Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM


MWAKYEMBE KUHUTUBIA UWANJA WA MWAKANGALE LEO MCHANA.

Mbunge wa Kyela dr Harison Mwakyembe leo atahutubia wananchi wa kyela katika uwanja wa mpira wa miguu wa Mwakangale hapa mjini kyela.
Dr Mwakyembe alifika jana usiku na kulala nyumbani kwao Tukuyu na Baadaye leo ataingia mjini kyela na kuhutubia wananchi wa kyela.

Kama alivyo mheshimiwa mwakyemba,ameongozana na waandishi wa habari wa mengi.wandishi wa magazeti ya majira na Tanzania Daima.

Hivi karibuni, Dr Mwakyembe,amekuwa akiyatumia sana magazeti ya mengi katika siasa zake na ata anaposafiri ,anaongozana na wandishi wa magazeti ya mengi. Mengi ambaye anajulikana kama fisadi nyangumi na mmoja kati ya mafisadi walio saidia kuia Bank ya NBC na baado anamfadhili mtu ambaye anasema anapambana na mafisadi.

Wafuasi wa mwakyembe watasafiri hadi Usare ambako mheshimiwa huyo atapokelewa na kupewa pole na ajali iliyompata.

Moja ya vitu ambavyo,mwakyembe anategemea kuvifanya hapa wilayani ni kupita kila kata na kuchinja ng'ombe yeye na wafuasi wake na uku akisimikwa kama chifu wa kinyakyusa na kupewa pole kwa ajali.Mwakyembe anafanya hivyo ili kujaribu kuuzuia upepo mkali wa siasa unaomkabili hapa wilayani kyela.

Swali kwa wanakyela liko palepale,Je hayo ndiyo maendeleo amabayo wana kyela wanayahitaji?

Nitaendelea kuwajulisha kila kinachoendelea kutokea hapa kyela
 
katika watu weupe juu wewe ni namber one, kwa taarifa tu sisi watu wa Kyela tunajua hata hutubia Mwakangale na unatunga maneno ya kinafiki yasiyo na upeo wa uelewa. hivi kwa nini uandike tu bila kufanya utafiti? Dr. mwakyembe yupo kyela, amelala Ikolo na Matangazo yametolewa atahutubia viwanja vya CCM. Acha kuishi kwa kuambiwa, yaani matangazo yote yale ya Usiku hukuyasikia?wewe Samuel huishi Kyela bali ni kibaraka unaambiwa tu.
 
Mbona hasira je ulikutana na Lowassa Arusha na uwe unauhakika kwani waijua vizuri JF.

AAARRHHGRRRRA@#^&&())((%$@!!#@$%

Mkuu, soma thread mwanzo mwisho kisha uliza maswali, topic ipo page 107 wewe unaulizia maswali yaliyojibiwa page 70.

Kweli tuweni fair jamani watu kama hawa wanakera! ni sawa na jitu cha pombe kikao kinaenda mwishoni lenyewe limechelewa halafu linauliza maswali yaliyokwisha jibiwa!!

FP
 

Shalom,
Urafiki wa Mwanjala na Mwakalinga umetokea wapi? Msiwe mnamwingiza Mwakalinga hata kwenye ugomvi wenu binafsi. Mwanjala ni playboy na mlijua hilo wakati mlipokuwa mnamtumia, alipowageuka mnaanza kulalamika? Mwanjala ana ubinadamu, angekuwa na elimu angetufaa kyela. Hivyo Mwakalinga nasikia ana ubinadamu sana.

Ni sawa na mnavyomtumia Kifukwe pamoja na kujua ufisadi wake, siku akiwageuka mtalalamika? Kwa taarifa Kifukwe mwenyewe kaanza kuweka mguu mmoja kwa Mwakalinga ila mwakalinga hataki uhusiano wowote naye zaidi kusalimiana kama wana Kyela.

Ulitaka Mbeya iwe na mawaziri wangapi? Hayo yalikuwa makosa ya dr kuwaambia wapambe wake na wananchi kwa ujumla kwamba katumwa na jk na atakuwa waziri huku akijua si kweli.

Hapa kyela watu wamegawanyika kati ya ujasiri wa Mwakyembe na upenda maendeleo wa Mwakalinga. Vilabuni kote ni ubishi huo huo. Kama politics za kitaifa hazitaingilia kati basi George atashinda. Dr akiweza kumhusisha George na mafisadi hasa wale ambao sio wana kyela atakuwa na nafasi ya kushinda.

pia kuna suala la apewe awamu mbili, huku vijijini wanafikiri ni sheria kuongoza awamu mbili. George kwa kutambua hilo anasema dr kawa mbunge awamu mbili ikiwemo EA.

Mpambano tayari ni mkali na hii bado ni 2009. Wacha leo tukamsikilize dr na tutawaletea taarifa baadaye.
 

Viwanja vya CCM ndio vinaitwa uwanja wa Mwakangale. Pia jana mpaka saa sita usiku dr alikuwa Tukuyu.
 
Mbona hasira je ulikutana na Lowassa Arusha na uwe unauhakika kwani waijua vizuri JF.

Wee Mzee wa Kinepi.

Siku ukikuwa, wazazi watakuambia kuwa "ukitaka kwenda barazani kwa wazee, usirukie mambo katikati. Tulia na usikilize (usome) kila kitu hadi mwisho na hapo ndiyo uanze kuuliza maswali au kutoa maoni. Unavyorukia haya mambo unakuwa kama huyu kijana wa KIRUSI:

Kutokana na shida za nyumba mjini Moscow na uaghali wake, watu huwa wanalala chumba kimoja mtoto na wazazi. Kijana mmoja aitwaye Sergei alikuwa akilala na wazazi wake. Ila alikuwa na tatizo moja kuwa alikuwa akisinzia darasani. Alipoulizwa akasema "baba huwa anamsumbua kwa maswali ya - Sergei, umelala?" Maswali hayo huulizwa kila baada ya dakika 10. Jamaa wakamuambia kuwa siku moja ajifanye amelala na hapo atafahamu sababu hasa ya baba yake kumsumbua. Siku moja kweli jamaa akajifanya kalala. Baba kaita mara mbili kimya, akasimama na kumwambia mkewe "Tatiana twende jikoni tukaanze shughuli".
Sergei akaruka "ehhh, mwaenda wapi? Shughuli gani hiyo? Tafadhali na mimi nataka kwenda".
 

Naelewa kuwa mafisadi yanakereka sana, tena wanatamani tufe au JF izime ghafla isiwepo. lakini hii ni hali halisi. Na majibu ya kebehi na dhalilishi yanaonyesha mwisho wa fikra na uwezo wa kufikiri je kweli mtaweza kuwajibu watanzania walioteswa na umasikini na wenye hasira na ufisadi, na wizi wa kila aina, au majibu yenu yatakwenda kujenga chuki badala ya kutatua matatizo. Hata Rostam anatamani kuchinja mtu ila ndio hivyo tena

nasoma vizuri sana post hapa, na hata majibu ya Mwakalinga nayasoma pamoja na mashabiki wake, mimi si kwamba nataka mwakalinga awe na wakati mgumu la hasha ila Mwakalinga kajiweka mwenyewe kwenye kikaango.

Mwakalinga akijua kabisa kwamba kundi linalomsaidia ni la kifisadi yeye mwenyewe kalishika mkono. sasa fisadi ni fisadi na unaanzia kuona, kutenda, takrima, msaada, na kurithishwa.

Sasa majibu kwamba Mwakalinga akiwa Arusha Lowassa yupo dodoma hayakidhi.
Swali Mwakalinga alikutana na Lowassa Arusha kwanini huyo mwakalinga asijibu? na kama walikutana walizungumza nini? na Je mwakalinga laikutana na Lowassa Uingereza kati ya 2008-2009 ajibu na aseme je mkutano wao ulihusu nini.

Mkumbuke kwanza huwa wanakataa ila siku zinavyozidi kwenda ukweli na uongo vinasambaa na ufisadi ni ugonjwa lazima utaonekana tu hata ukiuficha vipi. hakuna mwenye nia ya kuonyesha ufisadi wake ila huwa yanawashinda na pua zetu zinanusa vibaya sana.

NA MTAKIA UBUNGE SALAMA NA NI WAJIBU WA WANA-KYELA KUCHAGUA MBIVU NA MBICHI. ila wasi wasi wangu ni pale dodoma tutakapotaka kura za kuchoma mafisadi je ya Mwakalinga itapigwa vipi? kutetea au kukubali wachomwe. eyez on the prize.
 

Asante mzee nitabeba kebehi zako kwa maslahi ya watanzania wengi wasio na uwezo wa Ku-vet viongozi wao. Nitabeba kebehi zako kwa ajili ya taifa langu linaloliwa kila siku na kunyimwa haki ya kujua viongozi wao kabla hawajachaguliwa.

Nitabeba kebehi zako nikijua kwamba ndio njia pekee ya viongozi wasio bora kuzima hoja elimishi na hasa zile zinazoingilia maslahi yao na rafiki zao.

Nitabeba kebehi zako kwa heshima na taadhima nikijua kwamba nasaidia wengi kujua ukweli.

na mwisho nakwambia Asante sana, huniumizi moyo wala hunikatishi tamaa ila najua panapo hasira ukweli huwa karibu kutoka. lets keep pressure up.
 

Hizo zenye nyekundu zinaonyesha au HUJASOMA, na kama umesoma basi HUKUELEWA. And we can't do anything to pull your sox. Kama nilivyosema, ukikuwa utaelewa kijana.

1. Naomba hapa uniwekee ujumbe wowote alioandika MWAKALINGA.

2. Naomba utueleze wakati Mwakalinga yuko Arusha, Lowassa alikuwa wapi?

Ukishindwa, basi nenda kwenye blog ya wabeba mabox (zeutamu style). Huko utakutana na wenzio wengi tu wakiandika kuwa wanasubiri kugawiwa LAPUTOPU na Mwakalinga.
 

Kama ulikuwa makini kwenye post yangu uliyo copy majibu ungeyaona, vaa miwani na usome katikati ya mistari.
 
Huyo Mwakalinga kama kweli katumwa na mafisadi kumng'oa mpiganaji wetu Mwakyembe anapoteza muda na resources zake. Hatutaruhusu nguvu za kifisadi zituondolee mashujaa wetu Bungeni. Kama anadhani ayaweza kufanya zaidi ya kile anachofanya mpiganaji basi aingie ngomani, tunampima. Hii ya kukutana na Lowassa inatia shaka kuhusu uadilifu wake. Halafu kwa nini anatangaza mapema namna hii kuhusu kugombea kwake Kyela. Hapa lazima kuna kitu, sio bure!
 
Dr. Mwakyembe ndio sasa hivi anaingia hapa kwenye ukumbi wa CCM wa wilaya ya Kyela akitokea Tukuyu.

Kuna ngoma vikundi mbalimbali na pia music. Kuna watu around 1000.

Inasemekana walitaka maandamano lakini uongozi wa wilaya umekataa na kusema wanaandama kuunga au kupinga lipi?

Pia kuna magari mawili ya FFU yanazunguka mjini.

Wacha niendelee kufaidi ngoma.
 
naona mwakalinga yupo hapa anajaribu kufuatilia kinachojiri kyela!
 
Kama ulikuwa makini kwenye post yangu uliyo copy majibu ungeyaona, vaa miwani na usome katikati ya mistari.

Mie nimevaa miwani na nikasoma kuwa wakati Mwakalinga yupo Arusha, Lowassa alikuwa DODOMA. Sasa wewe mwenye macho ulisoma nini?
Au ndiyo yale ya wimbo wa "mwenye mapenzi haoni, ingawa macho anayo?"
Kati yetu hapa NANI ANAHITAJI MIWANI?

Jibu hayo maswali mawili. Kwani ni magumu sana, mtoto mwenye macho?

Isije kuwa una macho kama ya ndege, UNAONA UPANDE MMOJA TU.
 

MzeePUNCH,

SI ubadili tu jina na ujiite MZEE JANGALA? Usiharibu hilo jina la LEGEND wa UDSM.
 
Swali Mwakalinga alikutana na Lowassa Arusha kwanini huyo mwakalinga asijibu? na kama walikutana walizungumza nini? na Je mwakalinga laikutana na Lowassa Uingereza kati ya 2008-2009 ajibu na aseme je mkutano wao ulihusu nini.

Kinepi,

Unataka Mwakalinga akanushe mara ngapi ndio ukubali? Mwakalinga hajawahi kukutana na Lowassa mahali popote hapa duniani. Hajawi kupeana mkono na Lowassa, hajawahi kuwa hata chumba kimoja na Lowassa.Hajawahi kuwa hata meter 100 toka alipokuwa Lowassa. Anamwona Lowassa kwenye TV na magazeti tu.

Nakuomba kama unataka ukweli tafuta contacts za Choroa Luxury Safaris ya Arusha na waulize unachotaka kuhusu huyo George na linganisha na maelezo yaliyoko hapa.

Mwakalinga ni mpinzani wa ufisadi kwa vitendo na wala sio maneno matupu. Hushangai husomi hata mmoja anayesema mimi namfahamu Mwakalinga na alifisadi hiki mahali hapa?

Huu ni ujumbe wangu wa mwisho kwenye thread hii na badala yake tunapeleka nguvu zote kule Kyela kuandaa mikakati ya kumkomboa mwana Kyela na hasa vijana kutoka hizi siasa za usanii. Ni mapambano ambayo tunayaamini kwa dhati na hakuna kurudi nyuma. Wanaofikiri watamtisha na kumchafua Mwakalinga ili eti aogope na kuendelea na kazi zake basi mnajisumbua bure, mapambano ndio kwanza yanaanza! Tunatoka kwenye mapambano ya fikra kwenda kwenye matendo na kuwasaidia vijana waweze kujijengea maisha yao ya baadaye.

Karibu Kyela ujifunze siasa za vitendo na maendeleo.
 

- Saafi sana, mkuu tupo pamoja sana ilikuwa apewe uwaziri ila ni Lowassa ndiye aliyeng'oa jina lake dakika za mwisho, mnyonge mnyongeni.

- Otherwise, hoja zako ni nzito sana kwa machache ya huko Kyela ninayoyajua.

Respect.

FMEs!
 

Wakati umefika sasa watanzania tuache upuuzi wa kupoteza muda na rasilimali nyingine za taifa kama polisi kucheza ngoma na kufuja kwa ajili ya kupokea wanasiasa

Enaf is enaf jamani... siasa kila sehemu halafu productivity sufuri!!! Inauma sasa

Na sie tukipumzika kuwajadili hawa wawili na ku-focus kwenye maendeleo labda tutaimprove katika kujenga taifa letu... kwa sasa naona watashinda kuchungulia humu badala ya kufanya vibarua vyao

JF is very addictive
 
Na sie tukipumzika kuwajadili hawa wawili na ku-focus kwenye maendeleo labda tutaimprove katika kujenga taifa letu

- Hoja nzito huwa hahitaji matusi wala kejeli, inajisimaia yenyewe na miguu yake, saafi sana mkuu.

Respect.

FMEs!
 

Mkuu acha utoto. Ulichemsha. Uli quote kipengele cha kurasa ya sabini wakati ilishajibiwa.

Kuna watu wengine mnaandika tu kwasababu sio illegal kuandika. usitumie neno la ufisadi kuficha uwezo wako wa kufikiria.

Imeandikwa: ficha upumbavu wako, ila usifiche hekima yako -- Yoshua bin Sira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…