Laana ya Adam na Hawa


pengine nisijibu swali,ila nikuongezee utata zaidi kwenye swali lako kwa swali jingine
ni hivi,habari ya Adamu na Hawa na laana waliyopewa,iliandikwa na Nabii Mussa katika kitabu chake cha mwanzo,swali ni jee,Mussa alipata kuyaona wapi hayo yote,au yalipata kuandikwa wapi kabla?
Habari zote za babu wa waebrania,Ibrahimu,Tunazipata kwenye kitabu hicho hicho,na sote tunajua kwamba Ibrahimu alikuwa kabla ya Mussa,miaka mingi tu,tena linakuja swali,Mussa alidownload wapi taarifa hizo?

Point to note:mambo ya kiroho yanahitaji roho kuyatafsiri,habari ya Adamu na Hawa ina mkanganyiko wa kiroho na kimwili hivyo huwezi kupata mtiririko wa stori unaoutaka kama vile unasoma novel!ni hayo
 
By yero

Mimea na viumbe vingine vilianza kufa kabla ya binadamu..






Hayo ni kwa Mujibu wa mafundisho ya imani gani?

Kama alivyosema yero hapo juu.

Nafikiri mkuu ni kwa mujibu wa mafundisho ya common sense.

Fikiria:
Adam na Hawa waliruhusiwa na Mungu kula chochote kile katika ile bustani isipokuwa matunda ya ule mti mmoja tu.

Sasa tunda na mimea ni vitu hai. Vinapoliwa vinakufa. Sijui kama menu ya Adam na Hawa ilikuwa inajumlisha ndafu na kitimoto. Kama ni hivyo basi hata wanyama, samaki, nk. walianza kufa kabla ya binadamu.
 
Last edited by a moderator:

1. Sidhani kifo kinatokana na Adamu na Hawa kula tunda.
2. Maana inasomeka: "Siku mkila mtakufa" na wakati hata baada ya kula hilo tunda hawakufa mara moja, waliendelea kuishi.
 
Mkuu storyteller

Unajua watu husoma vitabu vya dini na kuvitafsiri literally.

Vitabu vingi vya dini huandikwa kwa mafumbo. Hadithi ya Adam na Hawa ni metaphor ya kutufundisha tuwe makini na amri/sheria zitolewazo na wakuu/viongozi wetu.

Inatufundisha kwamba hata kama sheria au amri uliyopewa na mkuu wako huipendi, ukiikaidi na kuivunja basi kuna consequences zake.

There was no such thing kama bustani ya Eden. Adam na Hawa hawakuwa physical beings walioishi Eden.

Lakini usinifuate mimi - "nimepotea au nimejipoteza", sina dini.
 

Naomban niongezee hapo kwenye mabano mkuu,Kwa ufahamu wangu mie na amini ilo ndio kosa kubwa,Wangeomba radhi nadhani wangesamehewa kwani huyu Mungu ni mwenye huruma,kwa nukuu ya bibilia takatifu.

Jambo lingine ambalo kubwa zaidi ni kuwa tunapenda kulaumu sana kwa kila kitu katika maisha.Na hii ndio dhambi kubwa tulionayo mpaka sasa.Kwani Mungu alimuuliza Adam kwa nini umekula tundaaa?.Akajibu ni Mwanamke ndo alionipa,Akamgeukia Eva na wewe kwa nini umekula tunda nae akasema ni nyoka.

Kwa kifupi Adam anamlalamikia Mungu kama usinge muumba Eva basi mimi nisingekula Tunda,na Eva nae ana mlalamikia Mungu kama usingemuumba nyoka basi nisinge kula tunda.

Hata humu kwenye JF,hasa kwenye hii mada watu wanalaumiana sana.
 
1. Sidhani kifo kinatokana na Adamu na Hawa kula tunda.
2. Maana inasomeka: "Siku mkila mtakufa" na wakati hata baada ya kula hilo tunda hawakufa mara moja, waliendelea kuishi.

Mkuu naomba kuchangia kidogo kwa hii mada,Ni kweli Mungu alimaanisha siku wakila tunda watakufaa,na Walikufa siku hiyohiyo.Na nukuu kutoka kwa bibilia "MIAKA ELFU MOJA KWA MWANADAMU NI SAWA NA SIKU MOJA KWANGU,NA SIKU MOJA KWA MWANADAMU NI SAWA NA MIAKA ELFU MOJA KWANGU KWA ATAKAE TUBU'Mwisho wa kunukuuu.

Katika historia ndani Bibilia kama referrence yetu,hakuna mtu alie ishi miaka zaidi ya elfu moja,na alieishi mingi ni Methusela,aliekufa na miaka miatisa sitini na tisa.kwa hio Mwenye enzi Mungu halimaanisha na hakuna atakae toboa miaka elfu moja ambayo ni siku moja kwa Mungu.

Karibu kwa mchango zaid au swali mkuu
 

Ni kweli mkuu,kwa common sense nakubaliana na wewe
 
Kuna vitu vingine ni ngumu kuingia kichwani. Muda mwingine hizi dini zinaongeza maswali yasiyo na majibu ukianza fikiria critically. Hivi si Adamu na Hawa waliambiwa wakazaliane? Sasa kama kusingekuwa na kufa, hii dunia ingekuwaje na itakuwaje? Hivi yule Kaini baada ya kumuua mwenzake Abeli alienda akazaa na nani wakati tumeambiwa walizaliwa watatu tena wote wanaume (Kaini, Abeli na Seth)??
 

Mkuu ktk mambo ya Kiroho ni lazima umshirikishe Roho Mtakatifu ili kuweza kuyaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…