Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 257
- Thread starter
-
- #121
Jamani mimi mwanamke siyo mrembo kwa kweli. Mzuka na weaving, wigi siko. Kisa hiki ni cha kweli natoa hapa si kwamba nadharau wale wavaaji ila muwe makini .
Juzi nikiwa kwenye dala dala natoka kariakoo, akaingia dada mmoja mtanashati kavaa mlegezo ili kale ka CUPI kenye kamba kaonekane. Ile anaibuka kwenye dala dala mlangoni kulikuwa na chuma kikamata wigi likachomoka kichwani likabaki kwenye chuma. Huko ndani ya kichwa chake ilikuwa hatari, manywele mabaya, yamevurugika nahisi alitoka kufumua rasta akaweka ili kuficha uchafu wake AKAUMBUKA. Dada wenzangu shaurini hapo. Kwa wanaume naomba wapigeni marufuku wake zenu kuvaa mawigi, tena wekeni msistizo.
Wanawake wengine wakivaa hawapendezi lakini wamo tu. Siku hizi kuna consultants wa urembo nenda katoe hela yako wakushauri nini ufanye na mwili wako, uso au hata kwenye hizo nywele unazotaka wakwambie kama utapendeza au la.
Samahani wanawake wenzangu, ni mtizamo tu ila mawigi siyo INSHU.
Tungekuwa karibu, ungeagiza soda bill kwangu. Bahati mbaya nyingine tena kwenye simu ya kiganjani hakuna sehemu ya kukong'oli 'thanks'. Nimebaki nahangaika tu.