Laana ya mtandao na kuvurugika kwa chaguzi za chama: 1995-2025

Laana ya mtandao na kuvurugika kwa chaguzi za chama: 1995-2025

Mkuu, Suluhisho la kweli ni kuimarisha utamaduni wa mchujo huru ndani ya chama kwa kuhakikisha kila mgombea anapita kwenye mchakato wa wazi na unaosimamiwa kwa uwazi.

Mfano tunaweza kujifunza kutoka Marekani ambapo primaries zinafanyika kwa uwazi mkubwa, zikihusisha wanachama wote na matokeo kutangazwa hadharani. Hii itasaidia kupunguza nguvu za mitandao ya kifisadi inayojipenyeza kimyakimya.

Njia nyingine ni kuunda kamati za uchunguzi wa wanachama watakaogombea nafasi za juu kwa kushirikisha wanachama wa kawaida na asasi za kiraia ili kujenga uhalali na kuzuia mtu mmoja au kikundi kidogo kulazimisha maamuzi. Ujerumani kupitia chama cha SPD kimefanikiwa kwa kutumia kura za maoni kwa wanachama wote kabla ya kumuidhinisha mgombea, jambo ambalo limeongeza uwazi na mshikamano wa ndani ya chama.

Teknolojia inaweza kutumika kuongeza uwazi na usalama wa kura. Estonia imepiga hatua kubwa kwa kutumia kura za mtandaoni zenye usalama wa blockchain, na mfumo kama huo unaweza kusaidia hata vyama vyetu kuhakikisha matokeo hayabadilishwi. Hii ikijumuishwa na elimu ya wanachama kuhusu haki zao na taratibu za uchaguzi ndani ya chama, kama ambavyo Afrika Kusini imekuwa ikifanya kupitia warsha na semina, inaweza kuondoa ujinga unaotumiwa na mitandao ya kifisadi.

Tunisia baada ya mapinduzi ya 2011 ilibadilisha katiba ya vyama na kuanzisha vikao vya wazi kwa wanachama wote, hali iliyosaidia kuongeza mshikamano na kupunguza nguvu za makundi ya kifisadi. Hatua kama hizi zinaweza kuondoa kabisa nguvu za “mtandao” na kujenga demokrasia ya kweli inayotegemea ushiriki wa wanachama wote.

Nimetoa tu suggestions japokuwa mimi sio mwanachama wala muumini wa hicho chama
 
Q
Haya yanayotokea Kwa CHADEMA ni kama ni sehemu ya mkakati maana Lissu hajawahi kuwa na "connection " na watoto wa mjini.

Watu wanadhani CHADEMA inashambuliwa ili CCM ishinde, kumbe inashambuliwa ili mtandao usivurugwe na "mlugaluga" asiye na simile au kujua siasa za wahuni (Kwa mtazamo wa Polepole) zinavyoendeshwa.
😂😂😂
 
Nafikiri ni tarehe 12/07/2024 ulichangia kwenye mojawapo ya Uzi na mchango wako ulikuwa ni:

"How to deal with a rougue & corrupt intelligence agency."

Ulichokiandika leo hakitofautiani na ulichokiandika kipindi hicho, na daima na huo ndiyo ulibakia kuwa msimamo wangu.

Ukitazama kwa mapana nchi inakoelekea si pazuri, na sijui huyo Mzee ananufaika na nini kuharibu nchi kwa namna hiyo.

Nafikiri wakati umefika sasa wa kujifunza kwa lugha ngumu. Naunga mkono hoja yako!
------------
Nimepitia moja ya kitabu ulichopendekeza kisomwe "A brief History of Humankind Sapiens" cha Yuval Noah Harari, mwanzoni kimenikata pumzi! "An Animal of No Significance"
 
...njia ni moja tu, kufunga madirisha ya nyumba na KUPULIZA SUMU, kisha kufunga mlango.

Asante Mleta mada, kwa muda na hoja yako hii.

Hitimisho la mada linatafakarisha. Najaribu kufikiria mbadala wake yaani njia ya pili!

Labda, kama hao panya wamezoea kula mahindi yetu ndani kwa nini tusiwafanyie GME (genetic modification engineering) ya wao kuanza kula mbu na mende kama chakula chao na hao mende na mbu tuwafanyie GME wakiona panya wajipeleke kwake kama mbwa kamuona Chatu? Pia kama kuna paka shume mla vifaranga vya kuku, naye Tumfanyie GME aanze kula panya tu...! Na mifano mingine na mingine...lengo badala ya kupoteza ecosystem hasi tuifanyie tu GME hiyo ecosystem iwe chanya.

Nina imani nimesomeka.
 
Mwaka 1996 nyumbani kwetu Kintinku kulikuwa na wadudu wengi ndani ya Nyumba ikabdi wazazi wakubaliane wamatafute mtu wa kupiga dawa, ila walipewa sharti la kufunga kila eneo la wazi ili hewa isiingie na wadudu wengine wasikimbie nje maana makali ya sumu yakishaisha wanaweza kurudi kuja kuzaliana tena.

Baada ya makubaliano mwenye solo lake yaani lile bomba la kupulizia tulikuwa tunaliita solo na linatumia betri za kawaida unaliwasha, baada kupuliza hatukuruhusiwa kuingia ndani masaa 8 hadi wadudu wote walipoteketea na kuja kuanza kufagia tu.

Tusubiri deal done!
 
Kila siku nasema. Tungekuwa na TISS wenye akili nchi hii ingekuwa The Most developed country in Africa.

Kukosa kwao akili na kushindwa kuzuia hatari kwa wakati kunaligharimu na kutaligharimu hili Taifa milele.
Wapo wenye nia njema na wazalendo lakini wapo kimya wasijulikane wapo upande upi au kupinga kwa kuhofia mapandikizi miongoni mwao, ni kama hawaaminiani tena...
 
Back
Top Bottom