Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
MWALIMU wa timu ya soka ya taifa ya Brazil Carlos Dunga ambaye anaaminika kuwa ndiye mwalimu kiburi,
mwenye kujiona yeye ndo yeye, asiyesikia la kushauriwa,
mwenye vinyongo na waliomzidi mafanikio,
ambaye hakupata kuchezea timu kubwa barani ulaya,
ambaye hakupata kuchukua kombe lolote kwa ngazi ya klabu barani ulaya,
ambaye hakupata kukubalika na kuwa gumzo barani ulaya,
asiyekuwa na washabiki kama waumini wake huko brazil,
ambaye amepata kukosolewa zaidi ktk soka la Brazil,
asiyejuwa kuvaa,
asiyekuwa hata na kumbukumbu japo ya mnara wake huko kijijini kwao chaka ili kuonyesha kuwa anakubalika huko, ambaye anafananishwa na ndege mbilikimo waishio kando ya Bahari,
ametangaza kikosi chake kitakachokwenda South kutalii.
Ktk kikosi hicho kijana huyu ambaye anaonekana kama mzee ameutusi mchezo wa Soka na kuudhalilisha baada ya kumuacha kiungo mshambuliaji asiyefananishwa na mwingine,
ambaye inaaminika alishushwa kwa ajili ya kuja kuonyesha jinsi soka mbinguni linavyochezwa,
Ambaye pia inaaminika kuwa kama mpira ungekuwa unaongea basi ungefumbua mdomo na kusema kuwa ''kila baada ya dakika moja basi nipelekeni kwa The Saint Ronaldo de Assis Morreira'' ili mbinguni na duniani wote wafurahi.
Dunga ameonekana kupuuzia shinizo toka jumuiya mbalimbali za kimataifa zikimtaka amjumuishe RONALDINHO GAUCHO ktk kikosi chake, laikini Dunga ameonekana kuwa na roho ya korosho kwa kuwa Gaucho amemzidi mafanikio na anakubalika na kupendwa ulimwenguni kote.
Wabrazil kadhaa wameonekana kando ya fukwe za Bahari wakilia kwa uchungu na wengine wameonekana wakiwa na mabango yenye maneno makali na ya Laana yanayomuelekea Mwalimu huyu.
Mpk napost thread hii nilikuwa sijapata habari yoyote iliyotolewa na Dinho, ingawa kuna tetesi kuwa Dinho alishaufahamu mpango huo hivyo anaendelea kula biriani kwa raha zake, ukizingatia hakuna kitu ambacho Dunga Kamzidi....labda ufupi na chuki.
Baadhi ya wabongo niliofanya nao mahojiano wameonyeshwa kumdharau dunga na kusema wazi kuwa ''there is NO world Cup on south african pitch without Dinho''
Na wengine wametanabaisha kuwa Word Cup bila Gaucho ni sawa na ''kashata bila sukari''.
Na kumalizia kuwa laana toka Mbinguni linamsubiri.