Mkuu!!katika uchaguzi wa 2005, wananchi 63, 939 walipiga kura katika Jimbo la Kyela, hivyo kuwepo na wanachama wa CCM 17,000 it's not a big deal ukizingatia kuwa maeneo ya vijijini asilimia kubwa ya wananchi ni wanachama wa CCM.
Na hii sio Kyela tu, majimbo mengi ya Vijijini yana wapiga kura zaidi ya hao wa Kyela, ila Kyela imetokea tu kuwa Mgombea aliyepigiwa kura kwa wingi ni mmoja tu.
Check majimbo haya...
Katika jimbo la Arumeru Magharibi, Goodluck Joseph ole Medeye aliibuka mshindi dhidi ya wagombea wenzake wanane katika kinyang'anyiro hicho, kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchaguzi huo, Lightness Mweteni. Ole Medeye alipata kura 7,481, Loy Thomas Ole Sabaya (6,715) na aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Elisa David Mollel alimbulia kura 2,603.
JUMLA: Atleast 16, 799
Jimbo la Arumeru Mashariki mtetezi wa nafasi hiyo, Jeremiah Sumari ndiye anayeongoza kwa kura 11,377, akifuatiwa na Wiliam Sarakikya (1,371), Elirehema Kaaya (1,349) na Anthony Amos (1,026).
JUMLA: 15,123
Manyara Mbunge anayemaliza muda wake jimboni Mbulu Philip Marmo ameibuka mshindi baada ya kupata kura 20,927 na akimbwaga katibu tawala wa Wilaya ya Simanjiro, Michael Lowry (15,446).
JUMLA: 36,373
Jimbo la Hanang Dk Mary Nagu ameshinda kwa kishindo kwa kupata kura 19,700 dhidi ya Rose Kamili mke wa Dk Wilbroad Slaa aliyepata kura 5,430.
JUMLA: 25,130
Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka amepata ridhaa ya wanachama kugombea tena ubunge wa Simanjiro baada ya kuzoa kura 18,070 wakati James Ole Millya aliambulia kura 4,907, kwa mujibu wa katibu wa CCM mkoani Manyara, Avelin Mushi.
JUMLA: Atleast 22,977
Tanga Jimbo la Handeni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (Taifa), Dk Abdallah Kigoda ameibuka kidedea baada ya kupata jumla ya kura 11,227, wakati Mohamed Mhita akishika nafasi ya pili kwa kuambulia kura 4,318, kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchaguzi huo, David Mkude.
JUMLA: Atleast 15,545
Jimbo la Mkinga Dunstan Kitandula aliibuka mshindi kwa kupata kura 10,867 na kumbwaga Naibu Wazir wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza (9,114).
JUMLA: Atleast 19,981
Source:
Vigogo wengi CCM watoswa ubunge