Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

This is typical Kayanza's words.....yale yale tunawalaumu wanasiasa.....sheria hazifuatiwi kinachobakia ni tisha toto....

Wewe na huyu
yo_yo.jpg
mna tofauti gani?
 
Hapa una rap mwenyewe......

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=_rJe2tOS90E"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
KUGOMBEA AU KUTOKUGOMBEA

Tulipokuwa Ngorongoro crater tukapigiwa simu na watu mbalimbali kwamba Malafyale kaandika habari ndefu kwamba Mwakalinga yuko Kyela na anaendesha kampeni na kaandika na mengine mengi. Akawaambia hayuko Kyela na badala yake yuko Ngorongoro na familia baada ya kutoka Manyara na kisha kulala Karatu jimboni Dr. Slaa.

Baadaye tukapigiwa simu na mhusika mmoja wa JF, akatusomea article yote. tukamwambia 90% ni uwongo maana mwandishi akakosea hata kijiji anakotoka. Tukawambia hiyo habari ni uwongo kwa zaidi ya asilimia 90 na waamue nini cha kufanya.

Sisi tulienda Kyela Kyela Jumapili tarehe 26/07/2009 na kuanza kukutana na wananchi siku ya Jumatatu na kuwajulisha juu ya dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge mwakani.

Tunashukuru wananchi ambao tulikutana nao na wengi wakashangaa kuona Mwakalinga mwenyewe kumbe ni kijana, hana umbo kubwa, na hana maringo.

Kila tulipopita hicho kitu kilikuwa kinajitokeza. Watu walitegemea kuona bonge la jitu baada ya kulisikia jina lake kwa muda mrefu, lakini wakakuta ni mtu wa kawaida kabisa.

katika utambulisho wake Mwakalinga alikuwa anazungumzia jinsi migogoro ya watu wawili inavyoathiri Kyela, elimu duni wilayani ambayo matokeo yake ni huko mbeleni Kyela kutokuwa na vijana wake wasomi kama ilivyo sasa, kilimo duni, na huduma mbovu za afya.

Pia alikuwa anaelezea jinsi Kyela wanavyoshindwa hata kumtumia mkuu wa majeshi anayetoka Kyela ili kuwahamasisha vijana kwamba wakijituma kwenye shule siku moja wanaweza kuwa kama Mwamunyange, badala yake wanampiga vita hata yeye mpaka kukwamisha baadhi ya shughuli zake pale wilayani. Akifanya jambo wanadai eti anataka kugombea ubunge. Alikuwa anawaambia wananchi kwamba kama kuna wana Kyela wanataka kuleta maendeleo nyumbani ili baadaye wagombee ubunge basi waje tu na yeye atafurahi hata wakiwa 1000.

Pia sehemu zote alikuwa anawaambia kwamba yeye sio mwanasiasa na hataki kuiga tabia za wanasiasa; kwamba yeye strength yake iko kwenye kuchapa kazi, kuwajibika na kuwaambia wananchi ukweli badala ya kuwadanganya majukwaani.

Kumbe siasa nayo ni kazi ngumu sana maana vikao vilikuwa vinaanza saa moja asubuhi mpaka saa sita usiku. Kwa siku tano tukaweza kutembelea kata 19 kati ya 21.

Hayo ndiyo ya Kyela ndugu zangu, ndiyo yamewachanganya watu, badala ya kwenda huko wilayani wakazamia JF na kueneza kila aina ya kashfa.

Nikikumbuka mengine basi nitawaandikieni.

Huko tumeambiwa ahadi za wanasiasa mwaka 2005 mpaka unaficha uso, hivi kweli ni muhimu kuongea mambo ambayo unajua kabisa huwezi kuyatekeleza?

Binafsi nimefarijika na mengi niliyoyaona Kyela, opportunities ziko nyingi ila na umaskini nao umejaa.

Nawahakikishieni mwakani 2010 Kyela kutakuwa na mpambano wa nguvu. Mwakalinga yuko focused na anajua anataka kufanya nini Kyela. Naamini mshindi Kyela itakuwa ni demokrasia kama wahusika wataamua kupambana kwa hoja.

Kyela hakuna vurugu kabisa tofauti na watu wanavyoamini huku JF au Dar. Sisi tuliambiwa eti tutazomewa na kupigwa mawe. Lakini badala yake tuliona vijana wanaotaka kuongea na kutaka kukujua zaidi. Siku ya kwanza tukakuta kijijini wameandaa ulinzi lakini tukakataa na kuwaambi hatudhani kuna watu wanataka kutudhuru. Baada ya ku access security situation na kuona ni wanasiasa wanaikuza tu, baada ya siku ya pili tuliweza kutembea kwa miguu kwenda sehemu mbalimbali pale mjini.

karibuni Kyela wakuu, hakuna vurugu kabisa. Yale ya kifo cha yule kijana yangeweza kutokea sehemu yoyote. Mimi namlaumu Mwakipesile na mkuu wa wawili kwa kushindwa kwao kusimama na kusikiliza malalamiko ya wale vijana. Wakati mwingine solutions za hii migogoro mikubwa ni kuwapa nafasi ya kutoa dukuduku zao. Hata kama walikuwa busy, bado wangeweza kupanga kukutana na wawakilishi wa hao vijana hata jioni.
Mtanzania, tunashukuru kwa kutupa yaliyojili Kyela wakati wa ziara ya Mbunge Mtarajiwa Mwakalinga.

Ni ukweli usiopingika kuwa wanasiasa wanataka sana huruma ya wapiga kura ili kunusuru ulaji wao hata kama hawajafanya chochote kwenye term iliyopita.

Wanazua mambo ambayo kwa msomi yantia kinyaa ili mradi wakombe tena kura katika uchaguzi ulio mbele yao.

Mtu anatumia ajali aliyopata kama mtaji kisiasa, wakati hiyo inamtokea mtu awae yeyote yule. Hata Kasyupa ilimtokea kipindi cha G55, mbona hakulalama?

Tuko nyuma yako na tunakuombea afya njema 2010 iwe mwisho wa wapiga gita na pambio majukwaani.

kgwamaka
 
Mwafrika;

Hujanielewa ndugu yangu, ninaposema undava undava nina maana tumejitahidi kutetea na kuwajibu vizuri sana, ila kwa maksudi kabisa kuna watu kama Masanilo anaendeleza vijembe, Nyani tunamjua yeye ni mzaha siku zote..ok. Undava undava ni kuwa mtu akijibu kwa kejeli naye anajibiwa kwa kejeli. Akiwa serious naye tunamjibu seriously.

Ndo maana nikakwambia kuwa nakuona upo serious, wasikuchanganye ukaishia kukejeli mara laputopu mara shule mara Duka etc.

Na naomba for sure utambue kuwa hakuna hapa aliyetumwa na Mwakalinga, kila mtu anaandika kile anachokijua na anachoamini.

Baadaye ngoja nikatengeneze chai ya bosi.
 
Tunashukuru wananchi ambao tulikutana nao na wengi wakashangaa kuona Mwakalinga mwenyewe kumbe ni kijana, hana umbo kubwa, na hana maringo.

Mijitu mingine bana hebu angalia kituko hiki Mtanzania anamsemea Mwakalinga unategemea impartiality ? Mtanzania leo amekuwa microphone ya Mwakalinga George acheni ujinga bwana kauze sera si kuendeleza chuki
 
may be ndio huyu msela....
attachment.php


SteveD tumwangie data..najua sasa hivi uko page ya 2 kwenye MS word....


MKUU ASANTE KWA HII PICHA, INAKUMBUSHA MENGI YA HUYU JAMAA A.K.A GEORGE BEER, HAPO MJINI READING (UK) NA MANCHESTER, WADAU WENGI WANAMJUA HUYU JAMAA KABLA HAJAENDA SCANDINAVIA COUNTRY NA KUMPATA KIDOSHO .....!!! NA KUMPA MAKARATASI.....Mhhh MIE UDAKU SIPENDI!!!!!, SIO MBAYA WAZUNGU KUMFADHILI LAKINI NA UHAKIKA HIYO KYELA ITAJAA MAKOPO YA BIA ZA STELLA BADALA YA HIZO LAPTOPS, TUJADILI KUHUSU WASIFU WAKE WA KUWA KIONGOZI BORA AMA BORA KIONGOZI, STAY TUNED MORE NEWS TO COME!!!!!
 
MKUU ASANTE KWA HII PICHA, INAKUMBUSHA MENGI YA HUYU JAMAA A.K.A GEORGE BEER, HAPO MJINI READING (UK) NA MANCHESTER, WADAU WENGI WANAMJUA HUYU JAMAA KABLA HAJAENDA SCANDINAVIA COUNTRY NA KUMPATA KIDOSHO .....!!! NA KUMPA MAKARATASI.....Mhhh MIE UDAKU SIPENDI!!!!!, SIO MBAYA WAZUNGU KUMFADHILI LAKINI NA UHAKIKA HIYO KYELA ITAJAA MAKOPO YA BIA ZA STELLA BADALA YA HIZO LAPTOPS, TUJADILI KUHUSU WASIFU WAKE WA KUWA KIONGOZI BORA AMA BORA KIONGOZI, STAY TUNED MORE NEWS TO COME!!!!!

Hapana,

Huyu anaishi U**** kwa sasa. Huchukua Wazungu na kupeleka Tanzania kwenda ku-invest. Huyu ndiye hasaa George Mwakalinga. Tunashukuru sana kwa picha na tabia za huyu jamaa, mzee wa Vikopo.
Hawa ndiyo watu wa karibu wa mtu na wetu Tanzania na Kyela.

Wee mwenye picha hapo na jina la George Mwakalinga, tumeshakufahamu sasa habari zako. Wenye data za Mwakalinga hapo U***, tafadali tumwagieni hapa na siku ikifika, tutamfunua mwaaa huyu jamaa ambaye hata kwenye hii makala, ameandika sana kwa kutumia jina la M********.
Sasa naunganisha DOTS kwa nini wakati fulani aliambiwa kuwa anaishi kwa msaada wa mkewe Mzungu na kuwa hubeba wazungu Tanzania eti waende waka-invest, kumbe ni tapeli fulani na Mlevi. Wee Mwakalinga, sasa unaanza kuumbuka kidogokidogo. Siku ikifika tutamuanika mwali.
Next step ni kumchambua Nsesi na huyu Mwafrika.

NB: Kumbukeni hii picha ili kampeni zikianza mlinganishe na ya Mgombea wa Kyela.
 
Last edited:
MKUU ASANTE KWA HII PICHA, INAKUMBUSHA MENGI YA HUYU JAMAA A.K.A GEORGE BEER, HAPO MJINI READING (UK) NA MANCHESTER, WADAU WENGI WANAMJUA HUYU JAMAA KABLA HAJAENDA SCANDINAVIA COUNTRY NA KUMPATA KIDOSHO .....!!! NA KUMPA MAKARATASI.....Mhhh MIE UDAKU SIPENDI!!!!!, SIO MBAYA WAZUNGU KUMFADHILI LAKINI NA UHAKIKA HIYO KYELA ITAJAA MAKOPO YA BIA ZA STELLA BADALA YA HIZO LAPTOPS, TUJADILI KUHUSU WASIFU WAKE WA KUWA KIONGOZI BORA AMA BORA KIONGOZI, STAY TUNED MORE NEWS TO COME!!!!!

Umejiandikisha kwa ajili ya Mwakalinga tu!!!

YAAP Mwakalinga yupo juu kweli kumbe
 
MKUU ASANTE KWA HII PICHA, INAKUMBUSHA MENGI YA HUYU JAMAA A.K.A GEORGE BEER, HAPO MJINI READING (UK) NA MANCHESTER, WADAU WENGI WANAMJUA HUYU JAMAA KABLA HAJAENDA SCANDINAVIA COUNTRY NA KUMPATA KIDOSHO .....!!! NA KUMPA MAKARATASI.....Mhhh MIE UDAKU SIPENDI!!!!!, SIO MBAYA WAZUNGU KUMFADHILI LAKINI NA UHAKIKA HIYO KYELA ITAJAA MAKOPO YA BIA ZA STELLA BADALA YA HIZO LAPTOPS, TUJADILI KUHUSU WASIFU WAKE WA KUWA KIONGOZI BORA AMA BORA KIONGOZI, STAY TUNED MORE NEWS TO COME!!!!!

Looh! kazi kweli mwaka huu, huyo Mwakalinga wa kwako naona umemtengeneza mwenyewe maana tunayemwongelea sisi hana lolote hata moja katika hayo uliyoweka hapo juu.
 
Topic imepoteza mvuto. Wabeba mabox wote wapo bize na mabox. Vioja vimekwisha
 
Washikaji nipo Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JK Nyerere kumsindikiza mwana JF mwenzetu, George Ambwene Mwakalinga, ambaye alikuwa Kyela kufanya vitu vyake vya kisiasa. Anaondoka sasa hivi na ndege ya Shirika la Ndege la Qatar kwenda London kupitia Doha. Ndege inaondoka sasa hivi(yaani saa saba na nusu).
Hivi majuzi jina la Mwakalinga lilitawala vyombo vya habari nchini kwa kuwania kiti cha ubunge cha Kyela kinachoshikiliwa na Mbunge maarufu nchini, Dk. Harrison Mwakyembe. Anatarajiwa kufika Doha jioni na boarding pass yake inasema ataondoka Doha saa sita usiku hadi Heathrow, London ambapo mshikaji ataingia mapema alfajiri kesho.
Mimi nilimpokea Mwakalinga alipoingia nchini wiki mbili zilizopita na nilikuwa miongoni mwa wale waliomsindikiza katika kujinadi kwa viongozi na wananchi wa Kyela. Ni wajibu wangu vilevile kuwaeleza kuwa anaondoka!
Kalengama

Kalengamab,

Mheshimu mungu wako, hii taarifa yako ni ya kupika.

Kuna mambo umechemsha ambayo yananifanya niamini unajifanya unatuunga mkono kumbe lengo lako ni kutuchafua.

Hii habari ya mimi kuondoka umeipata kwa kuulizia ratiba ya Qatar Airline. Kuna watu tuliwaambia tunaondoka na Qatar Airline nahisi mmoja ndio
katoa hii habari upande mwingine na kisha wakachunguza ratiba ya Qatar Airline kwa jana.

Kuna ndege kweli ilikuwa inaondoka jana usiku saa sita Doha kuja Heathrow. Sisi tuliondoka na ndege ya saa nane usiku kuja Gatwick airport. Hapo ndipo ulipochemsha ndugu yangu na bahati njia ya mwongo ni fupi.

Nafikiri najua nani kavujisha hii habari. Shame on you brother! kwa umri wako unatakiwa uwe na busara na sio kuingiza siasa za kijinga kama hizi.
 
Minyakyusa ndivyo ilivyo yote hiyo sababu. Ya unyafu(wali) wa bure kutoka kwa mafisadi jitu jiongo linataka kugombea ubunge kwanza kaongopa hapa jf na mkafunga mjadala leo hii bila soni mnakula matapishi yenu .
 
looh! Kazi kweli mwaka huu, huyo mwakalinga wa kwako naona umemtengeneza mwenyewe maana tunayemwongelea sisi hana lolote hata moja katika hayo uliyoweka hapo juu.

ni yupi unayemwongelea? Na una maana gani ukisema "sisi" labda picha ya huyo jamaa iliwekwa kimakosa!!!!
ama kweli mapenzi ni kama donda!!!
 
KUGOMBEA AU KUTOKUGOMBEA

Tunashukuru wananchi ambao tulikutana nao na wengi wakashangaa kuona Mwakalinga mwenyewe kumbe ni kijana, hana umbo kubwa, na hana maringo.
kumbe umbo dogo ni moja ya sifa za ubunge

MWAKALINGA AFUATWA NA PCCB KYELA:

Basi wenzenu tulitumiwa mpaka na PCCB kwamba eti tumeanza kampeni mapema na tunahonga wananchi. Wakatusimamisha njiani, kagua gari, wakakuta tu Mwakalinga na Diary yake ikiwa imeandikwa tunataka maendeleo zaidi sio maandamano zaidi.

Wakasema walipewa habari kwamba sisi tunahonga wananchi na tumejaza pesa kwenye gari letu na kwamba ilibidi wachukue hatua maana ndio kazi yao.

"tunataka maendeleo zaidi sio maandamano zaidi." kumbe hii ndio slogan ya mwakalinga

embu tueleze maandamano unamaanisha nini?? au ni kwa ajili wana kyela walivyoandamana kum support DR

embu tueleze maendeleo unamaanisha nini?? au mabilioni binafsi na malaputopu

embu tufafanulie slogan "yako" tafadhali
yako - sisemi kama wewe ni mwakalinga, bali wewe kama mtu wa karibu wa mwakalinga ambaye ulikuwa kwenye msafara wake (haya ni madai yako na sio mimi)
 
Nakushukuru Mkuu. Huyu Kapela nahisi namfahamu pamoja na kutumia jina tofauti,ni wale wasanii wa kisiasa wilayani Kyela ambao hawana msimamo kabisa. Akija Mwakyembe wapo, Mwakalinga wapo! Wao wanajali fedha tu! Undumila kuwili ni ajira!

Kwa kuwa amenitukana na hajaanza leo huyu jamaa, basi mimi sasa namwaga analysis yangu ya kweli kuhusu huyu "Mbunge Mtarajiwa", potelea mbali. Nataka nimwonyeshe kuwa anayoyajua na mimi nayajua!
Mwakalinga ameweza kupita Kata zote za Kyela kupima upepo. Kwa ujumla upepo si mzuri sana kinyume cha matarajio. Tutake tusitake bado wananchi hawajamkinai Mbunge wao. Aidha, viatu vya Mwakyembe ni vikubwa mno kwa Mwakalinga ambaye ana tabia tofauti kabisa na mpinzani wake: si mcheshi, si mvumilivu wa mawazo tofauti, hana uzoefu wa kisiasa (anaamini mno watu. Anaamini hata matapeli wa kisiasa akina Kapela alimradi wamemsifia), hana upeo wa kutosha wa elimu kufanya tathmini halisia na kusoma alama za nyakati na, kwa kifupi, ana papara.
Alipofika tu, kosa kubwa alilofanya ni kumhakikishia kila mtu aliyekuwa karibu yake kuwa anaungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mwakipesile pamoja na wapambe wake wakubwa: Nawab Mulla, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa na Cornel Apson Mwang’onda, aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa. Alidhani kwa kufanya hivyo, atakubalika zaidi!
Amefanya vikao kadhaa na wazee hao ambao kabla ya kuja kwake walikwenda mbio sana kuwatangazia wananchi wa Kyela kuwa “Mkombozi wa Kyela Anakuja”! Ilibidi Mwakipesile azue ziara ya kiserikali ya “uongo na kweli” wilayani Kyela mwezi uliopita ili kumsafishia njia George Ambwene Mwakalinga kwa kukutana na madiwani wote wanaomsikiliza, wenyeviti na makatibu wa CCM wa Kata na viongozi wa UVCCM, UWT na WAZAZI wilaya ya Kyela.
Wote mnajua kuwa ziara ya Mwakipesile ikachafuliwa na vurugu za Kyela ambazo kwa kiasi kikubwa zilisababishwa na Polisi na yeye mwenyewe kuendekeza sana visasi hadi kuwajibu vibaya wananchi waliokuwa na hasira. “Leo ndiyo mnanijua; nendeni kwa huyo Mbunge wenu mkamlalamikie!”
Kundi la Mwakipesile liko kazini siku nyingi, kumsifia Mwakalinga na kumponda Mwakyembe. Linapewa posho nzuri sana. Kampeni hii inaendelea Kyela, Mbeya na Dar es Salaam. Kyela inaongozwa na jamaa mmoja wanamwita Makete; Dar es Salaam na jamaa anayeitwa Mwanjala na Mbeya na Mkuu wa Mkoa mwenyewe. Wote tulikutana Kyela alipokuja Mwakalinga! Kama si kweli, basi Kapela abishe!
Katika kampeni hii kila kundi linaongozwa na “mwongozo maalum” ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambao una hoja 20. Vilevile si siri, Kapela anajua, fedha inatoka kwa Rostam kupitia kwa RC. Ndiyo maana kundi la washikaji ni kubwa. Wengi wao hawamtaki Mwakalinga, kwa sababu hawamjui vizuri, ila wanaitaka pesa yake!
Baada ya muda si mrefu nitawatumia mwongozo huo wa Mkuu wa Mkoa ambao Mwakalinga anaufuata kama biblia, kitu ambacho ni kosa kubwa!

Kalengamab,

Kumbe ndiko huku ulikuwa unakuja? Nimekujua mkuu wangu. Namshukuru mungu wangu kwa kuniepusha kukutana na wewe siku ya Jumanne.

Pamoja na kwamba ni mpambe wa Mwakyembe, nilifikiri kwa umri wako umekubali kwamba siasa si uadui lakini kumbe mambo yale ya kwenye mipira ya Yanga na Simba bado unataka kuyatumia kwenye siasa?

Ulipokosea ni pale uliposema umenisindikiza airport. Imebidi nipitie list yangu yote ya kila mtu ambaye nilimwambia naondoka na ndege gani. Kumbe kuniuliza naondoka na ndege gani lengo lilikuwa baadaye utunge habari ukijifanya unaniunga mkono na baadaye kunigeuzia kibao?

Pole sana ndugu yangu na mungu akusamehe sana!
 
Back
Top Bottom