La Liga: FC Barcelona watwaa ubingwa bila kufungwa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Klabu ya FC Barcelona ya Hispania imetwaa rasmi ubingwa wa Ligi Kuu ya soka ya nchini humo bila kufungwa. Hii imefuatia ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu inayoteremka daraja ya Deportivo la Coruna ulioisha hivi punde. Kwa ushindi huo, wakicheza michezo 34, Barca wamefikisha alama 86 ambazo kimahesabu haziwezi kufikiwa na washindani wao wa karibu Atletico Madrid na Real Madrid.

Atletico Madrid iliyocheza michezo 35 ikiwa nafasi ya pili ina alama 75 huku Real Madrid iliyopo nafasi ya tatu ikiwa na alama 71 na kubakiza michezo minne. Katika mchezo uliowapa ubingwa Barcelona, Lionel Messi aka Andunje alifunga mabao matatu. Wakati wa mchezo baina ya Barcelona na Real Madrid tarehe 6 mwezi ujao, Real watalazimika kuwashangilia mabingwa Barca kabla na baada ya mchezo.
 
HAHAHAAAAA WAMBIE BARCA WASUBIRII KULIPOKEA KOMBE LA [HASHTAG]#UEFA[/HASHTAG]

[HASHTAG]#WAGARANYOOOOOOOONYOOOOOMADRID[/HASHTAG]
 

Asante bro
 
Hat trick ya jana unaweza kwenda nayo kazini leo j3 badala ya mafile

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ yule ndiye the lion Messi, haters wanatamani avunjwe miguu hata world cup akoseπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›
 
Hata Simba wanakaribia hiyo achievement
 
uzi wa kichochezi[emoji23][emoji23]... mashabiki wa Barca mnawashwa washwa... au tuwaitie As Roma[emoji23][emoji23][emoji23] kikombe kimoja uzi mkubwa
Upe basi ubongo wako akili na kumbukumbu sio kikombe kimoja ni vikombe viwili!
Madrid bhana ka yanga wanafurahia kuwepo uefa ka wamechukua tyr sawa na yanga wanafurahia kuendelea makundi wamesahau kua mwakani hawaendi kucheza CAF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…