Kyela: Wananchi wachachamaa , wataka Meya na Mkurugenzi wakamatwe , yumo pia diwani mmoja , Mwakyembe naye atakiwa kuhojiwa

Kyela: Wananchi wachachamaa , wataka Meya na Mkurugenzi wakamatwe , yumo pia diwani mmoja , Mwakyembe naye atakiwa kuhojiwa

Wakuu natanguliza salamu , baada ya salamu hii naingia moja kwa moja kwenye hoja ,

Soko Kuu la Wilaya ya Kyela kwa miaka yote ya Uhai wake lilikuwa mali ya Halmashauri , lilikuwa ni mali ya umma , Halmashauri ilitoa ramani ya muongozo kwa wananchi waliokuwa na uwezo wa kujenga vibanda vya biashara na kujenga meza ndani ya soko hilo , huku gharama zikiainishwa na baadaye kuingia mikataba ya upangaji na Halmashauri , kwa kukata gharama zao taratibu kwenye kodi , TAARIFA ZA SASA NI KWAMBA HALMASHAURI IMEAMUA KUGAWA SOKO HILO KWA CCM bila kufuata utaratibu wowote ule , Hakuna kikao chochote cha Madiwani kilichowahi kuidhinisha jambo hili , watendaji wa Halmashauri waliojaribu kulivalia njuga jambo hili wametishwa kufukuzwa kazi na kutekwa .

Viongozi Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM , Hunter Mwakifuna na Mkurugenzi wa Wilaya bila kufuata sheria yoyote wala utaratibu wowote ule wa kisheria wameamua kuligawa soko la Kyela kwa ccm , ambalo ndio Chanzo Kikuu cha mapato ya halmashauri , ndani yake kuna maduka zaidi ya 200 huku meza za soko la samaki wabichi na wakavu na meza za kuuzia nafaka zikiwa lukuki , Hili wananchi wa Kyela hatutakubali na tuko tayari kujaza makaburi mapya ya Kapamisya kwa siku moja.

Ili kufupisha habari tunaiamrisha Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kurejesha mara moja umiliki wa Uwanja wa Mwakangale kwa umma , kuirejesha timu ya mpira wa miguu ya Boma na nyaraka zake zote mikononi mwa wananchi haraka sana , hatuna ugomvi na " mwekezaji " Kipija ambaye ni diwani wa ccm , akitaka kuwekeza afuate taratibu , lakini hatutakubali achukue tu timu ya wananchi kama vile kaokota embe mfipo , ni lazima taratibu za nchi zifuatwe .

Suleiman Jaffo Waziri wa Tamisemi hakikisha ccm inarejesha vyanzo vikuu vya mapato vya Halmashauri ya Kyela bila masharti yoyote na ahakikishe Mbunge wa Kyela anahojiwa na TAKUKURU kuhusiana na jambo hili , maana haiwezekani dhuluma hii kufanyika bila Mh Mbunge kufahamu .

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO .

........ Itaendelea ..........

Mungu ibariki Kyela
Imbombo inghafu!
 
Safi sana chama langu CCM na serikali ya awamu ya 5. Kufuata sheria kuna chelewesha maendeleo!
 
Safi sana chama langu CCM na serikali ya awamu ya 5. Kufuata sheria kuna chelewesha maendeleo!
Unaweza kuainisha maendeleo yaliyopatikana kwa kuvunja sheria ?
 
Jaffo asipoingilia kati hili suala Kyela itaripuka vibaya sana !
 
Aiseee !!!
Hilo eneo ni Mali ya CCM halmashauri waliliomba kwa masharti watu wajenge halafu baadaye lirudishwe kwa CCM muda wa mkataba ukiisha.Mkataba umeisha .Ukipanga muda ukiisha utadai jengo la kwako?
 
Hilo eneo ni Mali ya CCM halmashauri waliliomba kwa masharti watu wajenge halafu baadaye lirudishwe kwa CCM muda wa mkataba ukiisha.Mkataba umeisha .Ukipanga muda ukiisha utadai jengo la kwako?
Wewe mtu wa Geita mambo ya Kyela unayajulia wapi , halafu kama hilo unalosema lina ukweli wowote kwanini hizo nyaraka zisiwekwe hadharani ?
 
Wewe mtu wa Geita mambo ya Kyela unayajulia wapi , halafu kama hilo unalosema lina ukweli wowote kwanini hizo nyaraka zisiwekwe hadharani ?
Mkataba ni Kati ya mwenye nyumba na mpangaji.Kitakachowakuta hao watu wenu Mungu ndie anajua.Wanashabikia jambo wasilolijua vizuri
 
Back
Top Bottom