La Rocka bar ya Kawe, Dar ongezeni ulinzi watakufa wengi hapo

Hofu mbaya, lazima ukimbie!
 
Kamwe usiwe sehemu ya ugomvi wowote maeneo ya bar, pub, club, lounge au grocery.
Surely . Umeongea point muhimu sana. Kuna jamaa alienda kuamua ugomvi wa jamaa yake. Ile oya oya ya kununua ugomvi usiomhusu , alikutana na kisu cha shingo ile paap, aliyumba mara tatu tu ikawa imeisha hiyo. Ogopa damu ilitoka chwaaa kwa presha kama vile ng'ombe anayekamuliwa maziwa . Ni hatr sana
 
Dah!...ungeuawa man.... hatari sana
 
Kiujumla tuwe tu makini tunapokunywa. Hao security men ni ngazi ya pili ya ulinzi ngazi ya kwanza ni wewe mwenyewe, pia licha ya ugomvi pia kuna masuala mengine kama unywaji uliopitiliza unaweza kukusababishia matatizo

Binafsi nishazika mshkaji wangu sababu ya pombe, alipiga vitu vikali tumboni hakuna kitu kufika asubuhi tunamuamsha mtu wapi kukimbiza hospitali dokta kachukua vipimo akatuambia tayari huyu nendeni mkafukie tu.
 
badala ya kusikitika nimecheka sana
 
Yule dem aliyenikimbia akafunga mlango akaaniacha nje na msala wa masela wa kitaani kwake....kama upo humu ulaaniwe.....uliniambia nikusindikize getoni kwako kumbe umekula bia za wahuni unataka kutoroka kupitia mim fala sana..

Nashukuru Mungu alituma malaika wa kheri tukamaliza kidemocracy maana madogo walikua wana visu na chumba za fanta zilivyo ngumu daah.......pia abalikiwe yule msela aliyesema uenda dem ndo malaya tusije tukumuua mwamba kwa umalayaa wa dem....

Pia alaaniwe yule dogo aliyekua anamuuliza mkuu wa kutengo atoe go ahead ya kushambulia,dogo nilikukata jicho baya sana.........
 
Ndio maana nimeamua kuacha kunywa POMBE maana najijua akili zangu nikishalewa huwa sipendi upumbavu.. dk 2 mbele mtu anakula kofi.

Sasa nikaja kuambiwa na washkaj kwamba nikishakunyw huw sio Mimi tena nakuw very aggressive hasa mtu akijichanganya..

Na mbaya zaidi huw nafata dem wa mtu yupo na bwana ake na nasaundisha hapo hapo..

Hii ni mbaya.. bahat nzr nakuw conscious ila kujiamini ndio 10000+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…