Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Klabu ya FC Barcelona ya Hispania imetwaa rasmi ubingwa wa Ligi Kuu ya soka ya nchini humo bila kufungwa. Hii imefuatia ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu inayoteremka daraja ya Deportivo la Coruna ulioisha hivi punde. Kwa ushindi huo, wakicheza michezo 34, Barca wamefikisha alama 86 ambazo kimahesabu haziwezi kufikiwa na washindani wao wa karibu Atletico Madrid na Real Madrid.
Atletico Madrid iliyocheza michezo 35 ikiwa nafasi ya pili ina alama 75 huku Real Madrid iliyopo nafasi ya tatu ikiwa na alama 71 na kubakiza michezo minne. Katika mchezo uliowapa ubingwa Barcelona, Lionel Messi aka Andunje alifunga mabao matatu. Wakati wa mchezo baina ya Barcelona na Real Madrid tarehe 6 mwezi ujao, Real watalazimika kuwashangilia mabingwa Barca kabla na baada ya mchezo.