Kuna uwezekano wa kupata maneno (tape) ya maneno ya Mwakyembe akisema kuwa Mwakalinga yuko jela UK? Itabidi haya yatumike sana wakati wa kampeni. Fanya juu chini upate tape ya maneno hayo.
Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa
Huko Kyela inaonekana wamesha legalize kabisa nini?
Muhimu kutembelea hii Hoteli, if only to take a picture of the banner.
Jana mheshimiwa Mwakyembe alihutubia Ipinda na kuanza kuweka vijembe vyake. Aliwaambia wananchi kwamba Mwakalinga kaletwa Kyela na DC Mashimba na ndio maana rais aliamua kumfukuza kazi huyo DC.
Pia kwenye mkutano wa ndani na wapambe wake aliwaambia Mwakalinga amekamatwa na yuko mahabusu Uingereza na kwamba serikali inafanya mpango wa kumrejesha nchini.
Hizo ndio siasa za Kyela, vipi Mwakalinga uko salama huko? Sikujua na wewe una matatizo kama yule jamaa wa Ze Utamu.
Huyo rais JK yuko sehemu ngapi? Mara anamuunga mkono Mwakalinga mpaka kumtuma mtoto wake kumpigia kampeni, mara kamwondoa DC kwasababu DC anamwunga mkono Mwakalinga. Mara sasa kawaagiza Interpol wamrudishe Mwakalinga TZ.
Kuna mtu anatapatapa kweli kweli!
Mkuu Sikonge,
Najua unachekelea kwakuwa uko kwenye kampeni ya kumnadi Mwakalinga, kwahiyo popote unapompatia upenyo Mwakyembe huchelewi kukandamizia, siwezi kukulaumu kwa hilo kwa kuwa una uhuru na haki ya kumuunga mkono mtu yeyote unayemuona anafaa kuwa mwakilishi wako mjengoni (ingawa mbunge wako toka sikonge ni Saidi Nkumba ambaye vilevile uko against naye).
Lakini pamoja na hayo yote ni ukweli ulio dhahiri kwamba Mwakyembe amefanya kile ambacho wengi hawawezi kuthubutu kukifanya. Tume ngapi za bunge zimewahi kuundwa na zikaishia kuilamba miguu serikali?
Wabunge wangapi wamepewa zawadi ya uwaziri kwa kazi yao nzuri ya kuisafisha serikali?unakumbuka Abdala Kigoda na Wilson Masilingi walivyopata uwaziri enzi za mkapa?
Mtanzania,
Mkuu ndio starehe ya JF kwani uzushi na vijembe ndio mseto unaokubalika..Wa ghana huita FUFU!
Tatizo moja tu ni kwamba tunagombana sisi wenyewe ktk swala dogo sana la Ubunge kiasi kwamba kumeingia uhasama mkubwa baina ya watu hawa...wakati mimi najua fika kwamba Mbunge hawezi kubadilisha kitu ikiwa serikali nzima imeisahau Kyela..That is a fact wakubali wasikubali maendeleo ya Kyela yanategemea huyo mbunge atakuwa na nguvu gani ktk serikali hiyo..
Haya madogo tu yamefikia hapo, sasa fikiria yanayowakuta kina Kibaki, Mugabe na wengineo upate kujua chuki za kiafrika huanzia wapi..Kinachoniuma mimi ni kufikiria tu kwamba hapa watu wanagombea zaidi lile jina la Ubunge -Tittle wakati hawa watu wawili wote ni muhimu kwetu sisi wananchi na ingekuwa vizuri wakajipanga wao kwa manufaa ya umma badala yake chuki inazidi kujengwa wakati Mwakalingfa hata hajarudi Bongo kugombea Ubunge.
Sasa fikiria akirudi na kutangaza itakuwaje, si ndio wataitafuta roho yake kabisa..Na yote hii kwa sababu tu mtu anataka kugombea Ubunge..
Jamani JK anazo nafasi 10 za kuchagua wabunge wake.. Mwakyembe bado anayo nafasi kubwa sana ya kuchukuliwa na JK kama mbunge wa Taifa, na hakuna sababu wala haja ya hawa ndugu wawili tena toka chama kimoja kugombania vipande vya nyama ktk sinia zima la Pilau..
Namwomba sana huyu Mwakalinga na Mwakyembe waondoe tofauti zao hata kama kuna chuki kubwa iliyotokana na Uzembe asili wa Kiafrika (Kujivunia cheo)..akumbuke tu cheo ni dhamana na udugu wetu hautoikani na kabila wala wilaya ni zaidi ya mapana hayo..
Mwita,
Achana na Said Nkumba, yule sasa hivi angelikuwa JELA huko Texas kwa Shilom na mke wake wa Kizungu, tungelikuwa tumeshaanza kumwita DEAD MAN WALKING. Hapo inasubiriwa tu sahihi ya Gavana Bush.
Hayo maneno MEKUNDU ya kwako, umeandika maneno makubwa sana. Kuna vitu tunafahamu ila wewe hufahamu. Kama ungelikuwa mfuatiliaji wa Makala hizi za Mwakyembe, basi pana wakati kama sikosei Mwiba aliliandika. Labda tu nikuambia kwamba "Ndiyo maana Mwakyembe alikuwa na uhakika ataukwaa na yeye UWAZIRI kwa kazi yake, mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2005. Ila Kikwete akamuweka chini. Na hilo sishangai maana kama wengine kama mimi hapa Sikonge napata habari zake, je Mkwere si ana nyingi zaidi?
Mwita, hii ni SIASA. Mwakalinga akishinda, naona nusu ya ushikaji utakufa siku hiyo hiyo kwi kwi kwiiiiiiiii. Naomba Mungu ASIZUZUKE na cheo kama ambavyo hajazuzuka na ELIMU, Kukaa Ulaya, Pesa na kazi nzuri.
I love watanzania, wanaichukia CCM ila wanampenda Mwakyembe!
Tatizo la Mwakyembe amejaa uongo na uzushi mwingi, ndio maana Kikwete alimnyima uwaziri safari zote mbili na hatapa ng'oo kama Kikwete akiendelea kuongoza Tanzania pamoja na kujikombakomba kote.Mkuu Engineer,
Imefika wakati sasa mnaolripoti matukio yanayoendelea kujiri Kyela mje na ushahidi, hii maneno matupu hii ni kujaribu kupakaziana na kuzushiana.
Mi nadhani wale mlio upande wa Mwakyembe pamoja na wale wa kambi ya Mwakalinga mnapotoa shutuma au tuhuma, mara mwakyembe kasema hivi mara mwakalinga kafanya vile, muwe mnaweka na ushahidi. Hii itatusaidia kuendelea vizuri na mjadala kwa kujadili hoja za msingi badala ya kuendelea kujadili ushabiki na majungu.
Naamini tangu tuanze kuwajadili Mwakyembe na mwakalinga kila mmoja amejaribu kuelezea namna anavyomuona nani anafaa kuwa mbunge wa kyela, sasa tufike mahali tuweke pembeni ushabiki na majungu, tuzungumze facts.Vinginevyo tutakuwa tunafanya debate isiyo na maana yoyote kwa maslahi ya kyela na Tanzania kwa ujumla.
Tatizo la Mwakyembe amejaa uongo na uzushi mwingi, ndio maana Kikwete alimnyima uwaziri safari zote mbili na hatapa ng'oo kama Kikwete akiendelea kuongoza Tanzania pamoja na kujikombakomba kote.
Watu wana macho na wanaona nini kinafanyika Kyela na nani anafanya mambo Kyela. Anacha kuchapa kazi muda wake umekwisha sasa anadhani majungu ya uongo yatamuokoa 2010. thubutu.
Kama Mashimba alifukuzwa kwa sababu ya Mwakalinga, je Hawa ngurume alifukuzwa kwa sababu ya nani? Njia ya muongo fupi.
Tatizo wapambe wake wote ni mbumbuu, watamshauri nini? utopia tu.
Anatapatapa ameshindwa pa kutokea na hana jipya, upeo wake kimaendeleo umefikia kikoma.
Kgwamaka
Blah blah tu
tu mara
George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!
Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!
Kwa mujibu wa habari za watu wa Kyela,kama uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM utafanyila leo kwenye kata 15 zinazounda wilaya hiyo, Mwakalinga na Dr Mwakyembe watashinda kata 6 kila mmoja na kata 3 zikiwa ni "swing states".