Nakumbuka siku moja nipo lodge nimenunua lager yangu moja nakunywa mdogo mdogo, ghafla nasikia sauti nakufa nakufa, kumbe mwanaume mmoja (Mme) alikuwa anamkimbiza mke ambaye alikuwa ameonekana kutoka kwenye ile lodge. Hivyo baada ya kukimbizwa yule mwanamke akawa amerudi pale lodge, sasa wakanikuta nakunywa kinywaji. Kwa mshituko na Mimi nikaanza kukimbia maana yule jamaa alikuwa ameshika chupa ya bia ambayo aliipasua. Jamaa baada kuona nimekimbia akadhani ndiye mtu niliyekuwa na mke wake, akasema leo lazima tuuae. Nilijukuta nimeruka juu ya ukuta wa Lodge nikiwa na vest na boxa