Kwa mchango wangu mimi kwenye mada ninaweza kusema kuwa lile ni fumbo.
Kuna mengi sana ukitaka kuyachukulia katika maana ya moja kwa moja utashindwa kutambua undani. Tunda lina maana yake, nyoka ana maana yake, bustani ina maana yake, mazingira yana maana yake, na tendo lenyewe la kula tunda, kufunguka, kuwa kama Mungu, nako kuna maana yake.
Nimewahi kufuatilia kwa kina kuhusu maana yake, nimegundua kuwa wakristu wengi wa sasa wana maana tofauti na wayahudi wa kale. Wayahudi ndio wamiliki wa dhamira na maudhui makuu hasa ya Agano la Kale. Mpaka leo Traditional Judaism ipo, lakini ukijaribu kusoma wao wana mtazamo gani utagundua wamegawanyika. Katika Judaism kuna Kabbalah. Kabbalah ni elimu ya kufunuliwa iliyokuwa inatolewa kwa wachache hasa wale watafutaji wa maana za undani za maisha. Ni elimu ambayo ilikwepo na mfano hata kipindi cha Musa kuna waliokuwa watu kumi ambao Musa alikuwa anazungumza nao na kuchambua ujumbe aliokuwa anapewa na MUngu. Sababu ya kufanya iwe siri ni kuwa sio kila mwanadamu ana uwezo wa kuelewa. Kuna wanadamu wameshikiliwa katika kifungo cha ujinga, mental slavery, na wapo katika giza. Hao wakiuona mwanga wanaweza wakapofuka na kushindwa kuelewa zaidi mwishowe wakapoteza maana kabisa ya uhalisia kwani Mwanadamu anaweza kutengeneza uhalia wake na aka uexperience. Kuhakikisha mafunzo ya Biblia kuhifadhiwa katika ustadi wake wa asili ni kuelezea masimulizi katika hadithi na kumuacha mtu azidi kusoma na kama yeye ni mtafutaji zaidi basi atazidi kutaka kufahamu zaidi na kwa kutumia akili zake binafsi anaweza kuuona mwanga na kutambua uhalisia zaidi..
Katika Kabbalah, ni elimu ya kuelezea undani wa Agano la Lake. Mbali na Hadithi ya Adamu na hawa bado kuna hadithi kama Hadithi ya Musa, Daudi na Goliati, Samsoni, Farao na Wana wa Israel, Yeremia na kadhalika. Sio mazimulizi tu bali ni zaidi ya masimulizi. Kulikuwa na hadithi maelfu lakini ni kwanini walichagua masimulizi hayo? Ni kwa sababu masimulizi hayo yana masimulizi mengine ya ndani. Na masimulizi ya ndani ndio kiini kikuu. Lakini sio lazima kutambua kiini kwani ulimwengu ni illusion na infinite. Huwezi kuumaliza kwa ufahamu wako. Lakini ukitaka kuuelewa elewa ufahamu wako ulivyo kwanza.
Ndio maana ukitazama sasa unajikuta unauliza ni kwanini wanyama nao wanakufa, kwanini Mungu alimuacha Nyoka adanganye na aendelee kupotosha? Je waliambiwa watakufa wakila, je mbona hawakufa kifizikia? Kumbe kuna maana zaidi mfano kufa kiroho zaidi ya kufa kifizikia? Then utagundua kuna message behind.
Hivyo haikuwa hadithi kwamba hapo kale kulikuwa na wanadamu wawili mwanamke na mwanaume walioishi kwenye bustani, wakala tunda walilokatazwa na ulimwengu huu unaangamia kutokana na kosa walilolifanya. NO