Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Ha ha ha ha wewe ndiye ushindwe na ulegee kabisaa kwenye hizo jitihada zako za kuigeuza Tanzania kuwa Tanzanistan. Wewe endelea tu kuwa nyuma ya Mwakalinga kisha uone wanaKyela watakachofanya siku ya kura.


I thought this thread was closed!!!! Anyway...
 
Financial crisis ya UK kiboko.......bora GT kaja kajishindia bandarini akituletea polution bongo
 
Hee,Bwana weeee....stop! stop! stop!.....nikweli hii? hapa ni homa kali ,mpiganaji kazi anayo bajameni...mnasema hajafanya nini?Kwa mawazo yenu mnafikiri jamaa kajitupa kichwa kichwa?uzuri mmoja mwakyembe anaelewa vizuri sana kuwa mtu pekee anaweza kumwondoa kyela ni mwakalinga na kama katangaza hivyo basi nyie subirini na pc zenu

Tunajua alianzia vacation yake kule Monduli kwa waziri Mkuu aliyejiuzulu Kwa kashfa ya Rich-monduli!
 
Financial crisis ya UK kiboko.......bora GT kaja kajishindia bandarini akituletea polution bongo

na udini..... GT siku hizi kawa mdini kweli utadhani alipitia Afghanistan kabla ya kuja bongo.
 
Tunajua alianzia vacation yake kule Monduli kwa waziri Mkuu aliyejiuzulu Kwa kashfa ya Rich-monduli!

H aha ha haha,

kazi kweli kweli, jamaa alifanya mambo kwa siri kumbe wana JF wanaingia hadi kwenye CCTV za monduli na kumuona mzee wa richmonduli akitoa shule.

Ama kweli siasa za Tanzania kiboko.
 
Tunajua alianzia vacation yake kule Monduli kwa waziri Mkuu aliyejiuzulu Kwa kashfa ya Rich-monduli!
shem hii ni khatari.....kumbe mwakalinga ile ziara ya mbugani alikuwa monduli kwa mamvi? anyway tumsubiri SteveD aje na waraka......
 
shem hii ni khatari.....kumbe mwakalinga ile ziara ya mbugani alikuwa monduli kwa mamvi? anyway tumsubiri SteveD aje na waraka......

Tunamsubiri aje hapa apinge ama wale wapambe wake tuweke picha zake akiwa na mamvi!
 
Tunamsubiri aje hapa apinge ama wale wapambe wake tuweke picha zake akiwa na mamvi!
tehe tehe tehe lakini ujue lile jina la JF hatalitumia kamwe.....anatusoma.....atakuwa anashauriana na yule m boko haram(kanda2)
 
tehe tehe tehe lakini ujue lile jina la JF hatalitumia kamwe.....anatusoma.....atakuwa anashauriana na yule m boko haram(kanda2)


Namsubiria Engineer wa Mbeya na Mtanzania waje na tetezi zao! Lile jina Kwishney hapa atakuwa na jina lingine...sifa zingine bwana eti ni Mwanzilishi na mfadhili wa JF...so what? Ubunge.....kazi ipo siasa za bongo! Jamaa atakuwa amefulia miaka yote hiyo 18 alokaa Ughaibuni anataka kwenda danganya wapiga kura?
 
kajinyonge ndugu yangu.mwakalinga yuko hatua kumi mbele.akiingia mjengoni kila mwanakyela anakula laptop.
Hivi tunavyozungumza mwakalinga inabidi apewe ulinzi mzito kwani wafuasi wa mwakyembe wameanza kuchanganyikiwa.


Hizi ndio siasa za kibabaishaji tunazokataa. Mambo ya Laptop ndio agenda yake? Watu wanataka kujua agenda, hatuingii kichwakichwa tu kwa sababu huyu ni mwanaJF basi apate tiketi ya kuwa mbunge na kila mtu hapa ampe sapoti. Eleza sifa unazodhani zinaleta mabadiliko Kyela!
 
All is good, ila hii ya kugombea kupitia CCM ndio imeniacha hoi kabisa!!
 
Mtoto wa Kikwete azua balaa kwa Mwakyembe

• Kundi la vijana lapanga kumfanyia vurugu kwenye harambee

na Moses Ng'wat, Mbeya

HARAMBEE ya kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Kyela, mkoani hapa, iliyopangwa kufanyika juzi, imeshindwa kufanyika kutokana na kile kinachodaiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, kushindwa kufika.

Habari za uhakika kutoka ndani ya umoja huo wilayani Kyela, zilidai kuwa Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, akiwakilisha Mkoa wa Pwani, alishindwa kufika kwenye hafla hiyo iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa Kyela Business Center (KDF), kwa madai ya kuwapo kwa kundi la vijana lililopanga kufanya vurugu, kwa sababu za kisiasa.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka Kyela, vinadai kuwa kundi hilo la vijana ambalo halijulikani liko upande gani, lina hofu kuwa harambee hiyo ilikuwa na lengo la kumjenga mmoja wa vijana (jina limehifadhiwa), anayedaiwa kutaka kuwania kiti cha ubunge katika jimbo hilo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mbunge machachari bungeni, Dk. Harrison Mwakyembe.

Kwa mujibu wa habari hizo, Ridhiwani alitarajia kufika katika ukumbi huo majira ya saa mbili za usiku juzi, lakini licha ya vijana kuwapo kwa wingi wakimsubiri mgeni huyo rasmi, hakuweza kutokea na hakuna sababu zilizotolewa na kusababisha harambee hiyo ishindwe kufanyika.

Ilipofika majira ya saa nne usiku, minong'ono ilianza kuzagaa ndani ya ukumbi huo kwamba huenda mtoto huyo wa Rais Kikwete, alishindwa kufika kutokana na taarifa za kiusalama kwamba kuna kundi lililoandaa vurugu ili harambee hiyo isifanyike kwa hofu za kisiasa.

Baadhi ya wanachama wa UVCCM, waliozungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotaja majina yao, walisema baada ya kukwama kufanyika kwa harambee hiyo, kuliibuka makundi mawili ndani ya ukumbi huo, moja likifurahia kutofika kwa Ridhiwani, likiamini kuwa limeshinda, huku jingine likihuzunika kwa kutofanyika kwa shughuli hiyo.

Hata hivyo kundi lililokerwa na kushindwa kufika kwa Ridhiwani, lilielekeza lawama zake kwa uongozi wa jumuiya hiyo kwamba haukuwa na uhakika na kitu walichokiandaa na kwamba hiyo ni ishara ya uongozi huo kushindwa kutekeleza majukumu mbalimbali ya umoja huo, ikiwamo kushindwa kuwashawishi vijana kuachana na siasa za makundi katika wilaya hiyo.

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa UVCCM, mkoani Mbeya, Reginald Msomba, alikiri kuwapo kwa ziara ya Ridhiwani mkoani mwake kwa ajili ya kuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo ya kuchangia fedha kwa ajili ya miradi ya vijana wilayani Kyela.

Alisema yeye kama mwenyekiti wa Umoja huo, alipewa taarifa za ziara hiyo kwamba Julai 31, mwaka huu, alitakiwa ampokee mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa kutoka mkoani Pwani ili kwenda naye Kyela kwa ajili ya shughuli hiyo.

Kwa kweli jambo hilo lilikuwapo ndugu mwandishi, lakini mimi nilishangaa kutompokea mgeni huyo ambaye tulikuwa tuongozane naye hadi Kyela, lakini hadi majira ya jioni hakutokea na mimi nilipewa taarifa za kuelekea huko bila maelezo mengine," alisema Msomba bila kufafanua alikokuwa akipata maelekezo hayo.

Alipotakiwa kueleza sababu za kuahilishwa ghafla kwa ziara hiyo wilayani Kyela, alisema yeye hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa liko nje ya uwezo wake, na kuongeza kwamba watu waliopaswa kulizungumzia ni viongozi wa umoja huo Wilaya ya Kyela.

Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa UVCCM Kyela, Hanta Mwakifuna, kwa njia ya simu kutoka Kyela zilifanikiwa, lakini hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo, hususan sababu za kushindwa kufika kwa mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete.

Mimi sidhani kama kuna haja ya suala hili kupelekwa kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa hata utaratibu wa kumualika hatukuufanya kupitia vyombo vya habari, naomba unielewe kuwa shughuli haikufanyika na sasa tunaangalia jinsi ya kuandaa upya, sihitaji kukuambia kama alifika au hakufika," alisema.

Alipotakiwa kuelezea iwapo kushindwa kufika kwa Ridhiwani kumekwamisha malengo ya umoja huo wilayani Kyela, mwenyekiti huyo alisema lengo lao halikutimia, na kusisitiza kuwa wanajipanga upya kumwita kwa ajili ya harambee hiyo.

Kuhusu tetesi za kuwapo kwa kundi lililopanga kumfanyia vurugu mgeni huyo kwa sababu za kisiasa, Mwakifuna alikanusha taarifa hizo, kwa madai kuwa si sahihi.

Alisema hafikiri kama kuna vijana waliochochewa kufanya vurugu, kwa kuwa kazi hiyo ililenga kufanikisha uchumi wa miradi ya vijana wa chama hicho.
Taarifa hizo ni za kisiasa tu na hazihusiki kwa namna yoyote na kutofika kwa Ridhiwani," alisema bila kutaja sababu nyingine iliyomfanya Ridhiwani kutofika kwenye harambee hiyo.

Alisisitiza kuwa harambee hiyo itafanyika katika tarehe itakayopangwa upya. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, UVCCM wilayani Kyela katika harambee hiyo walitarajia kukusanya zaidi ya sh milioni 155, ambapo hadi kufikia juzi, walikuwa wamekusanya sh milioni 21.9, zilizochangwa na watu mbalimbali, wakiwamo vijana wa umoja huo kutoka kata zote 21 za wilaya hiyo.
 
Kama kawaida utawajua watu weusi kutokana na michango yao kupondana na kukatishana tamaa hata kwa kutafuta taarifa shida, watu wanaanza kukandia ili watu waogope na kukata tamaa, manake hata Mwakyembe alimng'oa Mwakipesile ambaye sasa ni mkuu wa mkoa kama angeogopa inamaana tusingemjua Dr. Mwakyembe.

Kama anataka kugombea hakuna cha ajabu kwani ni haki yake kisheria kama ilivyo haki yako wewe, akaze buti ushindani upo na si wakitoto.

Jamaa yuko na business centre kyela ambayo ina supermarket, ofisi na ukumbi wa kisasa, kituo cha Radio FM na Hotel kwa viwango vya wilayani jengo lake ndio la kisasa zaidi ukilinganisha na watu wengi ambao ni guest kwa kwenda mbele ijapokuwa linatumika kabla halijaisha. Manake kyela kila baada ya nyumba kuna guest mbili. Wengine maisha yetu ya kuungaunga yanatupa elimu kubwa na kuona mengi kama "slum dog millionaire".

Nimeshindwa kutuma picha manake naulizwa URL ya picha ambayo, ningewamwagia labda ingesaidia kwa taarifa zaidi.
 
Hizi ndio siasa za kibabaishaji tunazokataa. Mambo ya Laptop ndio agenda yake? Watu wanataka kujua agenda, hatuingii kichwakichwa tu kwa sababu huyu ni mwanaJF basi apate tiketi ya kuwa mbunge na kila mtu hapa ampe sapoti. Eleza sifa unazodhani zinaleta mabadiliko Kyela!

anataka kuifanya KYELA ni kama India au Rwanda.kauli mbiu yake kila MwanaKyela na Laptop.
Mwafika upo?
 
anataka kuifanya KYELA ni kama India au Rwanda.kauli mbiu yake kila MwanaKyela na Laptop.
Mwafika upo?
this is very low....umeniudhi..naondoa thanks niliokupa kwenye post yako ya kuanzisha thread.....
 
Minyakyusa kwa uongo bwana hata lisoma vipi huyu si alikanusha kuwa hagombei na mkufunga mjadala leo hii bila haya na wapambe wake mnamleta hapa.Mtu mama huyu hafai kwani ni muongo hivi tu kaanza ongopa hata kwenye. Vita vya mafisadi atatuongepea tu.Wanakyela wanawajua wapambe wa mafisadi na hao vibaraka wao
 
Umeme wenyewe uko wapi watu hawali Laptop kaka ama kweli hawa ndio wanataka uongozi Mungu wangu
 
Minyakyusa kwa uongo bwana hata lisoma vipi huyu si alikanusha kuwa hagombei na mkufunga mjadala leo hii bila haya na wapambe wake mnamleta hapa.Mtu mama huyu hafai kwani ni muongo hivi tu kaanza ongopa hata kwenye. Vita vya mafisadi atatuongepea tu.Wanakyela wanawajua wapambe wa mafisadi na hao vibaraka wao
 
Mtanzania bwana! Baadhi yetu tulishamshitukia kwamba ni lifisadi flani hivi kutoka CCM. Lakini akajivunga vunga weee. Sasa imedhihirika. Huwezi kuwazuga watu wote muda wote.
 
Back
Top Bottom