Ulikuwa Kyela na Mwakalinga? Vp ishu ya harambee kwa nini iliingia nyongo?
Kwanini usimshauri akagombea sehemu ingine kama vile Mbeya mjini kuliko kujenga uhasama na Dr.?
HARAMBEE YA UMOJA WA VIJANA WA CCM
Mkuu Field80, kwasababu umeuliza wacha nikujibu. Ilikuwa hii niandike baadaye ila kwasababu watu wengi wameulizia wacha nijibu sasa.
Umoja wa vijana wa CCM Kyela walikuwa na harambee yao ambayo nasikia waliiandaa siku nyingi zilizopita. Wakaamua kumualika mtoto wa JK. Huu mwaliko nimeambiwa walimpatia wakati wa uchaguzi wa umoja wa vijana ngazi ya taifa. Mwenyejiti wa vijana Kyela ni Dr Hunter au Dr. Hanta sijajua jina lake vizuri, ndiye alimwomba mtoto wa JK aende Kyela kusaidia harambee kwa ajili ya miradi ya vijana Kyela.
Huyu Dr. hunter nimewahi kuongea naye mara nyingi ila sijawahi kuonana naye uso kwa uso. Ilikuwa nonane naye tarehe 01/08/2009 lakini ilishindikana maana alikuwa down mno baada ya harambee yao kushindwa kufanyika.
Kuna mtu mwingine kaniambia Dr. Hunter alikubaliana na mtoto wa JK juu ya hili wakati mtoto wa JK anapiga kampeni ya mtu aliyetaka awe mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM. Na kama kurudisha fadhila akawaahidi wakimwunga mkono basi na yeye atakuja kuwaunga mkono kwenye Harambee (hili sina uhakika nalo sana). Ilipofika huo uchaguzi ndipo wakampa mwaliko rasmi (sikumbuki uchaguzi wa vijana ulifanyika lini).
Baadaye tarehe ikapangwa kuwa ni Ijumaa tarehe 31/07/2009.
Kyela kuna kumbi chache sana ambazo ni kubwa kiasi cha kuchukua watu zaidi ya 200. Kama nakumbuka vizuri ni mbili tu, huenda kuna zingine. Ukumbi bora zaidi kwa maelezo ya baadhi ya watu ni ule kwenye jengo la Mwakalinga. Pia umezibwa kwahiyo sauti haitoki nje na una AC. Hao vijana wakaamua Harambee yao ifanyike hapo.
Siku hiyo ya Ijumaa Mwakalinga alikuwa kijijini kwao katumba na kulikuwa na mkutano wa kimila ambao uliandaliwa kumpa baraka mwanao. Hakuwepo pale mjini wala hakuwa na mwaliko wa kuhudhuria hiyo Harambee.
Kumbe kuna watu wamechukia kwanini ile Harambee ifanyike kwernye ukumbi wa Mwakalinga. Wakatengeneza majungu huku Dar na kutumia vitisho kwamba huyo mtoto wa JK anaenda Kyela kumpigia kampeni Mwakalinga na kwamba kuna vijana wamejiandaa kumzomea na kumrushia mawe.
Wakapeleka hizo habari mpaka kupitia watu wao walioko usalama wa taifa. Wakakuza jambo mpaka wakubwa wakaona hii inaweza kuleta balaa hasa wakiangalia zile vurugu za yule kijana aliyeuliwa na polisi. Inasemekana ikabidi viongozi waamue haraka haraka kwamba huyo kijana asiende.
Harambee hiyo ikavunjika, vyakula vikadoda, pesa milioni 155 walizotegemea zikawa hazipo tena, kisa wamefanya kosa kufanyia hiyo Harambee kwenye ukumbi wa Mwakalinga. Ndio siasa za Kyela hizo.
Mimi sikuwa na hili wala lile, nimerudi mjini hiyo Ijumaa usiku ndio naambiwa mtoto wa JK hajafika kwasababu mheshimiwa mmoja katia fitina.
Wao waliona wanamkomoa mwakalinga lakini ukweli ni kwamba hiyo center ilishalipwa hata kama mkutano ulivunjika. Kibaya zaidi ameishia kuwaudhi vijana wote ambao ndio walihangaika kwa nguvu na mali kuandaa hiyo Harambee.
Kama kuna mtu anamjua huyo mtoto wa JK basi amwulize kama amewahi hata kusikia jina la Mwakalinga.
Mambo kama haya ndiyo yanatufanya watu wengine tuamue kurudi nyumbani na kujaribu kuleta mabadiliko ya kweli. Mimi sikushangaa maana hata sisi huko nyuma tumeshafanyiwa visa kibao. Kuna bank walitaka kufungua branch pale kwa Mwakalinga, mhusika huyo huyo akaenda kutumia undungu na mtoa maamuzi ili kuzuia.