Elections 2010 Kyela elections!

Status
Not open for further replies.

Sikonge;
siasa za Kyela ni ngumu sana,na wa"ngonde"ni watu wenye misimamo yao na hawateteleki wakiamua kitu,na mara nyingi hupiga kura ya umoja ili kumchagua mtu wampendae!

Sikonge;
Wanyakyusa wa Kyela huwezi kuwafananisha na wapiga kura wa majimbo mengi hapa TZ,wana Kyela huwa wanamchagua mgombea anayewasikiliza na kuwakilisha maslahi yao kama walivyomtuma kwenye mihimili ya serikali;katu huwezi pata ubunge Kyela kwa sababu tu umeanzisha Radio kwani sio vigezo vyao vya kuchagua mbunge wao!

Sikonge;
Kyela ilipata hadhi ya Wilaya mwaka 1972 na Mzee Mwakipesile akashinda Ubunge kwa kura chache mwaka 1975.Uchaguzi huo uligubikwa na hisia za "Nyakyusa" na "Ntebela'na kila tarafa kati ya hizo 2 walitaka watoe Mbunge wa Kwanza kuiwakilisha Kyela bungeni!

Mafuriko makubwa yaliyoikumba Kyela mwaka 1979 ndiyo yalikuwa kibali tosha cha kumuondoa Mbunge Mwakipesile wilayani Kyela.Ingawaje wananchi Kyela walimtaka Mbunge wao akatishe vikao vya Bunge na kujiunga nao kwenye kipindi hiki kigumu lkn yeye hakuwasikiliza,na kibaya zaidi akiwa mmoja wapo wa wana kamati ya Bunge akaenda safari kikazi nchini China.Kwenye uchaguzi wa wabunge wananchi walimsusa kwa kumuita kama sio mwenzao na aliwakimbia kwa kwenda"ulaya"wakati wao wana shida,na kijana mdogo kipindi hicho Lumuli Alipipi Kasyupa akashinda kwa urahisi sana!

Sikonge;
Uchaguzi wa mwaka 1980 ulikuwa rahisi sana kwa Kasyupa kwani wote wawili walikuwa wanatoka tarafa moja ya Ntebela,na ikawa rahisi zaidi kwa Kasyupa kushinda akimuhusisha Mwakipesile na kuwatekeleza wana Kyela wakati wa mafuriko hayo.

Sikonge;
Mwaka 1985 Kasyupa akamshinda pia kwa urahisi Mwenyekiti wa chama cha Ushirika Kyela-Kyerucu- Mzee Mwakalukwa ambae pia walikuwa wanatoka tarafa moja ya Ntebela.Ingawaje Mwakalukwa alikuwa na uwezo mkubwa kifedha lkn hakuweza kumshinda Kasyupa kwa sababu wana Kyela walisema"hatujaona kosa la Kasyupa"kama Mbunge wetu.Kimsingi kung'olewa Ubunge Kyela lzm uhusishwe na kutowasikiliza wapiga kura wako!

Sikonge;
Mambo yalianza kumgeukia Mbunge Kasyupa mwaka 1990 kwa sababu ya maombi ya awali ya wana Kyela kuhusu kujitenga na kanisa la Moravian ambapo walidai kila mali ya kanisa hilo inawafaidisha zaidi watu wa Rungwe.Wana Kyela ambao wengi wao ni wafuasi wa kanisa hilo waliandamana mara kadhaa kutaka Mbunge wao ashughulikie suala hilo.Kasyupa akawahaidi kuwapatia kanisa lao huru haraka iwezekanavyo na wana Kyela wakamchagua tena ingawa kwa kura chache toka kwa hasimu wake mkubwa kisiasa Mzee Mwakalukwa;lkn wachambuzi wa siasa za Kyela tulijua kabisa kuwa kama hatafanikiwa kulileta jimbo jipya la Moraviani wilayani Kyela ni heri tu asigombee ubunge mwaka 1995.

Sikonge;
Hadi bunge linavunjwa mwaka 1995,Kyela walikuwa hawajapata jimbo lao la kanisa toka Rungwe,na kibaya zaidi mwaka 1994 mwanaharakati mkuu wa kudai jimbo hilo toka Kyela Mzee Mwakapegere akatiwa kizuizini mwaka,kwa sababu mahabusu kuu ya kuwatunza ipo Rungwe basi mwanaharakati huyu akapelekwa mahabusu yenye ulinzi mkali ya Tukuyu siku si nyingi akiwa mahabusu Tukuyu mwili wake ukaokotwa akiwa amekufa kwenye moja ya vyumba ya mahabusu hiyo,wana Kyela hadi leo wana amini Mwakapegere alinyongwa akiwa kizuizini.Kwenye mazishi ya mwanaharakati huyu yaliyoitingisha Kyela wananchi walikubaliana kuwa kwa vile jimbo halijaja Kyela na mtetezi wao kafa kitatanishi basi Kasyupa asichaguliwe kwa sababu hajawasikiliza na pia wakamlaumu Kasyupa kwa kujiingiza kwenye G55 ili hali bado hajamaliza tatizo lao la jimbo;naam Livingstone Mwakipesile akashinda kwa urahisi sana lkn kwa ombi la kuwaletea wana Kyela jimbo lao toka Rungwe akichaguliwa na yeye akakubali!

Sikonge;
Mfumo wa vyama vingi uliingia kwa kasi wilayani Kyela,na chama cha UNCCR na baadae TLP kilikuwa na nguvu sana wilayani humo,kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 hayati Japhet Mwakasumi alishindwa kwa mbali sana na mgombea wa CCM Mwakipesile lkn kwa ahadi ya kurekebisha suala la kuwaletea jimbo lao.Hadi miaka 5 ya ubunge wake inakwisha wana Kyela wakawa hawaoni dalili yeyete ya kupata jimbo lao na kibaya zaidi wafanyabiashara wa zao la kakao na mpunga wakawa wanadhukumiwa kwa kununuliwa bidhaa zao kwa bei ya chini;hii ilikuwa ni ishara kubwa kuwa siku za Mwakipesile kuwa mbunge zinahesabika!

Sikonge;
Mwaka 2000 kwenye kura za maoni Mwakipesile alishinda lkn akakabiliwa na upinzani mkali toka kwa Japehet Mwakasumi wa TLP;sera ya Mwakasumi ilikuwa ni kuwaomba wana Kyela wamuulize Mwakipesile kwa nini hatimizi ahadi zake,lkn Mwakipesile na timu yake wakajitetea kuwa miaka 5 haikutosha kutimiza ahadi zake na akashinda kwa tofauti ya kura si zaidi ya 500 ktk uchaguzi mkali na mgumu kupata kutokea ktk historia ya chaguzi za Kyela!Ingawaje Mwakasumi alianzisha hadi shule ya Sekondari kijijini Kalumbulu lkn akabwagwa,kwani Kyela hawakupigii kura kwa sababu ya kitu fulani bali wao wanataka mtu wa kuwasikiliza madai yao!

Sikonge;
Baada ya bunge kuvunjwa mwaka 2000 na si tatizo la jimbo la kanisa wala kuimarika kwa soko la kakao na mpunga kupatiwa ufumbuzi ikawa sasa zamu ya Mwakipeile kuondoka,na kibaya zaidi alipoulizwa kwa nini hujatimiza ahadi zako akawa anajibu "serikali haina dini",ndipo Dr Mwakyembe kiurahisi zaidi akashinda kwenye kura za maoni!

Sikonge;
Dr Mwakyembe ni mwanasiasa makini sana,kwanza hakuwahaidi wana Kyela kupata jimbo lao toka Rungwe maana sheria inakataza kufanya hivyo lkn akawahaidi wanaweza kujitenga na kuanzisha jimbo lao from the scratch,na Kyela wakalielewa jambo hilo.Dr Mwakyembe akaja na siasa na balancing yaani akisaidia tarafa hii kitu hiki basi anakuja na msaada kwenye tarafa ingine kwa suala lingine.Kujengwa daraja korofi la Lusungo kwenye tarafa ya Ntebela kumemfanya aonekane kama ni Mbunge anayesikiliza kilio cha wapiga kura wake.Kujengwa kwa barabara ya kasumulu-Itunge,na Ikolo-kasumulu kumemfanye aonekane shujaa kwa wapiga kura wake.Kikubwa zaidi kuongoza timu ya uchunguzi ndani ya Bunge kulikomfanya hadi Waziri Mkuu Lowasa aachie ngazi kunamfanya Mwakyembe aonekane kama mungu-mtu wilayani Kyela;wakati Kasyupa alilaumiwa kujiingiza G55 kama haina maslahi kwa Kyela,wangonde wanampongeza Mwakyembe hadi leo kwa kuiokoa Tanzania toka kwa mafisadi!

Sikonge;
Kimsingi,Dr Mwakyembe kasema mwaka 2015 hatagombea,ingawaje hadi sasa akicheza karata zake vyema za kuwasikiliza wapiga kura wake anaweza shinda kiurahisi zaidi akiamua kugombea mwaka huo!Ni muda muafaka sasa kwa Mwakalinga kuanza kujijenga Kyela hasa kwa kuwasikiliza wapiga kura wanataka nini.Nina wasiwasi kuwa Diwani mpya aliyeshinda kura za maoni wa Kyela mjini,kijana aliyetoka masomoni USA hivi karibuni anaweza kuja mrithi Dr Mwakyembe mwaka 2015 maana ni kijana msikivu kwa wapiga kura wake.Lkn tatizo linakuwa baya kwa Mwakalinga zadi kwani wana-Kyela walimuambia asigombee mwaka huu bali asubiri mwaka 2015 wakati Mwakyembe aking'oka kwa heshima yake mwenyewe lkn hakuwasikiliza;tunarudi pale pale kuwa Mwakalinga sio mtu wa kusikia!

HITIMISHO;
Siasa za Kyela sio siasa za visasi bali ni siasa za kusikilizwa kwa wapiga kura!Kama huwasikilizi wapiga kura wako wanataka nini huwezi shinda uchaguzi wowote wilayani Kyela toka Ubunge hadi udiwani
 
Malyafale,
Nashukuru kwa maelezo marefu namna hiyo kunijibu mimi. Nashukuru kwa heshima yote hiyo. Ila maadamu nimeshajitoa kwenye mjadala, na nilikuwa nisiandike tena, naomba tu uniwie radhi kuwa ntaishia kwenye kusema ASANTE kwa maelefu yako. God Bless!!!

Mungu Ibariki Kyela, Mungu ibariki Sikonge, Mungu ibariki Tanzania.
 
Mambo yote yaliyosemwa juu na Malafyale ndiyo picha kamili ya Kyela niijuavyo mimi. Baada ya yote hayo, kama tunataka kuisaidia Kyela naona tuanze mikakati ya kuzitumia kikamilifu mali za asili za Kyela. Kumekuwa na malalamiko kuwa samaki wamepungua sana ziwani,je kuna utaalamu wowote unaoweza kutumiwa kurudisha population ya samaki? Je tunawezaje kuongeza zao la kakao? Je kuna nijia nzuri ya kusaidia kuuza na kununa mazao kutoka kwa wakulima? Je tuanweza kuwasaidia wakulima wakawa commercial farmers wazuri? Wakati wa cooperatives wakulima wengi walinufaika. Sijui kama mnakumbuka vijana walivyokuwa wakiajiriwa na shamba la kijiji? Can shamba la kijiji now be a large commercial shamba owned by someone who can provide employment to the youth the way shamba la kijiji used to do? Je tunaweza kuendelea kutengeneza sabuni za mbegu za ndilolo na kuziboresha? Michikichi Je? Machungwa? Maembe na mananasi? Je zao la korosho tutawezaje kulirudishia umuhimu uliokuwa nalo miaka ya sabini? Tunaweza kuongeza misitu kwa kupanda ndengele mbugani? Vipi kilimo cha Minazi? Mwishowe kuna njia gani ya kupunguza athari za mafuriko?
 
.
Kweli nimeaamini kyela kuna matatizo.angali huyu anaandika bila kusoma post za wenzake huko mwanzo.

mh. luvishi mbunge wa itope ni hivi;
(a) ccm wilaya kyela ilikuta kuna wanachama wa ccm zaidi ya 25,000 wanaotaka kupiga kura za maoni mwaka huu.

(b)baada ya uchunguzi wa kadi feki na mambo mengine,ni wanachama 7,000 ambao walitakiwa kupiga kura ambao ndiyo wako kwenye madaftari.

(c)tarehe 31/07/2010,mh makamba alitangaza kuwa kila mwanachama wa ccm,atapiga kura.hii ina maana kila mwenye kadi.ata kama umeipata leo.

(d).ndipo kura zimefikia hapo 20,000.na ukizangatia kuwa kyela kulikuwa na kadi nyingi feki.hauon utofauti wa 7000 kwa 20,000?.hicho ndiyo walikuwa wanajadili na sio madudu yako.

soma kwanza post za nyuma kabla ya kukurupuka kama umekamatwa ugoni
 
.

Ama kweli nimeamini mswahili ni mswahili tu.Yaani inatia kinyaa jamaa huyu malafyale na phd yake kudanyanya watu hapa.nani haijui kyela?
kyela wamejitenga kuwa jimbo la morovian mwaka 1992 na muda huo mh kasyupa akiwa mbunge.mwaka 1995 wakati mwakipisile anagombea kwa mara ya kwanza,tayari morovian kyela walikuwa wamejitenga na Mwakijambile akiwa askofu wao wa kwanza.vipindi vyote viwili vya ubunge wa livingstone mwakipisile,tayari movian kyela lilikuwa jimbo.

jamaa huyu amesoma,lakini kila akija hapa ni uongo kwelikweli.please unaweza kubadilika ata kidogo?
 

Haya ni maneno toka kwa timu Mwakalinga ambao so far wamethibitika kuwa ni waongo, warongo, wazushi, wazukushi, warongoro, wadaku, wafitini, watusi (yaani wenye matusi), waroja (wenye viroja kibao), waongo, warongo, and the circle goes on and on and on

Wanatafuta tu sababu ya kusema ila NEC au CC wakimpiga chini Mwakyembe basi waanze hoo kura 10000 zilikuwa feki au ....ohhh ... mchele wa kyela ni kama wa rungwe etesetera etesetera
 
.Sikonge,ata mimi nilkkwenda kulala,sasa imenibidi niamuke.huyu bwana ni muongo kweli kweli.ni mtu mzima,lakini anaandika vitu kama hadithi,looh
 
.
hahahahahaaa.haya bwana.jamaa anapika kweli kweli.
 
.

Ama kweli nimeamini mswahili ni mswahili tu.Yaani inatia kinyaa jamaa huyu malafyale na phd yake kudanyanya watu hapa.nani haijui kyela?

Ona huyu naye ... nani kakuuliza kama malafyale ana PhD?

Au ndo yale yale mnataka kuleta hapa kuwa Mwakalinga alikuwa ameanza kusoma PhD poland na akaamua kuacha ili atengeneze pesa kwanza


Timu Mwakalinga ni rahisi sana kutabirika ... akizidiwa hapa, utaona atakavyoanza kuporosha mitusi kibao dhidi ya members hapa.

Wakati mwingine watu wanataka kuwaonea huruma ila kinyaa kama hiki kinaita mockings kama kawa
 
.
no.mwaafrika.hakuna anayehitaji huruma yako.
tangu mwanzo umemtukana sana mwakalinga.kwa hiyo wewe endelea tu.hakuna anayekukataza.ni uhuru na maoni yako ndani ya jf.umesema mengi sana juu ya mwakalinga kuwa ni mwizi,fisadi nk.keep on going kaka.
 
.
no.mwaafrika.hakuna anayehitaji huruma yako.
tangu mwanzo umemtukana sana mwakalinga.kwa hiyo wewe endelea tu.hakuna anayekukataza.

Ha ha ha ..... yaani ungejua raha niliyo nayo sasa hivi, usingesema chochote.

Kitendo cha Afande Samweli kuingia mtini kinanipa raha saaaaana ...... nimekunywa mirinda mpaka zimekwisha sasa nataka nianze ndovu.

Nikikuona vile unavyojaribu kulia lia hapo juu yaani ninacheka weeeeeeeee.... mpaka mbavu zinauma.

Hebu fikiria kuwa Mwakalinga hakushinda kata hata moja ... yaani hata kata alikozaliwa .. ndugu zake wote wamempiga puuuuuu chini.

Anyway, kwa vile nilimwahidi sikonge kuwa nitakuwa mpole, ngoja tu nikuache kwa sasa angalau upumue kidogo.
 

Jilala ndiye zamani alikuwa anajiita Afande Samwel

Jilala kwanini umebadili jina lako la Afande Samwel na sasa kujiita jina hilo jipya?Mtu makini anayesema anachojua ni kweli hawezi badili jina kwa sababu tu mtu wake kaanguka kwenye kura za maoni;hii inathibitisha sasa kuwa wewe ni mwana siasa wa hovyo hovyo!

Nakujibu hivi Afande Samwel aka Jilala kwa jina jipya;

Vuguvugu la kidini Kyela lilianza mwaka 1990's na hadi Kasyupa anadondoka Kyela haikupata maslahi yake kutoka mchanganuo wa mali za jimbo hilo toka Rungwe.Kujiondoa kwa kyela mwaka 1992 na wala sio Kujitenga kama anavyopotosha Afande Samwel hapa kuliifanya Kyela kupoteza mgao wao toka Rungwe kwa madai kuwa hawatambui kujitenga huko;Kyela ilimtuma Kasyupa na baadae Mwakipesile kudai mafao yao kw anjia ya serikali bila mafanikio!

Jimbo la Ipyana-kyela chini ya Mwakijambire sio walijitenga na Rungwe bali walianzisha kanisa lao jipya kabisa na ndiyo maana hadi leo hamna chochote walichogawiwa toka Rungwe;uwezo wa Dr Mwakyembe kulielezea jambo hili kisheria kumetuliza hali ya kidini jimboni humu!

Afande Samwel wewe ndiye muongo wa kuogopwa kwa kupotosha kila siku watu kuhusu siasa za Kyela hususani kwenye kura za maoni hivi karibuni,bado tunasubiri majibu yetu kuwa kauli zile ulizokuwa unazitoa kuwa Dr Mwakyembe kakaliwa kooni sana na akina Mwakalinga ulikuwa unaziokota wapi?Tafadhali ikiwezekana njoo tu na jina lako na utuombe radhi washika dau wa JF!
 

Jamaaa walikuwa wanaboa sana! Sasa ni amani waendelee kulia lia kama little high school girls on the first date
 
Muda wa malumbano naona umeisha. Tusubiri hukumu ya CC na NEC. Lakini kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho ni kwamba CC na NEC hata kama wana bifu na Dr. Mwakyembe, hawataweza kukata jina lake kwa kuzingatia asilimia ya kura alizozipata. Ikitokea wakafanya hivyo, watakuwa wana risk jimbo kwenda kwa wapinzani kwa kuwa watafanya watu wapige kura ya chuki.

Mleta mada hoja zako zilikuwa zimekaa upande upande na ukaanza kutoa hukumu kwa mgombea mmoja ingawa baadhi ya vipengele naona umemlalia Dr. Mwakyembe.

Katika uhalisia wa mambo, Mwakalinga ameshindwa kwa sababu kubwa zifuatazo na anatakiwa kuzifanyia kazi na kuzirekebisha kwa ajili ya 2015.

Kosa kubwa la Mwakalinga lilikuwa ni timing ya kuamua kwenda kugombea. Timing ilikuwa mbaya kwa kuwa ni mwaka 2008 tu Dr. Mwakyembe alikuwa maarufu sana baada ya sakata la Richmond. Sakata hilo lilimjengea uadui na vigogo wote walioguswa na Richmond na haswa Mh. Lowassa na Rostam Aziz, lakini pia likampa umarufu kwa wapiga kura. Sometimes wapiga kura hawaangalii Mbunge amefanya jimboni, wanaangalia anawakilisha nini Bungeni, je analinda maslahi ya Taifa au ndio anatetea ya kwake? Buzwagi ilimpa umaarufu sana Mh. Zitto, EPA ilimpa umaarufu sana Mh. Dr. Slaa pamoja na hoja nyingine za ufisadi na ndio maana CCM kwa sasa ina kiwewe hawajajua namna ya kujitetea kwa wananchi. Juzi tumemsikia JK akionyesha wazi hofu yake na akasema ni kwa kuwa upinzani wameweka watu makini na siyo wale tuliowazowea siku kwenye chaguzi zilizopita, hapa reference ilikuwa ni Dr. Slaa maana ndiyo chaguo jipya na hawakulitegemea..

Baada ya sakata la Richmond, whatever move iliyokuwa inaendelea kwenye majimbo ya "wapiganaji" ilikuwa associated na kisasi cha hao wakulu na ndiyo maana ukienda Same Mashariki, Simanjiro, Kahama, Nzega, Urambo, Kyela na baadhi ya majimbo ya Mbeya, kelele zilikuwa nyingi sana kwamba waliojitokeza wametumwa na mafisadi. Lakini si wote waliokuwa wametumwa na mafisadi. Kuna wengine walienda independently.

Ukweli unabaki pale pale kwamba Lowassa na Rostam Aziz are very unpopular kwa wananchi wa kawaida wanaotoka nje ya majimbo yao. So, whoever anayetuhumiwa kujihusisha na hao watu automatically anaingizwa kwenye "black book ya wananchi". Nadhani ushahidi uko wazi, kati ya hayo majimbo niliyotaja, ni Nzega pekee ndiko ambako mtu anayehusishwa na EL + RA ameshinda, majimbo mengine yote "wapiganaji" wameibuka kidedea na tena kwa kura nyingi.

Kwa hiyo Mwakalinga amekuwa victim wa kuhusishwa na hoja ya mafisadi kupeleka wagombea kwenye majimbo ya wapiganaji. Kibaya zaidi, hapa hapa JF, mara baada ya kambi ya Mwakalinga kuvujisha habari kwamba ana nia ya kugombea Ubunge, few days later wambea walikuja na habari za udaku kwamba Mwakalinga alionekana Arusha (Lowassa connection?). Huu udaku hauishii hapa hapa JF unasambaa kama moto wa kifuu na una-damage image ya mgombea kirahisi sana. Ndiyo wagombea wengi waliojitokeza kwenye majimbo ya "wapiganaji" walikuwa wanaitwa vibaraka.

Baada ya hilo, ikaingia hoja ya Mwakipesile kwamba yuko upande wa(anamuunga mkono) Mwakalinga. Inajulikana wazi kwamba Mwakipesile ni mwana mtandao na inawezekana amepewa ukuu wa mkoa wa Mby kwa ajili ya maslahi ya wana mtandao. Na unapoongelea mtandao ni sawa na kuwaongelea EL + RA, bado tunarudi kwenye black book.

Sasa ukiangalia mazingira ya siasa za Mby, wabunge wote ambao walikuwa vocal mfano Mwambalaswa, Mpesya na Zambi wote wamepeta na ilisemekana majimbo yao yalikuwa hatarini kupokwa na wana mtandao or pro-Lowassa.

Wale wote ambao walipakaziwa kwamba wana support ya Mwakipesile wameanguka kuanzia kwa Mama Florence Kyendesya, Tom Mwang'onda, Steve Mwakajumilo na ndugu yangu Mwakalinga.

Mwakyembe alishasema watanzania sio mabwege tena, wanaelewa. Hata mtu akidai kwamba Task Force ilitumika kwenye ushindi wa Mwakyembe, kwenye chumba cha kupigia kura Task Force kumlazimisha mpiga kura ampe Mwakyembe kura.

Mtoa mada anasema kwamba TAKUKURU na POLISI hawakuwajibika, swali ni dogo, inaeleweka wazi kwamba Mwakipesile na Mwakyembe ni mahasimu, hivi kweli ni nani ambaye ana nguvu ya kutoa amri kwa polisi na TAKUKURU kwa ngazi ya mkoa? Mkuu wa Mkoa ni Rais wa Mkoa, polisi na PCCB wanachukua amri toka kwake, sidhani kama wangemwacha Mwakyembe na Task Force afanye anavyopenda na ili hali wakijua wazi kwamba wakishampata kwenye rushwa ndo anakuwa kajimaliza mwenyewe. Sikubaliani na hoja hiyo kwamba polisi na PCCB walimwacha Mwakyembe akitanua.

Tufike mahali tukubali ukweli hata kama ni mchungu. Tuungane na kauli ya Steve Mwaka, kwamba mwaka huu alikuwa anajifunza, so ataanza kujipanga upya kwa ajili ya 2015. Ni rahisi sana kumng'oa mbunge aliye madarakani kama hajawajibika kwa kiwango kinachotakiwa, lakini pia ni rahisi sana kumng'oa madarakani mbunge ambaye ameshindwa ku-deliver. Kama Mwakyembe alishindwa ku-deliver this was an opportune moment ya kummalizia mbali.

What is next for Mwakalinga?
Kama bado ana nia ya kugombea come 2015 kuna mambo ambayo anatakiwa kuyafanyia kazi kweli kweli. Kwanza anatakiwa kujipambanua kwamba hana uhusiano wowote na the so called Lowassa + RA. Pili, hata kama ana uhuru wa kukutana na mtu yeyote, lakini ajiweke mbali na Mwakipesile ili asije akapakwa tope la mtandao.

Anatakiwa kuwa makini na wapambe ambao wako hapa JF. Ni rahisi sana kujipa matumaini kwamba JF si wapiga kura, lakini kinachoandikwa hapa ndicho unakuja kukikuta kwenye magazeti na kwenye vijiwe huko Mby. Hawa wanaochangia hapa wengi wao wanajua mengi ya Kyela na wanawasiliana na watu wao kila siku, ni rahisi sana kuharibu image ya mgombea kwa kusambaza pumba ambazo zilikuwa zinaandikwa hapa kwenye mada za Kyela.

Next time ukiwa na nia ya kugombea, wapambe wako hawana sababu ya kuja kutangaza hapa. Ni swala la kuweka mikakati na kuanzaa timu nzuri ya kuangalia nini kinaweza kufanyika. Kampeni ni mikakati na ku-identify watu makini ambao ukiwa nao kwenye nusu ya kata na nusu ya matawi yote una uhakika wa kuongoza kwenye hizo kata. Hao ndio ambao watakuambia nini cha kusema na matatizo ya wananchi ni nini ndani ya kata husika. Lakini kama wapambe wenyewe ni akina Afande Samwel sidhani kama tunaweza kufika, maana hata sentesi zao hazieleweki achilia mbali lugha ya kejeri na matusi.
 
Pamoja na mapungufu ya Mwakyembe na mazuri ya Mwakalinga, ile tofauti ya kura ilikuwa ni kubwa sana kiasi kuwa siamini kabisa kuwa eti task force, kadi za bandia rushwa na mengineyo yalichangia matokeo yale. What happened ni kuwa watu wale walionyesha kuwa mtu wao ni Mwakyembe, full stop. Ukianza porojo watakusikiliza, ukiwapa chakula hawatasusia, ukiwapa hela watapokea, lakini ukiomba kura watakuambia uwasubiri kwenye voting booth, - and I like that. Natamani watanzania wote wangekuwa namna ile.

BTW: Simfahamu Mwakyembe sawasawa kwani wakati ninaondoka UDSM yeye hakuwa mmojawapo wa wanasheria maarfu pale kitivo cha sheria, nadhani labda alikuwa bado ni junior sana. Ila kwa kuangalia utendaji wake bungeni na jinsi alivyosambaratisha wapinzani wake huko Kyela, inaonyesha kuwa ni mtu imara sana.

Kwa wanaomfahamu Mbunge Harrison Mwakyembe, je ana undugu wowote na Mwalimu Gordon Isegelekesye Mwakyembe aliyekuwa anafundisha Advanced Maths Tabora na Mazengo?
 
.

Jamaa huyu katumwa nini.
Jilala ni jilala au magoli na Afande Samwel ni Afande Samwel.Acha kinifananisha mimi na watu
Ndiyo maana ninasema .Wewe ni mpishi tu

Mwaka 1990,Morovian kyela,waliamua kujitenga na kunyang'anya baadhi ya makanisa na Mwaka 1992 chini ya askofu mwakijambile,wakasajili kanisa lao na kujiita morovian kyela na wakati huu mbunge ni kasyupa.

Morovian kyela ni kanisa linalo tambuliwa.Ndiyo maana ninakwambia wewe ni mpishi tu.

Morovian kyela wamepata askofu mpya mwaka jana 2009 na mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa mbeya,Lakin aliwakilishwa na viongozi wa serikali wilaya,ambapo ata mbunge Harison Mwakymebe alikuwepo na alitoa zawadi ya pikipiki kwa askofu mpya.

Acha kuwa mpishi.
 
.

mhhh.yatasemwa mengi sana hapa juu ya mwakalinga.
La mwakalinga kuhusishwa na ubunge,lilianza kabla ata jf haijaanzishwa.ukiangalia post za huko nyuma ni kwamba mwakalinga aliwahi kugombana na mwakipisile,akimshitukia kuwa kwanini anasaidia jamii ya kyela na kwamba pengine anataka ubunge.

Keil,
Kama unakumbukumbu, hoja ya mwakalinga kugombea kyela, haikuletwa na wapambe wa mwakalinga.Ililetwa na Malafyale mwezi july 2009,akisema mwakalinga yupo hotel ya stiva akiongea na waandishi wa habari.Ndipo invisible, alipotujulisha kuwa yeye ameongea na mwakalinga,lakini amesema yuko ngorongoro na familia yake.Waanga, wakaanza kusema kuwa amekwenda kumuona Lowassa.ohoo ni fisadi.

Ukianza kuangalia, taarifa nyingi za mwakalinga,zilikuwa zinaletwa na yeye mwenyewe hapa jf na kukanusha zile za uongo.Wapambe wa mwakalinga wamekuwa wakitetea tu hoja zake,lakini hawajawahi kuwa wasemaji kama wengine mnavyofikiria.Mwakalinga yeye aliwaambia wazi kuwa yeye ndiye mtanzania na taarifa zinazomhusu yeye,alikubali za ukweli na kuzikanusha ambazo anafikiri ni za uongo.

Huyu,Malafyale ni mmoja wapo wa viongozi wa kampuni ya umeme wa upepo,ambayo mwakyembe naye alikuwa mmoja wao na yeye ndiye alileta hizi habari. Kumbuka mwaka jana,kwa mara ya kwanza ,mwakyembe alipohutubia viwanja vya ccm wilaya kyela, baada ya kunusulika na ajali ya gari, malafyale alikuja na hoja kuwa zaidi ya watu 1000 walihudhulia mkutano huo, na barabara zote zilifungwa, kitu ambacho ulikuwa ni uongo mkubwa sana.

Keil,
Haujasoma kuwa baadhi ya mikutano ya kampeni kwa wagombea wa ccm, ilivunjika kwa sababu ya vurugu za task force, kwani polisi hawakuwepo?.Waliliteka gari la mmoja kati ya wagombea na kwamba gari aliondoki mpaka TAKUKURU waje walikague,kwani polisi hawakuwepo?.Kadi zilizokamatwa na baadye wagombea wanne kugomea kampeni kuanza siku ya tarehe 22/07/2010 kwani TAKUKURU, hawakuwepokuzikamata hizo kadi,mpaka zilikamatwa na wananchi?

Kama nilivyoandika mwanzo,kuwa kushindwa ni kubaya sana.Yataibuka mengi sana na ushauri mwingi sana.Mwingine anasema kwenye kampeni za mwakalinga,aliwaweka ndugu zake wote.Mwingine anasema hakuwa na kampeni manager.duh, kazi ipo
 
.

Nakubalina na wewe mkuu
 

Mkuu Jilala,

Kwenye siasa huwa hakuna permanent enemy wala friend, ndio maana Mwakyembe na Mwanjala walikuwa kambi moja mwaka 2005, lakini mwaka huu walikuwa mahasimu. Kwenye siasa kila kitu kinawezekana.

Mimi sijaongelea kutuhumiwa, nimeongelea yale yaliyotokea mbele ya macho ya Mwakalinga hapa JF. Kwa hiyo kwamba alituhumiwa na Mwakipesile na mpaka wakagombana, hilo mimi silijui. Nilichokuwa ninajadili ni yale yaliyotokea kipindi cha kuelekea 2010 hasa baada ya taarifa kuwekwa wazi kwamba Mwakalinga ana nia ya kugombea.

Tuje kwenye hoja ya kuleta mada hapa, unajua mada ikiletwa hapa na ikaanza kujadiliwa na wapambe ndipo maana na umuhimu wa mada huwa unapotea. Ukianza kujadili kitu kwa misingi ya upambe huwezi ukawa na balanced argument. Kwa hiyo dawa yake ilikuwa ni Mwakalinga kuwaomba hao wapambe wake waachane na mada hizo. Kama mtu anafuka pumba kwanini ubishane/ushindane? Itafika mahali watazamaji watashindwa kuelewa yupi mwenye akili timamu na yupi ambaye ana matatizo.

Mfano mdogo, Afande Samweli ametoa maneno mengi sana. Kama mada ya Kadi Fake na ile nyingine ya Mwakalinga kukamatwa zingekuwa bado zipo, ningekuambia kasome maandishi ya Afande Samweli na usome mabandiko ya Malafyale halafu uniambie nani alikuwa mkweli kuliko mwingine na nani alikuwa anajadili mada kiupambe na yupi alikuwa na hoja ambazo ziko balanced.

Unajua ukianza ku-dispute habari alizokuwa anatoa Malafyale na ilihali kuna ushahidi wa mambo aliyoyasema wakati wa kampeni za kura za maoni na kwenye uchaguzi wenyewe na yote yakawa yako sahihi, huwezi kunishawishi niseme kwamba habari alizotoa Malafyale huko nyuma zilikuwa ni za uongo. Kwa hiyo credibility ya Malafyale kwa sasa ni kubwa sana kwa kuwa mambo mengi aliyoyasema kwenye kura za maoni na uchaguzi yamedhihirika kuwa ni ya kweli.

Mwisho umesema kwamba Mwakalinga mwenyewe ndiyo alikuwa analeta taarifa na kukanusha za uongo, labda huko nyuma mwaka 2009, lakini siyo mwaka huu. Kwa hiyo taarifa ya kadi fake ililetwa na Mwakalinga mwenyewe? Ni Mwakalinga pia aliyekanusha kwamba hajakatwa? Ni Mwakalinga mwenyewe aliyekuwa anasema Mwakyembe amekaliwa kooni? Ni Mwakalinga mwenyewe aliyekuwa analeta propoganda za kura za maoni kwamba anaongoza? Labda kama siku hizi Mwakalinga amebadilisha jina hapa JF na inaonekana alikuwa na muda mwingi maana news zake zilikuwa zinamwagika hapa 24/7.
 
Hivi huko Kyela uchaguzi haujaisha tu????????????
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…