Malafyale
Platinum Member
- Aug 11, 2008
- 13,833
- 11,173
Acha wafurahie ushindi huku wakiwa viroho juu wakisubiri NEC na CC iamue. Walau sisi tumeshaanza kufikiria ku-date na akina Nyanso. Wenzetu hata wake zao sasa hivi hawawataki kwa pressure. Hawa ndugu zangu Wanyakyusa bana, kazi kwelikweli. Kama Wahaya walivyo na Baganda, na wao wako karibu sana na Wazambia. Inajalisha unavyoonekana. Mwakalinga na maendeleo yake SUCK.
Sikonge;
siasa za Kyela ni ngumu sana,na wa"ngonde"ni watu wenye misimamo yao na hawateteleki wakiamua kitu,na mara nyingi hupiga kura ya umoja ili kumchagua mtu wampendae!
Sikonge;
Wanyakyusa wa Kyela huwezi kuwafananisha na wapiga kura wa majimbo mengi hapa TZ,wana Kyela huwa wanamchagua mgombea anayewasikiliza na kuwakilisha maslahi yao kama walivyomtuma kwenye mihimili ya serikali;katu huwezi pata ubunge Kyela kwa sababu tu umeanzisha Radio kwani sio vigezo vyao vya kuchagua mbunge wao!
Sikonge;
Kyela ilipata hadhi ya Wilaya mwaka 1972 na Mzee Mwakipesile akashinda Ubunge kwa kura chache mwaka 1975.Uchaguzi huo uligubikwa na hisia za "Nyakyusa" na "Ntebela'na kila tarafa kati ya hizo 2 walitaka watoe Mbunge wa Kwanza kuiwakilisha Kyela bungeni!
Mafuriko makubwa yaliyoikumba Kyela mwaka 1979 ndiyo yalikuwa kibali tosha cha kumuondoa Mbunge Mwakipesile wilayani Kyela.Ingawaje wananchi Kyela walimtaka Mbunge wao akatishe vikao vya Bunge na kujiunga nao kwenye kipindi hiki kigumu lkn yeye hakuwasikiliza,na kibaya zaidi akiwa mmoja wapo wa wana kamati ya Bunge akaenda safari kikazi nchini China.Kwenye uchaguzi wa wabunge wananchi walimsusa kwa kumuita kama sio mwenzao na aliwakimbia kwa kwenda"ulaya"wakati wao wana shida,na kijana mdogo kipindi hicho Lumuli Alipipi Kasyupa akashinda kwa urahisi sana!
Sikonge;
Uchaguzi wa mwaka 1980 ulikuwa rahisi sana kwa Kasyupa kwani wote wawili walikuwa wanatoka tarafa moja ya Ntebela,na ikawa rahisi zaidi kwa Kasyupa kushinda akimuhusisha Mwakipesile na kuwatekeleza wana Kyela wakati wa mafuriko hayo.
Sikonge;
Mwaka 1985 Kasyupa akamshinda pia kwa urahisi Mwenyekiti wa chama cha Ushirika Kyela-Kyerucu- Mzee Mwakalukwa ambae pia walikuwa wanatoka tarafa moja ya Ntebela.Ingawaje Mwakalukwa alikuwa na uwezo mkubwa kifedha lkn hakuweza kumshinda Kasyupa kwa sababu wana Kyela walisema"hatujaona kosa la Kasyupa"kama Mbunge wetu.Kimsingi kung'olewa Ubunge Kyela lzm uhusishwe na kutowasikiliza wapiga kura wako!
Sikonge;
Mambo yalianza kumgeukia Mbunge Kasyupa mwaka 1990 kwa sababu ya maombi ya awali ya wana Kyela kuhusu kujitenga na kanisa la Moravian ambapo walidai kila mali ya kanisa hilo inawafaidisha zaidi watu wa Rungwe.Wana Kyela ambao wengi wao ni wafuasi wa kanisa hilo waliandamana mara kadhaa kutaka Mbunge wao ashughulikie suala hilo.Kasyupa akawahaidi kuwapatia kanisa lao huru haraka iwezekanavyo na wana Kyela wakamchagua tena ingawa kwa kura chache toka kwa hasimu wake mkubwa kisiasa Mzee Mwakalukwa;lkn wachambuzi wa siasa za Kyela tulijua kabisa kuwa kama hatafanikiwa kulileta jimbo jipya la Moraviani wilayani Kyela ni heri tu asigombee ubunge mwaka 1995.
Sikonge;
Hadi bunge linavunjwa mwaka 1995,Kyela walikuwa hawajapata jimbo lao la kanisa toka Rungwe,na kibaya zaidi mwaka 1994 mwanaharakati mkuu wa kudai jimbo hilo toka Kyela Mzee Mwakapegere akatiwa kizuizini mwaka,kwa sababu mahabusu kuu ya kuwatunza ipo Rungwe basi mwanaharakati huyu akapelekwa mahabusu yenye ulinzi mkali ya Tukuyu siku si nyingi akiwa mahabusu Tukuyu mwili wake ukaokotwa akiwa amekufa kwenye moja ya vyumba ya mahabusu hiyo,wana Kyela hadi leo wana amini Mwakapegere alinyongwa akiwa kizuizini.Kwenye mazishi ya mwanaharakati huyu yaliyoitingisha Kyela wananchi walikubaliana kuwa kwa vile jimbo halijaja Kyela na mtetezi wao kafa kitatanishi basi Kasyupa asichaguliwe kwa sababu hajawasikiliza na pia wakamlaumu Kasyupa kwa kujiingiza kwenye G55 ili hali bado hajamaliza tatizo lao la jimbo;naam Livingstone Mwakipesile akashinda kwa urahisi sana lkn kwa ombi la kuwaletea wana Kyela jimbo lao toka Rungwe akichaguliwa na yeye akakubali!
Sikonge;
Mfumo wa vyama vingi uliingia kwa kasi wilayani Kyela,na chama cha UNCCR na baadae TLP kilikuwa na nguvu sana wilayani humo,kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 hayati Japhet Mwakasumi alishindwa kwa mbali sana na mgombea wa CCM Mwakipesile lkn kwa ahadi ya kurekebisha suala la kuwaletea jimbo lao.Hadi miaka 5 ya ubunge wake inakwisha wana Kyela wakawa hawaoni dalili yeyete ya kupata jimbo lao na kibaya zaidi wafanyabiashara wa zao la kakao na mpunga wakawa wanadhukumiwa kwa kununuliwa bidhaa zao kwa bei ya chini;hii ilikuwa ni ishara kubwa kuwa siku za Mwakipesile kuwa mbunge zinahesabika!
Sikonge;
Mwaka 2000 kwenye kura za maoni Mwakipesile alishinda lkn akakabiliwa na upinzani mkali toka kwa Japehet Mwakasumi wa TLP;sera ya Mwakasumi ilikuwa ni kuwaomba wana Kyela wamuulize Mwakipesile kwa nini hatimizi ahadi zake,lkn Mwakipesile na timu yake wakajitetea kuwa miaka 5 haikutosha kutimiza ahadi zake na akashinda kwa tofauti ya kura si zaidi ya 500 ktk uchaguzi mkali na mgumu kupata kutokea ktk historia ya chaguzi za Kyela!Ingawaje Mwakasumi alianzisha hadi shule ya Sekondari kijijini Kalumbulu lkn akabwagwa,kwani Kyela hawakupigii kura kwa sababu ya kitu fulani bali wao wanataka mtu wa kuwasikiliza madai yao!
Sikonge;
Baada ya bunge kuvunjwa mwaka 2000 na si tatizo la jimbo la kanisa wala kuimarika kwa soko la kakao na mpunga kupatiwa ufumbuzi ikawa sasa zamu ya Mwakipeile kuondoka,na kibaya zaidi alipoulizwa kwa nini hujatimiza ahadi zako akawa anajibu "serikali haina dini",ndipo Dr Mwakyembe kiurahisi zaidi akashinda kwenye kura za maoni!
Sikonge;
Dr Mwakyembe ni mwanasiasa makini sana,kwanza hakuwahaidi wana Kyela kupata jimbo lao toka Rungwe maana sheria inakataza kufanya hivyo lkn akawahaidi wanaweza kujitenga na kuanzisha jimbo lao from the scratch,na Kyela wakalielewa jambo hilo.Dr Mwakyembe akaja na siasa na balancing yaani akisaidia tarafa hii kitu hiki basi anakuja na msaada kwenye tarafa ingine kwa suala lingine.Kujengwa daraja korofi la Lusungo kwenye tarafa ya Ntebela kumemfanya aonekane kama ni Mbunge anayesikiliza kilio cha wapiga kura wake.Kujengwa kwa barabara ya kasumulu-Itunge,na Ikolo-kasumulu kumemfanye aonekane shujaa kwa wapiga kura wake.Kikubwa zaidi kuongoza timu ya uchunguzi ndani ya Bunge kulikomfanya hadi Waziri Mkuu Lowasa aachie ngazi kunamfanya Mwakyembe aonekane kama mungu-mtu wilayani Kyela;wakati Kasyupa alilaumiwa kujiingiza G55 kama haina maslahi kwa Kyela,wangonde wanampongeza Mwakyembe hadi leo kwa kuiokoa Tanzania toka kwa mafisadi!
Sikonge;
Kimsingi,Dr Mwakyembe kasema mwaka 2015 hatagombea,ingawaje hadi sasa akicheza karata zake vyema za kuwasikiliza wapiga kura wake anaweza shinda kiurahisi zaidi akiamua kugombea mwaka huo!Ni muda muafaka sasa kwa Mwakalinga kuanza kujijenga Kyela hasa kwa kuwasikiliza wapiga kura wanataka nini.Nina wasiwasi kuwa Diwani mpya aliyeshinda kura za maoni wa Kyela mjini,kijana aliyetoka masomoni USA hivi karibuni anaweza kuja mrithi Dr Mwakyembe mwaka 2015 maana ni kijana msikivu kwa wapiga kura wake.Lkn tatizo linakuwa baya kwa Mwakalinga zadi kwani wana-Kyela walimuambia asigombee mwaka huu bali asubiri mwaka 2015 wakati Mwakyembe aking'oka kwa heshima yake mwenyewe lkn hakuwasikiliza;tunarudi pale pale kuwa Mwakalinga sio mtu wa kusikia!
HITIMISHO;
Siasa za Kyela sio siasa za visasi bali ni siasa za kusikilizwa kwa wapiga kura!Kama huwasikilizi wapiga kura wako wanataka nini huwezi shinda uchaguzi wowote wilayani Kyela toka Ubunge hadi udiwani