Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
This is typical Kayanza's words.....yale yale tunawalaumu wanasiasa.....sheria hazifuatiwi kinachobakia ni tisha toto....
Mtanzania, tunashukuru kwa kutupa yaliyojili Kyela wakati wa ziara ya Mbunge Mtarajiwa Mwakalinga.KUGOMBEA AU KUTOKUGOMBEA
Tulipokuwa Ngorongoro crater tukapigiwa simu na watu mbalimbali kwamba Malafyale kaandika habari ndefu kwamba Mwakalinga yuko Kyela na anaendesha kampeni na kaandika na mengine mengi. Akawaambia hayuko Kyela na badala yake yuko Ngorongoro na familia baada ya kutoka Manyara na kisha kulala Karatu jimboni Dr. Slaa.
Baadaye tukapigiwa simu na mhusika mmoja wa JF, akatusomea article yote. tukamwambia 90% ni uwongo maana mwandishi akakosea hata kijiji anakotoka. Tukawambia hiyo habari ni uwongo kwa zaidi ya asilimia 90 na waamue nini cha kufanya.
Sisi tulienda Kyela Kyela Jumapili tarehe 26/07/2009 na kuanza kukutana na wananchi siku ya Jumatatu na kuwajulisha juu ya dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge mwakani.
Tunashukuru wananchi ambao tulikutana nao na wengi wakashangaa kuona Mwakalinga mwenyewe kumbe ni kijana, hana umbo kubwa, na hana maringo.
Kila tulipopita hicho kitu kilikuwa kinajitokeza. Watu walitegemea kuona bonge la jitu baada ya kulisikia jina lake kwa muda mrefu, lakini wakakuta ni mtu wa kawaida kabisa.
katika utambulisho wake Mwakalinga alikuwa anazungumzia jinsi migogoro ya watu wawili inavyoathiri Kyela, elimu duni wilayani ambayo matokeo yake ni huko mbeleni Kyela kutokuwa na vijana wake wasomi kama ilivyo sasa, kilimo duni, na huduma mbovu za afya.
Pia alikuwa anaelezea jinsi Kyela wanavyoshindwa hata kumtumia mkuu wa majeshi anayetoka Kyela ili kuwahamasisha vijana kwamba wakijituma kwenye shule siku moja wanaweza kuwa kama Mwamunyange, badala yake wanampiga vita hata yeye mpaka kukwamisha baadhi ya shughuli zake pale wilayani. Akifanya jambo wanadai eti anataka kugombea ubunge. Alikuwa anawaambia wananchi kwamba kama kuna wana Kyela wanataka kuleta maendeleo nyumbani ili baadaye wagombee ubunge basi waje tu na yeye atafurahi hata wakiwa 1000.
Pia sehemu zote alikuwa anawaambia kwamba yeye sio mwanasiasa na hataki kuiga tabia za wanasiasa; kwamba yeye strength yake iko kwenye kuchapa kazi, kuwajibika na kuwaambia wananchi ukweli badala ya kuwadanganya majukwaani.
Kumbe siasa nayo ni kazi ngumu sana maana vikao vilikuwa vinaanza saa moja asubuhi mpaka saa sita usiku. Kwa siku tano tukaweza kutembelea kata 19 kati ya 21.
Hayo ndiyo ya Kyela ndugu zangu, ndiyo yamewachanganya watu, badala ya kwenda huko wilayani wakazamia JF na kueneza kila aina ya kashfa.
Nikikumbuka mengine basi nitawaandikieni.
Huko tumeambiwa ahadi za wanasiasa mwaka 2005 mpaka unaficha uso, hivi kweli ni muhimu kuongea mambo ambayo unajua kabisa huwezi kuyatekeleza?
Binafsi nimefarijika na mengi niliyoyaona Kyela, opportunities ziko nyingi ila na umaskini nao umejaa.
Nawahakikishieni mwakani 2010 Kyela kutakuwa na mpambano wa nguvu. Mwakalinga yuko focused na anajua anataka kufanya nini Kyela. Naamini mshindi Kyela itakuwa ni demokrasia kama wahusika wataamua kupambana kwa hoja.
Kyela hakuna vurugu kabisa tofauti na watu wanavyoamini huku JF au Dar. Sisi tuliambiwa eti tutazomewa na kupigwa mawe. Lakini badala yake tuliona vijana wanaotaka kuongea na kutaka kukujua zaidi. Siku ya kwanza tukakuta kijijini wameandaa ulinzi lakini tukakataa na kuwaambi hatudhani kuna watu wanataka kutudhuru. Baada ya ku access security situation na kuona ni wanasiasa wanaikuza tu, baada ya siku ya pili tuliweza kutembea kwa miguu kwenda sehemu mbalimbali pale mjini.
karibuni Kyela wakuu, hakuna vurugu kabisa. Yale ya kifo cha yule kijana yangeweza kutokea sehemu yoyote. Mimi namlaumu Mwakipesile na mkuu wa wawili kwa kushindwa kwao kusimama na kusikiliza malalamiko ya wale vijana. Wakati mwingine solutions za hii migogoro mikubwa ni kuwapa nafasi ya kutoa dukuduku zao. Hata kama walikuwa busy, bado wangeweza kupanga kukutana na wawakilishi wa hao vijana hata jioni.
Baadaye ngoja nikatengeneze chai ya bosi.
Tunashukuru wananchi ambao tulikutana nao na wengi wakashangaa kuona Mwakalinga mwenyewe kumbe ni kijana, hana umbo kubwa, na hana maringo.
Na wewe hueleweki. Mara oooh ngoja nikalale...mara ooh ngoja nikatengeneza chai....what the hell bruh? Make up your damn mind
Haya bwana. Unataka LIGI na mimi?!?
Unajua vizuri ligi naweza.
may be ndio huyu msela....
SteveD tumwangie data..najua sasa hivi uko page ya 2 kwenye MS word....
MKUU ASANTE KWA HII PICHA, INAKUMBUSHA MENGI YA HUYU JAMAA A.K.A GEORGE BEER, HAPO MJINI READING (UK) NA MANCHESTER, WADAU WENGI WANAMJUA HUYU JAMAA KABLA HAJAENDA SCANDINAVIA COUNTRY NA KUMPATA KIDOSHO .....!!! NA KUMPA MAKARATASI.....Mhhh MIE UDAKU SIPENDI!!!!!, SIO MBAYA WAZUNGU KUMFADHILI LAKINI NA UHAKIKA HIYO KYELA ITAJAA MAKOPO YA BIA ZA STELLA BADALA YA HIZO LAPTOPS, TUJADILI KUHUSU WASIFU WAKE WA KUWA KIONGOZI BORA AMA BORA KIONGOZI, STAY TUNED MORE NEWS TO COME!!!!!
Labda unaweza na wengine kugombea kombe la mbuzi....na mimi huwezi.
MKUU ASANTE KWA HII PICHA, INAKUMBUSHA MENGI YA HUYU JAMAA A.K.A GEORGE BEER, HAPO MJINI READING (UK) NA MANCHESTER, WADAU WENGI WANAMJUA HUYU JAMAA KABLA HAJAENDA SCANDINAVIA COUNTRY NA KUMPATA KIDOSHO .....!!! NA KUMPA MAKARATASI.....Mhhh MIE UDAKU SIPENDI!!!!!, SIO MBAYA WAZUNGU KUMFADHILI LAKINI NA UHAKIKA HIYO KYELA ITAJAA MAKOPO YA BIA ZA STELLA BADALA YA HIZO LAPTOPS, TUJADILI KUHUSU WASIFU WAKE WA KUWA KIONGOZI BORA AMA BORA KIONGOZI, STAY TUNED MORE NEWS TO COME!!!!!
MKUU ASANTE KWA HII PICHA, INAKUMBUSHA MENGI YA HUYU JAMAA A.K.A GEORGE BEER, HAPO MJINI READING (UK) NA MANCHESTER, WADAU WENGI WANAMJUA HUYU JAMAA KABLA HAJAENDA SCANDINAVIA COUNTRY NA KUMPATA KIDOSHO .....!!! NA KUMPA MAKARATASI.....Mhhh MIE UDAKU SIPENDI!!!!!, SIO MBAYA WAZUNGU KUMFADHILI LAKINI NA UHAKIKA HIYO KYELA ITAJAA MAKOPO YA BIA ZA STELLA BADALA YA HIZO LAPTOPS, TUJADILI KUHUSU WASIFU WAKE WA KUWA KIONGOZI BORA AMA BORA KIONGOZI, STAY TUNED MORE NEWS TO COME!!!!!
Washikaji nipo Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JK Nyerere kumsindikiza mwana JF mwenzetu, George Ambwene Mwakalinga, ambaye alikuwa Kyela kufanya vitu vyake vya kisiasa. Anaondoka sasa hivi na ndege ya Shirika la Ndege la Qatar kwenda London kupitia Doha. Ndege inaondoka sasa hivi(yaani saa saba na nusu).
Hivi majuzi jina la Mwakalinga lilitawala vyombo vya habari nchini kwa kuwania kiti cha ubunge cha Kyela kinachoshikiliwa na Mbunge maarufu nchini, Dk. Harrison Mwakyembe. Anatarajiwa kufika Doha jioni na boarding pass yake inasema ataondoka Doha saa sita usiku hadi Heathrow, London ambapo mshikaji ataingia mapema alfajiri kesho.
Mimi nilimpokea Mwakalinga alipoingia nchini wiki mbili zilizopita na nilikuwa miongoni mwa wale waliomsindikiza katika kujinadi kwa viongozi na wananchi wa Kyela. Ni wajibu wangu vilevile kuwaeleza kuwa anaondoka!
Kalengama
looh! Kazi kweli mwaka huu, huyo mwakalinga wa kwako naona umemtengeneza mwenyewe maana tunayemwongelea sisi hana lolote hata moja katika hayo uliyoweka hapo juu.
kumbe umbo dogo ni moja ya sifa za ubungeKUGOMBEA AU KUTOKUGOMBEA
Tunashukuru wananchi ambao tulikutana nao na wengi wakashangaa kuona Mwakalinga mwenyewe kumbe ni kijana, hana umbo kubwa, na hana maringo.
MWAKALINGA AFUATWA NA PCCB KYELA:
Basi wenzenu tulitumiwa mpaka na PCCB kwamba eti tumeanza kampeni mapema na tunahonga wananchi. Wakatusimamisha njiani, kagua gari, wakakuta tu Mwakalinga na Diary yake ikiwa imeandikwa tunataka maendeleo zaidi sio maandamano zaidi.
Wakasema walipewa habari kwamba sisi tunahonga wananchi na tumejaza pesa kwenye gari letu na kwamba ilibidi wachukue hatua maana ndio kazi yao.
Nakushukuru Mkuu. Huyu Kapela nahisi namfahamu pamoja na kutumia jina tofauti,ni wale wasanii wa kisiasa wilayani Kyela ambao hawana msimamo kabisa. Akija Mwakyembe wapo, Mwakalinga wapo! Wao wanajali fedha tu! Undumila kuwili ni ajira!
Kwa kuwa amenitukana na hajaanza leo huyu jamaa, basi mimi sasa namwaga analysis yangu ya kweli kuhusu huyu "Mbunge Mtarajiwa", potelea mbali. Nataka nimwonyeshe kuwa anayoyajua na mimi nayajua!
Mwakalinga ameweza kupita Kata zote za Kyela kupima upepo. Kwa ujumla upepo si mzuri sana kinyume cha matarajio. Tutake tusitake bado wananchi hawajamkinai Mbunge wao. Aidha, viatu vya Mwakyembe ni vikubwa mno kwa Mwakalinga ambaye ana tabia tofauti kabisa na mpinzani wake: si mcheshi, si mvumilivu wa mawazo tofauti, hana uzoefu wa kisiasa (anaamini mno watu. Anaamini hata matapeli wa kisiasa akina Kapela alimradi wamemsifia), hana upeo wa kutosha wa elimu kufanya tathmini halisia na kusoma alama za nyakati na, kwa kifupi, ana papara.
Alipofika tu, kosa kubwa alilofanya ni kumhakikishia kila mtu aliyekuwa karibu yake kuwa anaungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mwakipesile pamoja na wapambe wake wakubwa: Nawab Mulla, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa na Cornel Apson Mwangonda, aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa. Alidhani kwa kufanya hivyo, atakubalika zaidi!
Amefanya vikao kadhaa na wazee hao ambao kabla ya kuja kwake walikwenda mbio sana kuwatangazia wananchi wa Kyela kuwa Mkombozi wa Kyela Anakuja! Ilibidi Mwakipesile azue ziara ya kiserikali ya uongo na kweli wilayani Kyela mwezi uliopita ili kumsafishia njia George Ambwene Mwakalinga kwa kukutana na madiwani wote wanaomsikiliza, wenyeviti na makatibu wa CCM wa Kata na viongozi wa UVCCM, UWT na WAZAZI wilaya ya Kyela.
Wote mnajua kuwa ziara ya Mwakipesile ikachafuliwa na vurugu za Kyela ambazo kwa kiasi kikubwa zilisababishwa na Polisi na yeye mwenyewe kuendekeza sana visasi hadi kuwajibu vibaya wananchi waliokuwa na hasira. Leo ndiyo mnanijua; nendeni kwa huyo Mbunge wenu mkamlalamikie!
Kundi la Mwakipesile liko kazini siku nyingi, kumsifia Mwakalinga na kumponda Mwakyembe. Linapewa posho nzuri sana. Kampeni hii inaendelea Kyela, Mbeya na Dar es Salaam. Kyela inaongozwa na jamaa mmoja wanamwita Makete; Dar es Salaam na jamaa anayeitwa Mwanjala na Mbeya na Mkuu wa Mkoa mwenyewe. Wote tulikutana Kyela alipokuja Mwakalinga! Kama si kweli, basi Kapela abishe!
Katika kampeni hii kila kundi linaongozwa na mwongozo maalum ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambao una hoja 20. Vilevile si siri, Kapela anajua, fedha inatoka kwa Rostam kupitia kwa RC. Ndiyo maana kundi la washikaji ni kubwa. Wengi wao hawamtaki Mwakalinga, kwa sababu hawamjui vizuri, ila wanaitaka pesa yake!
Baada ya muda si mrefu nitawatumia mwongozo huo wa Mkuu wa Mkoa ambao Mwakalinga anaufuata kama biblia, kitu ambacho ni kosa kubwa!