Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Ikuluye Kichuguu, nimekupata.Kuhusu wimbo huo, nitatafuta hiyo thread niusikilize kwa makini. Tatzio kubwa kwetu tuliokaa sana nje ya nchi ni kule kushindwa kupambanua kinyamwezi na kisumbwa, kwa hiyo ukisikilza katika upande wa kinyamwezi tu bila kuchanganya kisumbwa kidogo unaweza kupotea. Ukiishi sana Tabora unakuwa huoni tofauti yoyote baina ya lugha hizo lakini kama umeshakaa nje sana, unaweza kupotea.
Huu wimbo ulinipa shida sana. Nilisikiliza pamoja na nyingine mwanzo sikuelewa na niliposikiliza mara ya tatu nikaanza kuelewa baadhi ya maneno. Jana nimempigia simu kaka yangu huko Ushirombo na nikaona basi walau nimuulize tu. Nikampigia kipande na akacheka sana. Akaniambia siwezi kuelewa maneno yote. Inawezekana kuwa hawa waimbaji wanachanganya na Kisumbwa ila ukweli ni kuwa hawa jamaa ni WASWEZI. Sikumbuki kwa sasa tofauti ya Maswezi na Mabisa ila kama sikosei Mabisa wanacheza wakiwa wamekaa na ku-move kwa kutumia makalio na utotoni nilikuwa naiita Sikinde (ngoma ya Ukae). Waswezi wao wanacheza kawaida wakiwa wamesimama.
Nakumbuka pia walikuwepo wengine wakiwa na Majini (hawa mara nyingi ni watu wanaotibu) na pia walikuwepo wengine wanaoamini Pepo liitwalo MIGABO (Migavo). Hawa sikumbuki vizuri walikuwa wakicheza vipi ila kwa Tabora walikuwa wengi sana.
Wakati mwingine walikuwa wakibadili badili utafikiri KKKT . Usiku mmoja watapiga ngoma wanaweza kupiga ngoma zote yaani wakapiga za Waswezi, Mabisa na Migabo.
Mtu maarufu sana Tabora kwa hizo ngoma za Maswezi ingawa zaidi alikuwa akijiita wa Migabo, alikuwa ni Mwana Lwelwe (Rwerwe). alikuwa na nyimbo/wimbo wake umerekodiwa RTD akiimba "aluyu Lwelwe wa Migavo, ........." Huyu nilikuja kupata habari kuwa alikuwa akiishi Itetemya/Kipalapala Tabora. Na mwaka juzi nikaja kuambiwa kuwa alikuwa akitoka familia ya Chief Fundikira. Imenipa sana hamu ya kwenda kuhiji kwenye makuburi ya mababu zetu pale Itetemya na kuangalia/kuambiwa Historia yetu.
Samahani Wanyakyusa kwa kuiteka hii habari. Ila naona ndiyo imeshaisha. Kichuguu, nakuwekea tena wimbo huu hapa. Nyingine ntakuwekeeeni Link ili mzivute kama mtataka. Wanyakyusa na nyie ntawawekea, msiwe na wasiwasi.
YouTube - ‪Nyamwezi-Uwi, mamsanga makumbulage wagela mnyabo‬‎