Kyela: Wananchi wachachamaa , wataka Meya na Mkurugenzi wakamatwe , yumo pia diwani mmoja , Mwakyembe naye atakiwa kuhojiwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wakuu natanguliza salamu , baada ya salamu hii naingia moja kwa moja kwenye hoja ,

Soko Kuu la Wilaya ya Kyela kwa miaka yote ya Uhai wake lilikuwa mali ya Halmashauri , lilikuwa ni mali ya umma , Halmashauri ilitoa ramani ya muongozo kwa wananchi waliokuwa na uwezo wa kujenga vibanda vya biashara na kujenga meza ndani ya soko hilo , huku gharama zikiainishwa na baadaye kuingia mikataba ya upangaji na Halmashauri , kwa kukata gharama zao taratibu kwenye kodi , TAARIFA ZA SASA NI KWAMBA HALMASHAURI IMEAMUA KUGAWA SOKO HILO KWA CCM bila kufuata utaratibu wowote ule , Hakuna kikao chochote cha Madiwani kilichowahi kuidhinisha jambo hili , watendaji wa Halmashauri waliojaribu kulivalia njuga jambo hili wametishwa kufukuzwa kazi na kutekwa .

Viongozi Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM , Hunter Mwakifuna na Mkurugenzi wa Wilaya bila kufuata sheria yoyote wala utaratibu wowote ule wa kisheria wameamua kuligawa soko la Kyela kwa ccm , ambalo ndio Chanzo Kikuu cha mapato ya halmashauri , ndani yake kuna maduka zaidi ya 200 huku meza za soko la samaki wabichi na wakavu na meza za kuuzia nafaka zikiwa lukuki , Hili wananchi wa Kyela hatutakubali na tuko tayari kujaza makaburi mapya ya Kapamisya kwa siku moja.

Ili kufupisha habari tunaiamrisha Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kurejesha mara moja umiliki wa Uwanja wa Mwakangale kwa umma , kuirejesha timu ya mpira wa miguu ya Boma na nyaraka zake zote mikononi mwa wananchi haraka sana , hatuna ugomvi na " mwekezaji " Kipija ambaye ni diwani wa ccm , akitaka kuwekeza afuate taratibu , lakini hatutakubali achukue tu timu ya wananchi kama vile kaokota embe mfipo , ni lazima taratibu za nchi zifuatwe .

Suleiman Jaffo Waziri wa Tamisemi hakikisha ccm inarejesha vyanzo vikuu vya mapato vya Halmashauri ya Kyela bila masharti yoyote na ahakikishe Mbunge wa Kyela anahojiwa na TAKUKURU kuhusiana na jambo hili , maana haiwezekani dhuluma hii kufanyika bila Mh Mbunge kufahamu .

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO .

........ Itaendelea ..........

Mungu ibariki Kyela
 
Ccm si ndyo zao kupora maeneo au ndyo unajua Leo?....Niliwahi kufika geita kuna uwanja was shule mgodi walitaka kujenga uwanja wa michezo. Ccm wakaingilia kati wakidai uwanja ni wao mgodi ukaghairi kuujenga.....sasa just imagine hadi viwanja vya shule wanadhulumu ije kuwa soko LA halmashauri
 
Aiseee !!!
 
safi sana shemeji zangu Wanyaki.... nawaaminia kwa misimamo!
 
Juzi nilifika pale Bomang'ombe wilaya ya Hai nikakuta majengo yote lilokuwepo soko la zamani yameandikwa CCM kwa rangi ya kijani sijui nako imekuwaje.
 
Juzi nilifika pale Bomang'ombe wilaya ya Hai nikakuta majengo yote lilokuwepo soko la zamani yameandikwa CCM kwa rangi ya kijani sijui nako imekuwaje.
Kila lenye mwanzo halikosi mwisho
 
Sawa ,amewatuma mtengeneze mgogoro harafu aje ajifanye ametatua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…