Laana ya mtandao na kuvurugika kwa chaguzi za chama: 1995-2025

Laana ya mtandao na kuvurugika kwa chaguzi za chama: 1995-2025

Naam hakuna njia nyingine zaidi ya haya inabidi nchi wapewe chama pinzani ilikuwa hizo siasa za huyo master mind zilizopo ktk chama tawala

La sivyo kumuondoa master mind pekee na Head of state pekee haitoshi maana tayari Kuna wafuasi wao ambao wameshaiga falsafa zao na endapo wakiachwa wazitumie nchi itarudi kule kule ama zaidi ya kule

Ila Sasa swali la kujiuliza ninani wa KUMFUNGA PAKA KENGELE !!?
Je kama jamaa ana control hadi huko??????😀
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA , umeandika kwa urefu lakini kilicho ndani ya andiko lako hili ni somo zito lisilohitaji kubishaniwa. Hapa si tu tunazungumzia mtu au kundi, bali mfumo uliotekwa na mpango wa muda mrefu, uliopandikizwa polepole, ukakua kimyakimya, na sasa umejigeuza kuwa “utaratibu mpya” kwa jina tu la utaratibu wa chama.

Unachokiita "laana" ni matokeo ya kuendelea kwa hali ya kuaminiana kwa nje, lakini kuvunjiana misingi kwa ndani. Hili si jambo la ajali tena , ni mkakati unaojirudia kwa ustadi wa hali ya juu, ukitumia kila nyenzo ya kisasa ya nguvu, uteuzi, propaganda, ushawishi wa kimyakimya, na taasisi zilizo kando ya mfumo rasmi.

Ninchofikiri, kilichobaki sasa si majina, bali urithi wa mfumo usiobadilika kwa miongo mitatu, unaojigeuza sura kila kipindi lakini ukibaki na roho ileile. Upo sahihi, hapa hatuhitaji mjadala, tunahitaji uamuzi mgumu unaoangalia afya ya nchi kuliko usalama wa kikundi au watu wachache. Wakati mwingine, hatua fulani huenda isiwe sahihi mbele ya macho ya siasa, lakini huwa ni hitaji lisiloepukika katika mkondo wa historia.
MKUU NYOKA HATA AWE MREFU VIPI NGUVU ZAKE ZIKI KICHWANI,TUPASUE KICHWA MWILI NA UREFU WAKE TUTAUMEGA TARATIBU KIMKAKATI.TUKATENI KICHWA
 
Haya yanayotokea Kwa CHADEMA ni kama ni sehemu ya mkakati maana Lissu hajawahi kuwa na "connection " na watoto wa mjini.

Watu wanadhani CHADEMA inashambuliwa ili CCM ishinde, kumbe inashambuliwa ili mtandao usivurugwe na "mlugaluga" asiye na simile au kujua siasa za wahuni (Kwa mtazamo wa Polepole) zinavyoendeshwa.
Mkuu, ni muhimu sana kubakisha maneno (usimalize yote). refer (Mch Msigwa, Dkt Slaa, FAM) hawa watu waliaminika sana aiseee
 
Mkongwe MALCOM LUMUMBA kongole kwa uzi jadidi wenye hadhi ya kuwepo jukwaa hili. Umeandika vizuri sana khs mtandao kuanzia sarakasi za 95 mpaka leo hii. Ni dhahiri shahiri kuwa ata huyu bwana akiondoka bado mazalia ya mtandao yatautesa na kulisumbua sana taifa hili.

Na jambo ambalo sina shaka huyu bwana na waasisi wenzie wa mtandao wamelifanya/wanalifanya ni kujua kuwa kuna kifo/kuzeeka au plans hii kufeli ivyo lazma plan nyingine iwe installed ili kuendelea kukita mizizi ya mtandao wao.

Ndio maana leo hii ukimakinika sana kuwafatilia ata wanasiasa vijana wanaoonekana kujijenga na ata kufanikiwa kiumaarufu na ushawishi katika taifa wengi wao(si wote) ni wana mtandao (hii kwa wapinzani na chama dola). Ni moja ya ishara kuwa hawa watu wamejipanga mtandao huu kuwepo leo, kesho na ata mtondogoo ata kama majina fulani fulani yatakua yanapotea ktk ulimwengu huu.

Mengi ya kuandika lakini niishie hapa. Je hii hatari koridoni hawaioni, hawaijui? Jibu ni wanayajua..walipuuza tangu wakati ule mpaka sasa limegeuka dubwasha kubwa sana. Kwa sasa tulipofikia ni nani hao wa kusafisha nyumba ??
 
Kind of Ethnic cleansing inahitajika.
Je hii hatari koridoni hawaioni, hawaijui? Jibu ni wanayajua..walipuuza tangu wakati ule mpaka sasa limegeuka dubwasha kubwa sana. Kwa sasa tulipofikia ni nani hao wa kusafisha nyumba ??
 
Ndio ukweli Mkuu, mimi naongelea kuaminika. aliaminika na there is no doubt about that.
Kwa waliowahi kuwa karibu naye walikuwa wanamheshimu badala ya kumuamini. Sisi tulio mbali naye ndio tuliokuwa tunamu idolize na kumuamini
 
SIASA ZA MTANDAO ZILIVYOUA JAMHURI YA RUMI YA KALE.

Dola la Rumi kabla ya kuwa Ufalme mkubwa duniani 44 BC, ilikuwa ni Jamhuri inayoongozwa kidemokrasia chini ya Seneti. Kabla ya hapo Rumi ilikuwa nchi ya kifalme, ambayo wafalme waliongoza kama MIUNGU WATU (Divine Right). Mwaka 509 BC, Warumi baada ya kuongozwa na Mfalme Dikteta Jehuri, Tarquinius Superbus, walijikusanya wakampindua na kumfukuza.

Warumi walitengeneza Jamhuri ya Kwanza (First Republic) duniani ambayo iliongozwa na kiongozi wa kuteuliwa (Consul), ambaye alikaa muda fulani kisha kuondoka. Utaratibu huu uliendelee kwa zaidi ya miaka 300 na Rumi ikafanikiwa mno. Ndani ya Seneti kulikuwa na makundi mawili, Optimates na Populares, ambayo ndiyo yalitoa wabunge wa majimbo.

Rumi lilikuwa ni taifa kubwa lililofanikiwa kwasababu, waliweza kuanzisha mfumo wa MERITOCRACY. Ambapo mtu aliyezaliwa tabaka la chini angeweza kufika tabaka la kutawala kama alikuwa na kipaji cha kijeshi, dini, sanaa au kuasiriwa (Adopted) na mtu wa tabaka la juu. Mfumo huu, uliweza kufanya warumi kuwa taifa lenye watu wenye uwezo mkubwa kiongozi.

MWANZO WA MATATIZO: Mwaka 60 BC, baada ya Jamhuri ya Rumi kufanikiwa kwa miaka mingi, kuna vijana watatu (Julius Ceaser, Gnaius Pompey na Marcus Crassus) walichipukia kwa nguvu kwenye siasa za nchi. Vijana hawa walikuwa hawana nguvu ya kushindana na wanasiasa wakongwe ndani ya Seneti ya Rumi ambao wengi walikuwa ni wanafalsafa nguli kama Cicero.

Hawa vijana wakaanzisha siasa za fitna na kuunda umoja wao uliotwa The First Roman Triumvirate, ambapo walikubaliana kuunganisha nguvu zao ili kuwala Rumi kihuni. Mtandao wa wao, The Triumvirate ulikuwa na nguvu kubwa kwasababu, Julius Ceaser alikuwa ni KUHANI MKUU WA RUMI (Pontifex Maximus), Gnaius Pompey alikuwa JENERALI ALIYESHINDA VITA (Roman Imperator), na Marcus Crassus akiwa TAJIRI MKUBWA (Richest Man In Rome).

Huu MTANDAO ulikuwa na nguvu kubwa mno na kuanza kuvuruga siasa za Rumi, kwa kutumia rushwa, ngono, utekaji, siasa za kuchafuana na uchawa kutishia watu. Hawa vijana watatu waliratibu makundi ya wahuni waliofanya fujo, kisha wao kuja kusawazisha na kuonekana wao ndiyo suluhu. Walifanikiwa kushika nchi, na Pompey akawa kiongozi mkuu (Consul).

Tatizo likatokea pale hawa vijana waliposhindwa kushirikishana madaraka (Power Sharing). Pompey alikuwa Consul na uwezo wake kijeshi ulikuwa mkubwa mno kuliko Ceaser na Crassus. Ceaser akaamua kuingiza nchi kwenye vita ili avunje rekodi ya Pompey pamoja na kulipa madeni ya watu aliyokopa wakati wa siasa chafu za Triumvirate.

Baada ya kuvunja sheria za nchi Ceaser alichukua vikosi vya kijeshi kinyume na Seneti na kuvamia BRITTANICA (Uingereza) ili tu kujenga jina kubwa kuliko Pompey. Alifanikiwa kuvamia GAUL (Ufaransa/Spain) na BRITTANICA na kupewa cheo cha JENERALI ALIYESHINDA VITA (Roman Imperator).

Crassus naye hakuwa nyuma, akachukua wanajeshi wasiopungua 40,000 akaenda kuvamia dola la Uajemi la Kiparthi (Parthian Empire) ili kufikia mafanikio ya kijeshi ya Ceaser na Pompey. Alitumia fedha zake binafsi kuendesha hii vita, lakini iliishia vibaya mno baada ya Warumi zaidi ya 40,000 kuuwawa kinyama, huku yeye pia akimwagiwa dhahabu iliyoyeyuka (Molten Gold) kichwani.

==========================================
Wakabaki Ceaser na Pompey, siasa zao zikaigawa Rumi.

Hapo zamani ili kuzuia uhaini, Seneti ya Rumi iliweka utaratibu kwamba kuna mipaka ndani ya nchi ambayo wanajeshi hawataki kuvuka na vikosi vyao na kuingia navyo Rumi. Ceaser baada ya kuona Pompey kama kiongozi wa nchi ameishawishi Seneti imuadhibu kwa kuanzisha vita, akaavusha vikosi vyake kwenye mpaka uitwao,The Rubbicon.

Rumi iligubikwa na Civil War kubwa kisa MTANDAO wa watu watatu, The Triumvirate ambao ulifundisha watu tabia za kutotii katiba na sheria, pamoja na kutumia mbinu yoyote ile kupata madaraka. Miaka 4, walipigana maelfu ya watu wakafa, na mwishowe Ceaser akaibuka mshindi.

MADHARA YA SIASA ZA MTANDAO: Ceaser alipoibuka mshindi alijigeuza Dikteta (Benevolent Dictator), jambo ambalo liliwakera Warumi wengi hasa wabunge wa majimbo. Chawa wake kama Mark Anthony wakaanza kupendekeza Ceaser awe mfalme kabisa, wakijifanya wanatania. Wabunge kama Cicero walikereka mno na hichi kitendo kwasababu kilivunja misingi ambayo ilidumu kwa miaka zaidi ya 300. Wazee na Wahenga wao, walilipia gharama kubwa kufukuza wafalme na kuanzisha Jamhuri, iweje Ceaser atake kujigeuza Mfalme ?

NJAMA YA KUIOKOA RUMI: Wabunge wa Rumi, wakiwemo marafiki wa karibu na Ceaser kama Brutus, waliamua kuiweka Jamhuri mbele kuliko uswahiba. Wakapanga njama ya kumuua Ceaser. Mwaka mmoja kabla, zilianza kutolewa nabii kutoka kwa waaaguzi mbalimbali waliomwambia Ceaser kwamba atakufa mwezi Machi (Beware of the Odes of March), lakini aliwapuuza.

Mwezi Machi ukafika baada ya mwaka kupita, Ceaser akamfuata yule mwanamke muaguzi na kumcheka huku akikashifu kwamba nimefika Machi na sijafa. Ceaser alikuwa ni BRILLIANT STRATEGIST, and AN EXCELLENT STATESMAN. Alikuwa anakubalika sana na makundi ya watu ndani ya nchi kwasababu alijionesha yeye ni mtu poa anayetaka kila mtu apate. Sifa yake kubwa ilikuwa ni kupenda kulala na wanawake wengi, wakampa jina The Bald Fornicator.

Siku hiyo, Ceaser anamkashifu Mwaguzi, huku akielekea bungeni ndiyo ulikuwa mwisho wake. Alivyoingia bungeni, wabunge wakatoa visu na kuanza kumchoma na kumuua. Alishangaa kumuona rafiki yake Brutus, ambaye aliamua kuiweka Jamhuri mbele. Ceaser akafa na huo ndiyo ukawa mwisho wake.

MATATIZO YA MTANDAO YANAENDELEA: Wabunge kwa kumuua Ceaser, walidhani wangemaliza matatizo kumbe madhara ya siasa za MTANDAO, The Triumvirate yalikuwa makubwa mno. Wanajeshi walifundishwa kupuuza wabunge na kutumia nguvu kupata chochote. Wafuasi wa Ceaser wakiongozwa na Mark Anthony wakaanza kampeni za kijeshi za kulipiza kisasi, ambazo zilisababisha Civil War nyingine ambayo iliwaua kina Brutus na Cicero.

Hata baada ya wapinzani wa Ceaser kuuawa, Rumi haikupona. Machawa wa Ceaser wenyewe nao wakageukana kila mtu akitaka kutawala Rumi. Mpwa wa Ceaser, Octavian, ambaye alikuja kuwa Kaisari wa kwanza wa Rumi (Roman Ceaser Augustus) alipambana na Mark Anthony na kumshinda.

Octavian baada ya kushinda vita, akaitisha Seneti na kuwaambia wachague wampe uongozi wa kudumu wa Rumi (Consul for Life) ambapo walikubali kwa woga. Mwishowe akajigeuza kuwa Mfalme (Emperor) na Jamhuri ya Rumi ikafa, likazaliwa dola la Rumi (Roman Empire). Kitu ambacho Warumi walikuwa wanakiogopa kwa miaka za ya 300, kikawatokea kisa siasa za MTANDAO wa watu watatu tu.

==============================================
Kuna mengi ya kujifunza hapa. Hakuna MKUBWA KULIKO NCHI, na hapa tulipofika hatuwezi kukwepa maswaibu ya MTANDAO uliojijenga nchini kwa miaka zaidi ya miongo mitatu.




Sic Semper Tyrannus ​
afu mbona hii ni script ya yanayo endelea hapa cuba
 
Ndiomana nilishangaa mtu kateuliwa kuwa waziri wa pesa kwenye hotuba yake ya kwanza anaanza kumshukuru mwenyekit mstaafu alafu nyuma kidogo alishasikika akimuomba poo mwenyekit mstaafu nafkir Ile poo ilkubalia yule wazir aliendelea kudumu na akaweka historia ya signature kwenye karatasi za bi-o-tii
 
hata yeye anatumwa na kutumiwa tu, anayechezesha mwanasesere ni mpersia, huyo ndiyo the root cause of all evil in tanzagiza …
Hizi ID hizi ...zenye JF posting rate ya 1.18 per day. Tusome maoni yake kwa utuo maana yake zimebeba 'madini'.
 
Back
Top Bottom