Samwel unayoongea sidhani kama yana ukweli wowote,kwa haraka haraka kati ya madiwani wote Kyela sidhani kuna anayempinga Mwakyembe ukiondoa tu diwani wa hapa Kyela mjini;asiyejua kusoma wala kuandika Mzee Makete na yule wa Katumba-songwe ambako ndiyo nyumbani kwa GAM ndiye wanaoleta matata kwa Mwakyembe!
Ni kweli Mwakyembe hapendwi na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya mzee Mwakasumi na mkuu wa Mkoa Mzee Mwakipesile lkn ana mtaji mkubwa sana wa wananchi walio nyuma yake,na itakuwa ndoto za abunawasi kwa Mwakalinga bila kuwa na strategies pana za kumuondoa Chief!
Ushauri wa Bure kwa Mwakalinga,afanye kampeni za kisasa,haya mambo ya kufuata mwongozo wa Mzee Mwakipesile na hata kuongozana na wapambe wa zamani wa Mwakipesile akina Andy Mwakang'ata na akina Biso hayawezi mfanya amuangushe Mwakyembe,na ataanguka vibaya mno asiporekebisha hali hii!
Mwakalinga kwa sasa anapaswa "awakamate wazee "kama akina Arthur Mwaitenda,Mzee Mwamunyange,General Mwamunyage,Shehe Mwafilango,Mzee Mwaikambo,Mzee Mwanjala,Mzee Ngalawa,askofu wa KKKT-Ipyana,Mzee Mwambogoja,Mzee Mwakalukwa,Mzee Mwakigonja na wazee wengine kote wilayani Kyela ambao wana nguvu sana kimaamuzi kwa vijana wao!
Halafu,Mwakalinga asipoteze muda kwenye kata na vijiji ambavyo hata afanye nini hawezi kumuangusha Mwakyembe,asiende kwenye kata ya Kajunjumele,kata ya Ngonga,vijiji vya Ikolo,kapwili,Ndandalo,na vijiji vya kando ya Matema,maana akienda huko ni kupoteza muda tu ambao anauhitaji kujiimarisha zaidi sehemu anayoungwa mkono au wanayochuana kwa karibu na Mwakyembe!
Na sidhani kama Mwakyembe atamkumbatia Kinanasi eti ndiye awe mpambe wake,kumbuka Samwel huyu Kinanasi hana mvuto wala nguvu ya yeyote kisiasa hapa Kyela,na elewa kuwa Mwakyembe ni hodari sana kwenye kupanga mashambulizi ya kushtukiza,au umesahahu mabomu aliyokuwa anamchapa nayo Mzee Mwakipesile mwaka 2005?