Laana ya Adam na Hawa

Laana ya Adam na Hawa

Kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa MFANO WAKE. viumbe wengine waliumbwa pasipo mfano wake. Maana ya mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa mungu si kufanaa sura, bali utashi na kuishi milele. Baada ya kula lile tunda Mungu alifuta kalama ya kufanana naye kwa wanadamu. Ndio sababu wanadamu wanakufa kama viumbe wengine ambao hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu

Hii point nadhani ndio jibu la ule uzi, kwamba kifo kilikuwepo kwa viumbe wengine wote isipokuwa binadamu. Baada ya binadamu kutenda kosa (ofcoz na kushindwa kuomba radhi) naye akaingia kwenye adhabu mbali mbali eg kula kwa jasho, kuzaa kwa taabu na hatimaye kufa.
 
Kwani ulaji wa nyama hata kwa binadamu ulikuwa tangu mwanzo?

Binadamu alipokosea alileta mabadiliko makubwa sana kwa viumbe vyote....!!

Mkuu binadamu ni Omniveras Animal anaekula vyote ie nyama, matunda, majani etc. Hivyo anaweza ku-survive kwa kula chakula chochote kati ya hivyo, hii na sawa na kusema binadamu anaweza kuishi bila ya kula nyama.

Swali langu ni kwamba, ikiwa vifo vilianza baada ya laana ya Adam na Hawa kula tunda, wale wanyama/viumbe wanaokula tu nyama (Carnivores) walikuwa wanakula nini kabla ya hiyo laana???
 
Ikiwa ni hivyo. Na ikiwa wanyama walianza kufa kabla ya kufa wanadamu or kabla ya laana ya wanadamu, Hiyo laana inawahusu nini wanyama? or Nini kilibadilika kwa wanyama hao baada ya kulaaniwa kwa wanadamu?
Ukweli ni kwamba Mungu aliwahukumu wale tu waliotenda kosa. Nyoka atatembelea tumbo na kupondwa kichwa na uzao wa mwanamke. Eva alihukumiwa kuzaa kwa uchungu, Adamu kula kwa jasho lake. Kulikuwa hamna hukumu nyingine iliotoka kwa Mungu baada ya kuwahukumu waliotenda kosa. Mungu akuwahukumu wasio na hatia.

Kabla ya kuumbwa kwa Eva, Adamu aliletewa kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani na kila mnyama wa mwituni ili awape majina na akawapa wote majina. Ina maana kulikuwa na wanyama wa kufugwa na mwituni hata kabla ya eva kuumbwa. Hivyo hamna kilichobadilika kwa wanyama wengine tofauti na nyoka baada ya kulaaniwa wanadamu.
 
Mkuu binadamu ni Omniveras Animal anaekula vyote ie nyama, matunda, majani etc. Hivyo anaweza ku-survive kwa kula chakula chochote kati ya hivyo, hii na sawa na kusema binadamu anaweza kuishi bila ya kula nyama.

Swali langu ni kwamba, ikiwa vifo vilianza baada ya laana ya Adam na Hawa kula tunda, wale wanyama/viumbe wanaokula tu nyama (Carnivores) walikuwa wanakula nini kabla ya hiyo laana???
Mkuu uwe unasoma basi kwa makini ninachokuwa nakuandikia ....

Nilichosema mimi ni KABLA ya binadamu kuubadili ulimwengu kwa tendo lake moja tu la kutokutii,huu ufahamu uyliouandika hapa ni wa baada ya hilo kosa,je kabla ya hapo unadhani Dunia ilikuwa hivi?

Hata ukiangalia namna binadamu alivyoumbwa utaona hakuumbwa ii ale nyama ila kitu kingine kabisa,lakini sasa anakula....!!
 
Ukweli ni kwamba Mungu aliwahukumu wale tu waliotenda kosa. Nyoka atatembelea tumbo na kupondwa kichwa na uzao wa mwanamke. Eva alihukumiwa kuzaa kwa uchungu, Adamu kula kwa jasho lake. Kulikuwa hamna hukumu nyingine iliotoka kwa Mungu baada ya kuwahukumu waliotenda kosa. Mungu akuwahukumu wasio na hatia.

Kabla ya kuumbwa kwa Eva, Adamu aliletewa kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani na kila mnyama wa mwituni ili awape majina na akawapa wote majina. Ina maana kulikuwa na wanyama wa kufugwa na mwituni hata kabla ya eva kuumbwa. Hivyo hamna kilichobadilika kwa wanyama wengine tofauti na nyoka baada ya kulaaniwa wanadamu.

Nakusoma vyema mkuu, embu ni-clarify kile ulichomanisha:

Kulaaniwa kwa Adam na hawa hakujaathiri ufaji wa wanyama wengine, wanyama walikuepo, walikua wanakufa na kuzaliwa hata kabla ya laana ya Adam na hawa.

Jee unamanisha hivyo?
 
Mkuu uwe unasoma basi kwa makini ninachokuwa nakuandikia ....
Nasoma vizuri mkuu, may be hujalielewa swali nililokuuliza!
Nilichosema mimi ni KABLA ya binadamu kuubadili ulimwengu kwa tendo lake moja tu la kutokutii,
Ulimwengu ulibadilika vipi? (Ukumbuke, mada kuu inaongelea laana ya Adam na Hawa na athari zake kwa wanyama)
huu ufahamu uyliouandika hapa ni wa baada ya hilo kosa,je kabla ya hapo unadhani Dunia ilikuwa hivi?
Unaposema "huu ufahamu uliyouandika hapa ni wa baada ya hilo kosa" unamanisha nini? Jee unamanisha kabla ya hapo hakukua na wanyama waliokula nyama? ukimanisha hata chui walikula majani? or unamanisha hakukuwa na wanyama wanaokula nyama tu? Au unamanisha wanyama walikua hawali chochote?

Mimi siamini hata hiyo mnayoiita laana ya Adam na Hawa. Na hii nahisi ni issue nyengine pana tu. wacha tuiskip.

Hata ukiangalia namna binadamu alivyoumbwa utaona hakuumbwa ii ale nyama ila kitu kingine kabisa,lakini sasa anakula....!!
Mmmh! Hapa ata sielewi, naweza kukuuliza aliumbwa ili ale nini, na nani na ushahidi wake ikawa tuengeza maswali nje na mada husika.
 
Nakusoma vyema mkuu, embu ni-clarify kile ulichomanisha:

Kulaaniwa kwa Adam na hawa hakujaathiri ufaji wa wanyama wengine, wanyama walikuepo, walikua wanakufa na kuzaliwa hata kabla ya laana ya Adam na hawa.

Jee unamanisha hivyo?

Ndio hivyo
 
Ndio hivyo

Okey.
Nakumbuka ulisema huo ni msimamo wa ki/ukiristo, mpaka hapo unamanisha mleta mada amekuja na hayo akidhani ni ukiristo, kwamba; kumbe laana ya Adam na Hawa haijaathiri lolote kwa wanyama.

But ukijaribu kusoma post za wadau humu, utaona kwamba wengi/wote ispokua wewe (Kwa wale wakiristo) wanakubali kwamba laana ya Adam na Hawa imeathiri ulimwengu kiujumla ikiwemo mfumo mzima wa maisha ya wanyama. Jee unaliongeleaje hilo?
Jee unaushahidi wowote especially wa kimaandiko (Biblia Takatifu) kuweza kusapoti huo msimamo wako? hiyo ni kwa vile inaonekana ni msimamo tofauti na wakiristo wengine.
 
Ukisoma kitabu cha Mwanzo 1:29-30 haisemi wanyama wote walikula majani..badala yake inasema mimea ilitolewa kwa ajili ya chakula..hamna sehemu kwenye biblia ambapo wanyama walianza kula nyama..Mwanzo 1:21 kuna viumbe wa majini kama nyangumi wakubwa walioumbwa siku ya tano hawajatajwa kwenye Mwanzo 1:29-30, Mungu hakuwaumba ili washinde njaa mpaka baada ya laana ya wanadamu...

Mwanzo 1:24 inayozungumzia kuumbwa kwa wanyama wa kufugwa na mwituni..ni wazi wanyama hao wa mwituni walikula wenzao , kusingekuwa na haja ya kutenganisha wanyama..

Inaonekana Adamu aliwapa majina wanyama baada ya kuwaona walivyokuwa wanaishi na tabia zao..mfano 'simba' kwa tafsiri ya kiebrania ni 'katika hali ya kikatili' ..sidhani alimuita simba simba baada ya kuona anararua mimea badala yake alivyokuwa anawala wanyama wenzake...yawezekana Adamu aliwaita kwa lugha nyingine, lakini hiyo lugha ilitafsiriwa kwa kiebrania..

Mwanzo 2:17, Mungu akamuonya Adamu kutokula tunda la kati, na kuwa akifanya hivyo atakufa hakika..inaonekana Adamu alijua maana ya kufa kwani hamna sehemu kwenye biblia Adamu akimuuliza Mungu maana ya 'kifo'..asingeweza kumuuliza Mungu alichokimaanisha kwa sababu alikwishaona wanyama wanavyokufa au kuuana...
 
adam na hawa walimilikishwa dunia na viumbe vyote..baada ya wao kula tunda(kufanya mapenzi)ndipo balaa la laana lilipokuja sababu alijua idadi ya watu itaongezeka kuliko rasilimali zilizopo lkn km wasingefanya wangebaki wao peke yao milele

Nani kakudanganya kwamba kula tunda walifanya mapenzi?
 
Ok nimekusoma Mkuu.
 
Mkuu....

Kwa context yako,Mungu ana sura kama yako?

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

1 Mwanzo 1 :26

👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆
Nadhani Yeye Mwenyewe Amesema Hapo Juu.......... kwahiyo Kwa Uelewa Wangu Ni YES

Sasa Sijui Kama Kuna Ukanushi wa Hilo Andiko.. Na Kama Kuna Sehemu Nimefanana Na Kiumb Kingine
 
Mkuu kifo sio adhabu ya Asam kukosea bali matokeo ya kula tunda,dhabu ni nyingine kabisa maana matokeo ya kula tunda yalikuwepo hata kabla hajakosea ....

Sawa Mkuu.. ila Kuna Sehemu Pia Imeandikw Kuwa Kulikuwa na Mti wa Uzima.. Amabapo kama Adamu angeusogelea Angeishi Milele.. Kwahiyo Miti Ilikuwa Miwili Wa Kifo na Uzima.. Ndo maana Kukawekwa Ulinzi...
 
adam na hawa walimilikishwa dunia na viumbe vyote..baada ya wao kula tunda(kufanya mapenzi)ndipo balaa la laana lilipokuja sababu alijua idadi ya watu itaongezeka kuliko rasilimali zilizopo lkn km wasingefanya wangebaki wao peke yao milele

Weee ndo mpotoshaji namba moja dhambi waliyo ifanya ni wali mwasi Mungu..na co kufanya mapenzi....Mungu aliwakataza wasile lile tunda kwasababu wakila watakuwa kama Mungu yani watajua jema na baya pia hawata kufa wata ishi milele....ndo mana wakafukuzwa katka bustani ya edeni'.....ndo wakapewa ile laana kwamba adamu utakula kwa jasho hawa utazaa kwa uchungu akamwambia utakuwa chini ya adamu....akamwambia kizazi chako kitakuwa adui wa nyoka....utamponda kichwani ...naye nyoka ata kuuma kisigino...Mungu akamwambia nyoka kwa tumbo utakwenda na utakula mavumbi ya nchi....pia hakuishia apo Mungu akasema hakika ww mwanadamu u mavumbi na mavumbini utaludi(kifo)....
 
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

1 Mwanzo 1 :26

Mbona Umeenda Tofauti na Andiko

Mungu akasema natumfanye mtu kwa mfano wetu basi mungi si mmoja bali wako wengi

Bila shaka wanawake wameubwa na mungu mwana

Wanaume na mungu baba

Kisha mungu roho akatupatia roho kwa kila mmoja

Ndo maana wanawake hawajakamilika vizurii kutokana waliubwa na mungu mwana

Asanteni
 
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

1 Mwanzo 1 :26

👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆
Nadhani Yeye Mwenyewe Amesema Hapo Juu.......... kwahiyo Kwa Uelewa Wangu Ni YES

Sasa Sijui Kama Kuna Ukanushi wa Hilo Andiko.. Na Kama Kuna Sehemu Nimefanana Na Kiumb Kingine

Wakuu, ni kwa nini hapo umetumika umoja na wingi? Ni Miungu wangapi waliumba mtu? Mungu "akasema" ..halafu...na "tufanye"!!!inakuwaje hapo jamani?
 
Kwa mchango wangu mimi kwenye mada ninaweza kusema kuwa lile ni fumbo.

Kuna mengi sana ukitaka kuyachukulia katika maana ya moja kwa moja utashindwa kutambua undani. Tunda lina maana yake, nyoka ana maana yake, bustani ina maana yake, mazingira yana maana yake, na tendo lenyewe la kula tunda, kufunguka, kuwa kama Mungu, nako kuna maana yake.

Nimewahi kufuatilia kwa kina kuhusu maana yake, nimegundua kuwa wakristu wengi wa sasa wana maana tofauti na wayahudi wa kale. Wayahudi ndio wamiliki wa dhamira na maudhui makuu hasa ya Agano la Kale. Mpaka leo Traditional Judaism ipo, lakini ukijaribu kusoma wao wana mtazamo gani utagundua wamegawanyika. Katika Judaism kuna Kabbalah. Kabbalah ni elimu ya kufunuliwa iliyokuwa inatolewa kwa wachache hasa wale watafutaji wa maana za undani za maisha. Ni elimu ambayo ilikwepo na mfano hata kipindi cha Musa kuna waliokuwa watu kumi ambao Musa alikuwa anazungumza nao na kuchambua ujumbe aliokuwa anapewa na MUngu. Sababu ya kufanya iwe siri ni kuwa sio kila mwanadamu ana uwezo wa kuelewa. Kuna wanadamu wameshikiliwa katika kifungo cha ujinga, mental slavery, na wapo katika giza. Hao wakiuona mwanga wanaweza wakapofuka na kushindwa kuelewa zaidi mwishowe wakapoteza maana kabisa ya uhalisia kwani Mwanadamu anaweza kutengeneza uhalia wake na aka uexperience. Kuhakikisha mafunzo ya Biblia kuhifadhiwa katika ustadi wake wa asili ni kuelezea masimulizi katika hadithi na kumuacha mtu azidi kusoma na kama yeye ni mtafutaji zaidi basi atazidi kutaka kufahamu zaidi na kwa kutumia akili zake binafsi anaweza kuuona mwanga na kutambua uhalisia zaidi..

Katika Kabbalah, ni elimu ya kuelezea undani wa Agano la Lake. Mbali na Hadithi ya Adamu na hawa bado kuna hadithi kama Hadithi ya Musa, Daudi na Goliati, Samsoni, Farao na Wana wa Israel, Yeremia na kadhalika. Sio mazimulizi tu bali ni zaidi ya masimulizi. Kulikuwa na hadithi maelfu lakini ni kwanini walichagua masimulizi hayo? Ni kwa sababu masimulizi hayo yana masimulizi mengine ya ndani. Na masimulizi ya ndani ndio kiini kikuu. Lakini sio lazima kutambua kiini kwani ulimwengu ni illusion na infinite. Huwezi kuumaliza kwa ufahamu wako. Lakini ukitaka kuuelewa elewa ufahamu wako ulivyo kwanza.

Ndio maana ukitazama sasa unajikuta unauliza ni kwanini wanyama nao wanakufa, kwanini Mungu alimuacha Nyoka adanganye na aendelee kupotosha? Je waliambiwa watakufa wakila, je mbona hawakufa kifizikia? Kumbe kuna maana zaidi mfano kufa kiroho zaidi ya kufa kifizikia? Then utagundua kuna message behind.

Hivyo haikuwa hadithi kwamba hapo kale kulikuwa na wanadamu wawili mwanamke na mwanaume walioishi kwenye bustani, wakala tunda walilokatazwa na ulimwengu huu unaangamia kutokana na kosa walilolifanya. NO
 
bila shaka mmeikuta jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.

Adam na hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.

Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..

Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..

Swali kuu ni kwamba je, baada ya adam na hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?

Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?

Najua jf naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.

Nawatakia jumapili njema.
mwanadamu hakuumbwa ili afe..
Ni tofauti na viumbe wengine....
.....kuna vyuo vinafanya utafiti na vina details ''infact sisi binadamu ni kama mbegu huwa tukifa tunatokea katika mwili mwingine hapahapa duniani...itaendelea hivyo mpaka kiama.....#fatilia uzi wangu wa ##ushahidi wa maisha baada ya kifo.
 
wakuu, ni kwa nini hapo umetumika umoja na wingi? Ni miungu wangapi waliumba mtu? Mungu "akasema" ..halafu...na "tufanye"!!!inakuwaje hapo jamani?
ukifananisha mungu na mtu au kitu...hutaipata maana ya mungu....ni zaidi ya umoja na wingi...akili za mwanadamu haziwezi.............
 
Back
Top Bottom