Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

eeh basi mwakalL atakuwa msanii sanii tu.....hivi zile habari za majira ina maana wamezibuni? maana keshaanza kusema ati mwakeY analitumia majira kumchafua.....hivi kwani mwakaL msafi?

Yo Yo

We subiri,Mwakyembe ni big name na unaona anavyoangaika,mambo magumu uko,nyie jiulizeni kwanini ndugu zake wa kyela wanamkimbia..Jamaa wa Kiwira wanasema wakati wa kampeni aliwambia yeye ni mwanasheria mzuri sana na atatatua matatizo yote ya kiwira,Leo hataki hata kufika Kiwira na kama hawezi si akaseme wazee wangu kiwira kazi nzito ndugu yenu nimeshindwa,yeye anawakimbia,Sasa kule wajanja wamewambia wananchi kiwira ni ya wachagga (mama mkapa) si unajua naye mkuu mama ni ukouko kilimanjaro(siasa mbaya)
 
Sidhani kama kuna jipya kwani hao wanakyela wanajua wanataka mtu wa aina gani na ofcourse watakuwa na vigezo vyao. Lakini kama vigezo ni kuwa na Hotel, kutoka UK au kujulikana sana basi hapo wameula wa chuya. Lazima wampime mtu wasije ingiza fisadi wakaanza kulialia hapo baadaye. Dr. Mwakyembe amefanya part yake hivyo watampima kwa aliyoyafanya kwao na kwa taifa. Lakini pia Dr. Mwakyembe na wengine wajiandae visasi uchaguzi ujao vitakuwa vingi hivyo kuna watu irrespective ya mambo mazuri waliyofanya wanaweza pigwa chini kwa mizengwe.
 
Kuna shida gani kwani mtu kugombea! Fujo nyingi zisizokuwa na msaada wowote kwa watanzania na wanakyela wenyewe. Wote wagomee tu, wananchi wataamua ni yupi anaefaa. Kama sheria ya mgombe binafsi itakuwa haijapitishwa basi waende kwa ticket za nra, nld, umd, updp, chadema, cuf, nccr, tlp n.k. Mbona vyote hivi vinaweza tu kuwakutanisha na wananchi kwenye sanduku la kura?

Hii inaonyesha jinsi watanzania wasivyoiweka mbele kwanza Tanzania. Wameibinsafsisha ccm na sasa wamebinafsisha majimbo na sasa ndio wanataka kukamilisha kuibinafsisha nchi. Cha ajabu, hawajeweka mipango madhubuti kuwa sisi wengine watatupeleka wapi! Ngojeni mioto ishike kasi ndio....
 
Sidhani kama kuna jipya kwani hao wanakyela wanajua wanataka mtu wa aina gani na ofcourse watakuwa na vigezo vyao. Lakini kama vigezo ni kuwa na Hotel, kutoka UK au kujulikana sana basi hapo wameula wa chuya. Lazima wampime mtu wasije ingiza fisadi wakaanza kulialia hapo baadaye. Dr. Mwakyembe amefanya part yake hivyo watampima kwa aliyoyafanya kwao na kwa taifa. Lakini pia Dr. Mwakyembe na wengine wajiandae visasi uchaguzi ujao vitakuwa vingi hivyo kuna watu irrespective ya mambo mazuri waliyofanya wanaweza pigwa chini kwa mizengw

Sasa wewe sema Mwakyembe Kyela amefanya nini?
Ofisi ya mbunge kyela iko Kunduchi sijuhi Tegeta,Unasema tutalia baadaye?sasa hivi ndo tunalia,
 
tunamkaribisha kyela lakini atatoka kwa aibu kibao. eti ana miradi kibao, hiyo hotel moja tu ambayo wameshare watu 3?
 
Nimeyasema haya sio kama Mtanzania tu bali pia kama Tuntufye wa Kyela.
 
Wakati mwingine hata ukipata vichwa, tatizo linakuwa ni sera za vyama kwa maana inafika wakati wanalazimika kuhubiri sera za chama na si yale wanayoyaamini wao wenyewe. Kama kungekuwa na utaratibu wa wagombea binafsi, hapo ndipo tungeshuhudia vichwa vikishindana kikwelikweli

Something is better than non mkuu....so bora mgombea akawa kichwa lakini tukawa na kasoro za vyama.....zile personal attributes zitajionyesha tu....watu vichwa huwahapenda unafiki mara nyingi.....! kuliko ukawa na mbumbumbus thena wanahubiri sera za vyama...hapa ndo tunakuwa na patashika!
 
Yo Yo

We subiri,Mwakyembe ni big name na unaona anavyoangaika,mambo magumu uko,nyie jiulizeni kwanini ndugu zake wa kyela wanamkimbia..Jamaa wa Kiwira wanasema wakati wa kampeni aliwambia yeye ni mwanasheria mzuri sana na atatatua matatizo yote ya kiwira,Leo hataki hata kufika Kiwira na kama hawezi si akaseme wazee wangu kiwira kazi nzito ndugu yenu nimeshindwa,yeye anawakimbia,Sasa kule wajanja wamewambia wananchi kiwira ni ya wachagga (mama mkapa) si unajua naye mkuu mama ni ukouko kilimanjaro(siasa mbaya)

Hii ni sumu mbaya sana ya ukabila na inapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote na watanzania wenye kuitakia mema Tanzania.Watu wakianza kufikiria kuwa matatizo ya kwa yanasababishwa na watu wa sehemu fulani/kabila fulani kutazaliwa tatizo ambalo litakuwa halina dawa.

Kwa wenzetu Kenya hali inazidi kuwa mbaya kwa sababu ya siasa za ukabila zilizoanza kama dalili zinazojionyesha hapa na matokeo yake ni watu kuuana kama kuku.Hii sumu inayoanza kumwagwa huko Kyela inapaswa kupigwa vita na wapenda amani kote Tanzania.Vinginevyo hali itakuwa mbaya.

Tatio la Kiwira sio Mama Mkapa ni zaidi ya hapo sasa uchambuzi wa kina usipofanyika kutazaliwa kitu ukabila ambacho sio kizuri kwa taifa letu.
Nawasilisha.
 
JFkatchillin.gif

538npqh.gif

SteveD,

Vipi leo vidole na lips vimebanwa kwa SUPERGLUE mkuu? Talk!Talk!Talk please ....nasubiri comments zako on this mkuu!
 
Wana JF,

Nimeongea na Mwakalinga sasa hivi na kafurahi sana kuwa tunajadili swala lake hapa.

Ni kweli kaahidi Laptops kwa member wote wa JF na kwa watu wote wa Kyela.

Pia kasema atajitahidi sana kuleta WANAWAKE wa Kizungu na Kichina ili watu wasafishe ngozi za watoto wao.

Kila Nyumba ya Kyela itakuwa na Umeme, Karai la TV na TV ndani, umeme wa uhakika.

Kila kwenye nyumba KUMI kutakuwa na UNGO au GOGO ili kuwe na usafiri wa haraka na salama huko Kyela.
Kila mwalimu atapatiwa VX au X6 ili wakawatambie walimu wa majmbo mengine.

Yo Yo amesema atahakikisha anapata LAMBORGINI jeusi ICED!!

Masanilo, utaletewa nyumbani kwako Mwalimu Jumma wa Urambo ili akutimizie shida zako zote na hata ukitaka UBUNGE wa Urambo, basi Sitta hatapata kitu.

Shalom, Manafyale, RazarusMtindi, nk nyie nyote mtajengewa mahekalu Kyela na kila mkipita mwawekewa Red Carpet.

Ili kutimiza haya, Lowassa na Rostam Azziz wamekubali kuuza mali zao zote na kuishi maisha ya ufukara ili muradi Mwakalinga ashinde na wao itakuwa ni kutubu madhambi yao yote waliyowafanyia Watanzania.

Kizuri zaidi ni kuwa hata Mkapa ambaye walikutana na Mwakalinga Zanzibar pia amekubali kutoa asilimia 90% ya mali zake na Anna Mkapa ili kutimiza ndoto hizo juu.

Kwa MATEJA ya Kyela, kaongea na Columbia na atahakikisha analeta unga safi sana kutoka huko kwa kutumia hizo NYUNGO na magogo yatakayowekwa na Mwalimu Jumma wa Urambo. (Masanilo hebu lete ile picha yako). Uzuri wa Ungo ni kuwa hauna control ya mipaka.

Kibunango, litakuja roli la Biaaa, kijana UTAKURA BIYAA hadi ile Karume akuonee wivu.

Kwa leo naishia hapa aliyoahidi Mwakalinga. Nafikiri sasa mwaweza kujadili sana tu juu ya Mwakalinga. Mie imenifurahisha ya wanawake wa Kichina. Duu, huyu ukimpata huku Sikonge, usiku kwenye giza wala taa huhitaji. Na kizuri zaidi ni kuwa unampata kwa bei poa kabisa. Maana Mswahili na kingozi cheupe, huku inabidi utowe Mang'ombe kama 50 hivi ya mahali.

Mwakalinga lazima ashinde, namsubiri Mchina wangu mwaka 2011.

Ili kupigana na AIDS, atajenga mashine za kugawa ndomu kila kwenye baa na klabu za pombe. Juhudi zitafanywa hadi na mama ntilie awe na mashine....

Habari zilizoingia hivi punde ni kuwa Chaves kasema ataweka lami barabara zote za Kyela kama Mwakalinga atashinda. Obama, kaahidi kuleta B52 na kuigawia wilaya ya Kyela. Warusi wao wataleta ANTONOV mbili.
 
Last edited:
mkuu soma alichokisema unless aseme tena hakuwa yeye..

mheshimiwa mwakalinga kawasaidia nini wana kyela mpaka sasa...maana nijuavyo kuleta maendeleo sio lazima uwe mbunge,mkurugenzi au waziri.....yeye keshawafanyia nini wana kyela?
YOYO,
Nadhani ungeitembelea Kyela na ungejua kazi kubwa aliyofanya Mwakalinga tangu enzi za Mwakipesile. Mwakalinga ni Mtanzania na mzalendo wa kweli, kawekeza Kyela na kasaidia ujenzi wa shule za sekondari za serikali Kyela, kapeleka vitabu katika masekondari yote.
Wangapi kati yetu wamefanya hayo? Mwakyembe amefanya nini Kyela? Moto umeanza sasa na ataondoka maana ni nabii wa uongo na hana tofauti na Mafalisayo wa Isarael.
Kgwamaka
 
Huku nyuma tulishasema Mtanzania ndiye Mwakalinga, tukatukanwa, leo hii imedhihiri. Tulitishwa kwamba anazo data za wachangiaji fulani hadi mmoja kutilia mashaka MODs kwamba yawezekana kuna uwezekano ID za watu zinafichuliwa. Naamini JF ni jamvi lenye malengo yake mazito kwa taifa hili kuliko siasa za Kyela, lakini Mwakalinga a.k.a Mtanzania aliligeuza kuwa jamvi la siasa za Kyela, waelewa tulilishitukia hilo na tukaamua kukaa kimya. Naye ID yake ilipobainika kupitia uchangiaji wake akakimbia, najua bado yupo kwa jina jingine anapochangia kwenye siasa za Kyela.

Tatizo haliko kwa yeye kugombea Kyela, la hasha bali ni pale alipogeuza jamvi hili kama jukwa lake la kufanyia kampeni na hata kinachoendelea hapa ni kumpamba aonekane ni mzalendo wa kweli wakati sio kweli, na wakati ukifika itabainika kama ilivyo sasa.

Mwandishi wa Majira hajapika kitu, huyu ni mpambe wake na ndio maana hakutaka waandishi wa habari wengine wahusike. Hivyo hajatafuniwa maneno, kilichoandikwa ndicho alichotaka kitoke, na hapa ndipo udhaifu wake unapojibainisha kwa mara nyingine tena.

Mwakalinga haelewi kuwa utaratibu kura za maoni umebadilika, amekumbatia UVVCCM ambao siku zote chaguzi kwao ni gulio la rushwa, na tayari wameanza kupingana wenyewe kwa wenyewe kila mtu kutaka kuwa karibu naye, na watamla kweli kweli.

Kutokana na kujitambulisha kwake kuwa mwanzilishi wa JF ni lazima aweke bayana humu isije ikawa ndiye MOD mwenyewe, la sivyo JF inapoteza umaarufu wake siku si nyingi, wengine sio wataalamu wa IT, tutakosa imani na jamvi hili kwa sababu litakuwa na sura ya mtu au watu.

Pamoja na kumkaribisha Kyela, yeye pamoja na wapambe wake wanapaswa kufahamu mambo makuu ya muhimu kwa siasa za Mbeya.

1. Unapotaka kugombea ni lazima ujiridhishe kuwa unakubalika na wananchi a sio viongozi wa CCM. Dr Mwakyembe tangu ajitose Kyela hakuwa chaguo la CCM, viongozi wote waliimba wimbo wa Mwakipesile akiwemo shemeji yake aliyekuwa Mwenyekiti CCM Wilaya, lakini aliwabwaga, na hadi leo ngome yake kuu ni wananchi na wala sio viongozi wa CCM.

2. Kuingia kwa gia ya kupigiwa debe na kina Mwakipesile, RA na EL ni mweleka tosha katika siasa za Mbeya, huku hawataki viongozi wa kuchongewa, na hilo ndilo linalomtesa Thom Mwang'onda. Mwakalinga anaeleweka kuwa kapelekwa na Mwakipesile kwani huyo RC anapita akiwaeleza wananchi huko kuwa anawapelekea kijana toka UK, utapigiwaje kampeni na mtu aliyechafuka! Alimpigania THOM kwenye U-NEC akitumia ma DC wote na viongozi wa CCM bado alibwagwa vibaya.

3. Ujasiri na misimamo ni moja ya sifa za kuwa kiongozi Kyela, Mwakalinga ameshaonyesha woga, leo aseme sigombei, akiandikwa kidogo kuwa anagombea anatuma wake wapambe kutishia waandishi wa habari, halafu anakuja tena kutangaza anagombea, hawezi kubalika. Moja ya kete nzito ya Dr Mwakyembe Kyela ni ujasiri, anachukuliwa kuwa taswira hasa ya watu wa Kyela, hasa pale alipoisoma ripoti ya Richmond bila kupepesa macho.

4. Fitina, uongo na inda anavyovionyesha hapa kupitia baadhi ya wachangiaji kuhusu Dr havimsaidii kabisa zaidi ya kumwonyesha kuwa yeye ni mtu wa aina gani. Mara amejenga ghorofa kwa fedha za KDF, mara sijui huko Dodoma kaja na lexus, mara hana nyumba Kyela nk.

5. Kampeni za kuwafanya wana Kyela kuendelea na utegemezi hazimsaidii chochote, e.g kila mtu laptop, nitaibadilisha Kyela kuwa kama Ulaya, nitatoa ajira, zinaeleweka kuwa ni ghiliba za CCM miaka nenda rudi, kwani walishambiwa Maisha bora kwa Kila Mtanzania na hawayaoni.

6. Akumbuke kuwa tunahita kiongozi mwenye mtanzamo wa Tanzania na sio kieneo- Kyela, matatizo ya kitaifa kama vile ufisadi uliopo huko juu ndio ukoma unaoitafuna nchi, tukisafisha huko juu ni wazi huku chini kila kitu kitaenda sawa.

Mwisho niseme kwamba ni mjinga tu ambaye hawezi tambua mchango wa Dr. Mwakyembe kitaifa na jimboni mwake Kyela.

Mwakalinga a.k.a Mtanzania karibu sasa Kyela utugawie hizo laptop nasi tukawauzie wenye kuelewa jinsi ya kuzitumia kisha pesa tukanywee KADANSANA kutoka Malawi!!!!!
 
Teh teh teh aendelee kufanya hayo basi kwani sisi wakazi wa Ipinda, Ikule, Mbaka na Lufilyo hatujaona kitu. Kwani ni lazima tumzawadie ubunge jamani? Acheni kupiga debe kijinga hapa...eti amewekeza mwananchi wa kawaida ananufaika vipi na ufisadi wa Mwakalinga aka Mtanzania?
 
Asante sana Nsesi naona umemaliza kabisa uchambuzi makini sana huu.....maslahi ya taifa mbele.....
 
6. Akumbuke kuwa tunahita kiongozi mwenye mtanzamo wa Tanzania na sio kieneo- Kyela, matatizo ya kitaifa kama vile ufisadi uliopo huko juu ndio ukoma unaoitafuna nchi, tukisafisha huko juu ni wazi huku chini kila kitu kitaenda sawa.

Mwisho niseme kwamba ni mjinga tu ambaye hawezi tambua mchango wa Dr. Mwakyembe kitaifa na jimboni mwake Kyela.

Mwakalinga a.k.a Mtanzania karibu sasa Kyela utugawie hizo laptop nasi tukawauzie wenye kuelewa jinsi ya kuzitumia kisha pesa tukanywee KADANSANA kutoka Malawi!!!!!

Nsesi,

Mwakalinga kasema kuwa hutahitaji kuuza hiyo LAPTOP ili ukanywee KADANSANA la Malawi. Mwakalinga atakujaza MAPESA nyie hadi mtakuwa mnatesa nje ya Tanzania. Sasa kwa nini uiuze tena LAPTOP? Na wewe utapata mbili maana utapata kwa mgao wa KYELA na ukija wa JF pia unapata. Na hapo ongeza Mke wa Kizungu na Kadansana ya Malawi, mwanangu huku waangalia Flat Screen la LG, ama kweli LIFE's GOOD.

Mapesa ya Lowassa ni mengi sana. Nasikia hata Mboma Liyumba wako mbiyoni kumpatia mahela yao ili afanikishe huu mpango. Mambo yakienda vizuri wale ma General wa Burma ( Union of Myanmar) na Mugabe wako mbioni kusaidia katika kampeni. Duuu, jamaa kweli KIBOKO.
 
Teh teh teh aendelee kufanya hayo basi kwani sisi wakazi wa Ipinda, Ikule, Mbaka na Lufilyo hatujaona kitu. Kwani ni lazima tumzawadie ubunge jamani? Acheni kupiga debe kijinga hapa...eti amewekeza mwananchi wa kawaida ananufaika vipi na ufisadi wa Mwakalinga aka Mtanzania?
Naamini kama umekwenda shule utajua maana ya kuwekeza kwenu na faida yake. Kila siku Rais wako anazunguka huku na huko kutafuta wawekezaji, wewe unanufaika vipi? Debe tutapiga na kwenye ukweli tutasema tu. Ajira watu wa Kyela watapata wakiwemo wadogo zako wa Ipinda. Mbona Mwakyembe amepeleka power pool Singida, Watu wa Kyela wananufaika vipi? Huyo sio mwenzetu na hatumtaki na kumdhihirishia hilo tutamkataa kwenye kura subiri kilio. Mwambie afanye kudeclare interest, huo ni ufisadi.
Kgwamaka
 
Debe tutapiga na kwenye ukweli tutasema tu. Ajira watu wa Kyela watapata wakiwemo wadogo zako wa Ipinda.

Haya kaka naona laptops zimekuchanganya....mweka hazina wa Tanzanet kumwangusha Dr Mwakyembe.....hii itakuwa sawa na Osama Bin Laden kuwa Papa wa Roman Catholic, tunasubiria hiyo 2010 tuombe uzima Gwamaka K
 
Duu, U make my day!!! Ha haaaaa

Ni kweli mkuu wangu, hawakawii kukushikisha adabu kwa kuingilia uhuru wa wenzako wa kuwa nyuma ya keyboard.

All in all siasa za pale Kasumulu, Mbugani, Ipinda, Ikolo, Ikombe na Itungi ni ngumu sana. Wananchi wa Kyela wanaweza kuamua suala hili leo na kesho wakaamka na suala jingine tofauti kabisa. Kama unakumbuka, ilishaongelewa sana hapa JF kwamba John Mwakipesile (mkuu wa mkoa wa Mbeya) kawekwa Mbeya si kwa makosa, bali kimkakati ili kuwadhibiti vijana waleta fujo walio nje ya mtandao.
Kimsingi wananchi wa Kyela si wababaishaji kama tulivyo Watanzania wengi, wana msimamo usioyumba, wanaamua wanalofikiri linawafaa na wwanatetea maamuzi yao kwa kila hali. Kama unakumbuka vema, wakati raisi alipozuru Mbeya miezi kadhaa iliyopita walisimama na mabango barabarani na kumuomba aondoke na Mwakipesile "wake" kurudi naye Dar, kwa sababu anaendeleza chuki jimboni badala ya kuunganisha watu. Pamoja na nguvu ya vyombo vya dola kuwadhibiti, ilishindikana kuzuia maandamano yao hadi ujumbe ukamfikia mhe. raisi. Juzi hapa wameandamana hadi kituo cha polisi kutaka maelezo ya kifo cha mwananchi aliyeuawa na polisi kwa sababu ambazo hazielezwi wazi.
Kwa utangulizi huo, naamini kwamba ndugu mgombea mtarajiwa Bw Mwakalinga kashayasoma mazingira ya Kyela na changamoto zake (kama) anaamua kugombea basi amejipima kwamba ana uwezo, nguvu na ari ya kuifanya kazi hii kwa moyo wote, ili kukwamua maendeleo ya jimbo la Kyela kwa ujumla, ikiwemo kuendeleza uvuvi ndani ya ziwa Nyasa (Lumbila na vijiji vya jirani) kilimo cha mpunga, kakao, mihogo, kahawa na iliki ,
ufinyanzi pale Ikombe pamoja na biashara katika ya Tanzania na nchi jirani ya Malawi.
Kimsingi namuunga mkono iwapo malengo yake ni haya na mengine ya kuleta maendeleo.

Kila la kheri
 
Back
Top Bottom