Mtanzania,
Mkuu ndio starehe ya JF kwani uzushi na vijembe ndio mseto unaokubalika..Wa ghana huita FUFU!
Tatizo moja tu ni kwamba tunagombana sisi wenyewe ktk swala dogo sana la Ubunge kiasi kwamba kumeingia uhasama mkubwa baina ya watu hawa...wakati mimi najua fika kwamba Mbunge hawezi kubadilisha kitu ikiwa serikali nzima imeisahau Kyela..That is a fact wakubali wasikubali maendeleo ya Kyela yanategemea huyo mbunge atakuwa na nguvu gani ktk serikali hiyo..
Haya madogo tu yamefikia hapo, sasa fikiria yanayowakuta kina Kibaki, Mugabe na wengineo upate kujua chuki za kiafrika huanzia wapi..Kinachoniuma mimi ni kufikiria tu kwamba hapa watu wanagombea zaidi lile jina la Ubunge -Tittle wakati hawa watu wawili wote ni muhimu kwetu sisi wananchi na ingekuwa vizuri wakajipanga wao kwa manufaa ya umma badala yake chuki inazidi kujengwa wakati Mwakalingfa hata hajarudi Bongo kugombea Ubunge.
Sasa fikiria akirudi na kutangaza itakuwaje, si ndio wataitafuta roho yake kabisa..Na yote hii kwa sababu tu mtu anataka kugombea Ubunge..
Jamani JK anazo nafasi 10 za kuchagua wabunge wake.. Mwakyembe bado anayo nafasi kubwa sana ya kuchukuliwa na JK kama mbunge wa Taifa, na hakuna sababu wala haja ya hawa ndugu wawili tena toka chama kimoja kugombania vipande vya nyama ktk sinia zima la Pilau..
Namwomba sana huyu Mwakalinga na Mwakyembe waondoe tofauti zao hata kama kuna chuki kubwa iliyotokana na Uzembe asili wa Kiafrika (Kujivunia cheo)..akumbuke tu cheo ni dhamana na udugu wetu hautoikani na kabila wala wilaya ni zaidi ya mapana hayo..
Mkandara,
Hamna cha kuongeza wala kupunguza. Ukianzia ukurasa wa kwanza, na kusoma ujumbe wa ndugu yangu Masanilo, unapata picha ya wazi kabisa TAI walikuwa wanasubiri jina la Mwakalinga litokee JF na walibebe juu juu.
Kwa kuwa hawamfahamu Mwakalinga, na kazi anakofanyia hawawezi kupata data zozote, inawawia vigumu sana kupigana na adui ambaye yeye anawaona mabaya na mazuri yao yote, na wao hawamuoni.
Hii inakuwa kama mtu mwenye kigugumizi akigombana na mtu. Wee unavyompa maneno yake na yeye hawezi kukujibu, hawa jamaa huwa wanakuwa watu wa hasira sana sana.
Wengine tunajitahidi kutoa data za Mwakyembe ambazo zinajulikana. Hatutungi habari zozote kama Malafyale. Pia kuna mtu anaitwa ENGINEER. Huyu bwana kila mtu anamfahamu kuwa ni mtu wa kuongezea chumvi na hampendi Mwakyembe. Nilishasema waziwazi kuwa huyu hata kama angeligombea Lowassa jimbo la Kyela, Mugabe, RA, Chenge nk basi yeye angelisaidia hao watu. Sidhani kama anampenda Mwakalinga ambaye ndiyo kwanza juzi kakiri mwenyewe kuwa "nilishangaa kumuona G. Mwakalinga" -kwa mara ya kwanza.
Sasa Mkandara hebu niambie hili jambo kweli linawezekana? Na hili kaliandika Malafyale na kuja kupewa suport na akina Masanilo, Mwafrika, Shalom, Yo Yo, NN, Nsesi nk nk.
Kwamba Mwakalinga kwa kutumia Nguvu za kiroho:
Alikuwa Arusha na hapohapo: kuwan na Lowassa aliyekuwa Dodoma bungeni, kufungua mkutano Kyela, kutembelea vijiji vya Kyela, kuwa jela UK, kuja kujibu shutuma JF.
Na huyo anayeandika ni Malafyale. Tena aandikia kutoka Texas anapoishi na yeye na kutunzwa na Mkewe wa Kizungu. Hana cha kufanya na muda wote anautumia kutunga Pumba.
Labda tuwafungulie makala maalumu Malafyale na Engineer. Washabiki wawe Masanilo, Shalom na upande mwingine Samwel na Ibombo