Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,375
- 4,784
Nimeipenda sana picha ya bondia Hassan Mwakinyo, ikimuonesha Simba wa vita vya haki nchini, Tundu Antiphas Lissu, na Simba mwingine wa vita vyake, Samia Suluhu Hassan.
Kwa maono ya kinabii, naweza kusema kwamba, kitendo cha bondia Mwakinyo, kina kauli ya Mwenyezi Mungu - ambaye kwa mujibu wa vitabu vitakatifu, amekuwa akionesha ishara kwa wanadamu kupitia roho mtakatifu. Kwa hiyo, wanaomponda Mwakinyo - kwamba ni mchochezi; hawayajui matendo ya Mungu. Mwakinyo ametumika tu kama daraja.
Kwa sababu pia yeye aliibuka mshindi, ile picha inakuwa na maana zaidi, kwamba: ili nchi itoke kwenye mtanziko, ni lazima hawa Simba wawili wa vita vyao, wafanye dialogue. Na ni hiyo dialogue, itakayokuwa mwanzo wa kuondoa hali ya mtanziko uliopo nchini kwa sasa.
Ukweli mchungu ni kwamba: CCM wasijidanganye kwamba mtanziko utaondoka tu wenyewe bila dialogue na mwanasiasa mwenye nguvu zaidi Tanzania kwa sasa (ndo uhalisia uliopo, ambao hauwezi kubadilika, hata ukifuta hizo picha za Mwakinyo zinazomuonesha TAL - huwezi kuupinga ukweli kwa kuukataa, kwamba haupo)
Ukweli mwingine mchungu na unaouma ni kwamba: hakuna pia namna yoyote, mtanziko utaondoka bila kumuhusisha Rais Samia. Bila kujali amekuwaje Rais, lakini hakuna namna yoyote utafanya chochote cha kuleta amani bila yeye kuhusika kwa namna kubwa. Kama yeye asipochukua hatua kubwa, yenye kuleta amani; hakuna kitachotokea.
Hivyo, picha ya bondia Mwakinyo, ni unadhiri mwingine wenye neno la Mungu, unaobeba uhalisia mchungu kwa mirengo yote miwili ya kisiasa nchini; na ni picha inayogusia, njia ya kweli ya kuvunja mtanziko uliopo.
Kazi ya Mja, Maneno Kunena!
MC nimenena!