatilia kwa umakini uchaguzi wa NEC wa mkoa wa mbeya kati ya Mwandosya na Thom
Mwang'onda?
9.Unajua kilichomfanya Mwang'onda ashindwe ni kundi aliloambatana nalo japo alikuwa akiungwa mkono na viongozi wa CCM mkoa na taifa?
10.Unajua kuwa Mwang'onda aliungwa mkono na nguvu kubwa sana kuliko hata yako ndani ya chama kitaifa paka ungozi wa mkoa lakini hakuungwa mkono na wana Mbeya?
Ndug yangu nikushauri uusome kwa makini upumbavu wangu hapo juu na ujue unatakiwa kuchagua fungu jema. Kundi linalokuunga mkono halina upepo mzuri kisiasa,unaweza ukawa na malengo mazuri sana na wana Kyela lakini wakakuchukia kwa watu unaoambatana nao.
Kumbuka Obama alipohusishwa na wanaharakati weusi au Mchungaji wake alipoanza kuponda race zingine kwamba zilikuwa zinawanyanyasa weusi, aliwakana si kwamba aliukana weusi bali alijua kuwa yeye ni mmarekani na anaomba kura kwa wamarekani wote.
Kama Obama angekuwa ni kizazi cha wanaharakati weusi wa marekani asingeweza kupewa kura na watu wengi kiasi kile. Kumbuka akina Jesse Jackson waligombea miaka ya 80 lakini hawakufika mbali kwani walikuwa wanahisishwa direct na kundi fulani.
Soma alama za majira na nyakati,tafuta washauri wazuri otherwise umeukosa ubunge kabla ya uchaguzi.