Laana ya mtandao na kuvurugika kwa chaguzi za chama: 1995-2025

Na ndiyo ukweli waliokuwa mbali naye walikuwa wakimweshimu. Kumbuka Sio kila mtu atapata previlage ya kuwa karibu na FAM, TAL, JK., JPM, SSH nk nk ...
Watu wengi wakubwa niliopata bahati ya kuwa karibu nao nilipoteza hali ya kuwaheshimu kuanzia siku hiyo hiyo baada ya kugundua na wao ni viazi kama regula people.
 
Sahihi sana Mkuu.. wengi wao ni wa kawaida tu. Ndio maaana nilimwambia mu mmoja humu hata TAL wasimu idolize sana... viongozi kwenye TV ni tofauti na walivyo kabisa;
 
Suluhisho ni kuvunja hizo pattern/mazoea

When we break a pattern we create a space for possibility.
 
"Once is an accident. Twice is a coincidence. Thrice is a pattern"

Watanzania tumefika hapa kwasababu ni watu tunaopenda kupuuza mambo, kutokufikiria ipasavyo na kuendesha maisha yetu kimazoea. Binafsi huwa naamini kama tungekuwa hatupuuzi mambo kuna watu wasingediriki hata kuomba ridhaa ya kututawala. Hebu angalia huu mlolongo, halafu fikiria kama kuna bahati mbaya yoyote.

Mwaka 1995, uchaguzi wa mgombea Uraisi ndani ya CCM, huyu BWANA alikuwepo. Yeye na MTANDAO wake wakiwa vijana kabisa walifanya jaribio la kutaka wamsimike kuwa mgombea lakini wakazuiwa na kundi la wakubwa lililoongozwa na KAISARI. Kiukweli alishinda, lakini KAISARI alimdhibiti na kwasababu ni mjanja alikubali kushindwa.

Mwaka 2005, KAISARI hayupo. BWANA huyu na MTANDAO wake walifanya vurugu za kukipasua chama vipande-vipande. Walianza kujipanga kimya-kimya tokea mwaka 1995 hadi 2005, wakitumia mbinu chafu kama Rushwa, Mauaji, Ngono, Vitisho, Ahadi, Ushirikina na Propaganda. Watanzania walipuuza hii michezo ambayo ilifanywa na vibaraka wa MTANDAO walioko kwenye taasisi nyeti za dola, asasi za kiraia, taasisi za kidini na sekta binafsi.

Kipindi hiki BWANA huyu hakufanikiwa kuvuruga tu uchaguzi ndani ya chama, bali aina mbinu hizi alizihamishia hadi kwenye utawala wake ambao tulishuhudia nchi ikiendeshwa kama genge la YAKUZA. Siasa za chuki na makundi, rushwa iliyokithiri, uzembe kazini na siasa za kichawa zilianza na huyu BWANA. Watanzania kwasababu ni watu wakupuuza haya hatupendi kuyasikiliza au kuyajadili.

Mwaka 2015, BWANA huyu na MTANDAO wake waliamua kuvuruga kwa maksudi uchaguzi wa mgombea wa Uraisi. Hapa Afrika Mashariki, CHAMA ni moja ya taasisi kubwa zenye watu wenye akili na weledi. Wengi wao waliomba ridhaa kugombea Uraisi wa nchi, lakini MTANDAO ulioaanza 1995 ukawavuruga mchakato mzima. Mgombea aliyepatikana alikuwa ni wa SHINIKIZO LA WASTAAFU na BAHATI MBAYA.

Ila mbali na hayo BWANA huyu hakukubali kushindwa, akaamua kuvuruga mchakato wa MAKAMU. Watanzania na tatizo lao la kupuuza mambo, wakiwemo WASTAAFU hawakujiuliza kwanini BWANA yule amependekeza hivi kuhusu MAKAMU. Mgombea alikuwa wa BAHATI MBAYA/SHINIKIZO lakini MAKAMU alikuwa yupo KIMKAKATI.

Mwaka 2021, BWANA huyu alifanikiwa tena kuvuruga mchakato ndani ya CHAMA kwasababu mwaka 2015 alifanikiwa kupenyeza Farasi Wa Troa (Trojan Horse) kwenye nafasi ya UMAKAMU. Jambo hili watanzania wengi kwasababu ni watu wanaopenda kupuuza mambo, wakiwemo WASTAAFU hawakuona uzito wake kipindi hicho walikuja kustuka tu BWANA na MTANDAO wake wanajirudisha kwenye USUKANI kinyemela.

Mwaka 2025, BWANA huyu na MTANDAO karudia kufanya yaleyale aliyoyafanya kwenye chaguzi zote za mgombe Uraisi tokea 1995, 2005 na 2015. Jinsi utaratibu ulivyovunjwa mwaka 2015, ndivyo utamaduni umevunjwa 2025 yeye akiwa kinara. MTANDAO utafanya hivi tena 2030 na 2040. Bahati mbaya kipindi hiki watanzania washafahamu kwamba UMAKAMU kumbe ni mkubwa, uwepo wa BALOZI ambaye alikuwa mwana-MTANDAO huko nyuma, imeonekana ni CHANGAMOTO kwa BWANA.

==================================================================

KWENYE ULIMWENGU WA SIASA, SIYO BAHATI MBAYA mtu mmoja kuwepo na kuwa na ushawishi kwenye chaguzi za nafasi ya URAISI kwa kipindi cha miaka isiyopungua 30. Mnaweza mkamuita MWANAMKAKATI, BORN-TOWN, MASTER-MIND, KING-MAKER lakini, jambo ambalo BWANA huyu amefanikiwa kulifanya hata KAISARI kule kwenye kaburi anaona WIVU. Kuwa muhusika mkuu (MAIN PROTAGONIST) kwenye kila CHAGUZI ndani ya CHAMA kuanzia mwaka 1995, 2005, 2015 na 2025, ni jambo ambalo inabidi wanazuoni walifanyie TAFITI.

KINACHOSHANGAZA: Mwaka 2015, wakati BWANA na MTANDAO wamevuruga mchakato mzima wa UCHAGUZI ndani ya CHAMA. Aliyependekezwa UMAKAMU kipindi hiki alitoka nje kupinga mchakato mzima. Lakini mwaka 2025, yeye naye amerudia kufanya kilekile ambacho alikipinga kwa nguvu mwaka 2015.

Tena zaidi CHAMA kimegawanyika kwasababu aliyeratibu mchakato wa kutoa FOMU MOJA KWA MGOMBEA mwaka 2020, kaibuka kupinga uharamu uliofanyika kwenye mchakato wa kumpata mgombea Uraisi mwaka 2025. Yeye naye akipewa nafasi ya kugombea nafasi za juu kupitia njia haramu atanyamaza kama BALOZI mwenzake alivyofanya mwaka 2025.

Anachokifanya BWANA na MTANDAO wake kilifanikiwa tu kufanywa na Dikteta Sani Abacha kule Nigeria ambaye alifanikiwa kuvuruga michakato ya siasa Nigeria tokea mwaka 1966-1998, ambapo alikuwa nyuma ya uhaini (MAIN PROTAGONIST) ulioingiza au kutoa madarakani MARAISI 10 akiwemo na yeye.

CHAMA kumuweka BALOZI Uraisi kupitia UMAKAMU ni kijidanganya tu. CHAMA kilimuweka TINGATINGA lakini bado LAANA YA MTANDAO haikukiacha CHAMA, SERIKALI na NCHI. Mkishavunja utaratibu ndani ya CHAMA msidhani mtaweza kupambana na watu kama BWANA na MTANDAO.

Mpaka leo hii siasa za Nigeria zimekuwa ngumu kwasababu ya Sani Abacha na mtandao aliouacha. Hivyo hata kama BWANA ataondoka, madhara ambayo MTANDAO wake umeuacha kwa zaidi ya miaka 30 yataendelea kuiumiza NCHI, CHAMA na SERIKALI kwa miaka mingi mbele.

===============================================================
KIUFUPI TULIPOFIKA: Ili kuisadia nchi hapa ilipofika ni kufanya UWENDAWAZIMU (Doing the unthinkable). Hatuna utofauti na koloni la wakoma (A Leppers' Colony) ambapo huwezi kutofautisha baina ya mtu aliye MZIMA na MGONJWA. Katika mazingira kama haya, njia ni moja tu, kufunga madirisha ya nyumba na KUPULIZA SUMU, kisha kufunga mlango.

SUMU itaua WATOTO UNAOWAPENDA, itaua WATOTO WASIO NA KOSA, itaua WAGENI WALIOHAMIA, itaua DADA WA KAZI, itaua PANYA, itaua CHAWA, itaua WANYAMA na itaharibu CHAKULA na nyumba haitakalika kwa muda, lakini UGONJWA utakuwa umetoka na hautaweza kusambaa zaidi.

HAKUNA NJIA NYINGINE NJE YA HII.
​
" Katika mazingira kama haya, njia ni moja tu, kufunga madirisha ya nyumba na KUPULIZA SUMU, kisha kufunga mlango."
 
Taifa limeshazama sasa kulikwamua ndo mtihani mkubwa kwa marais wajao kwenye hii miaka 10 ijayo wataonja joto ya JK.Ata matusi anayotukanwa sa100 ni matokeo ya mtandao wa JK kufyonza rasilimali na watu wanaongezeka rasilimali zinapungua.Tunakoenda ni pabaya saaana.
 
Mimi naona Nyerere ndio alikuwa chanzo cha haya mambo. Yeye alitengeneza mfumo wa one mashow toka enzi hizo na walio kuna wamepita humo humo.
Hakupaswa kukaa miaka yote ile ya 25+
 
Mko nchi gani mbona hamridhiki na matunda ya ardhi yenu.

Mimi siwezi kuipinga nchi yangu nakula, nakunywa, napata hela, naona fursa, naoa, nazalisha, napenda, napenda, nafanya miamala, nalala. sijaona kosa la mfumo nimeridhika na maisha hayahaya
Akili kubwa
Haya ndio maisha ya mtafutaji...
Kuna vilaza wengi nchi hii hawajui cha kufanya, kwa hio hapo ndio akili zao zinachotwa na matamshi ya mihemko anapotokea mlopokaji mmoja kama HITLER.....
Ukiwasika mara hii nchi kiwake tu tutaelewana, sijui imwage damu ndio ushindi...
Hizi kenge zinazosema hivi hazijui kuwa hizo pilika zitawahusu wao, ila huyo mlopokaji ameshajitengenezea mahali pa kukimbilia.....
 
"Once is an accident. Twice is a coincidence. Thrice is a pattern"

Watanzania tumefika hapa kwasababu ni watu tunaopenda kupuuza mambo, kutokufikiria ipasavyo na kuendesha maisha yetu kimazoea. Binafsi huwa naamini kama tungekuwa hatupuuzi mambo kuna watu wasingediriki hata kuomba ridhaa ya kututawala. Hebu angalia huu mlolongo, halafu fikiria kama kuna bahati mbaya yoyote.

Mwaka 1995, uchaguzi wa mgombea Uraisi ndani ya CCM, huyu BWANA alikuwepo. Yeye na MTANDAO wake wakiwa vijana kabisa walifanya jaribio la kutaka wamsimike kuwa mgombea lakini wakazuiwa na kundi la wakubwa lililoongozwa na KAISARI. Kiukweli alishinda, lakini KAISARI alimdhibiti na kwasababu ni mjanja alikubali kushindwa.

Mwaka 2005, KAISARI hayupo. BWANA huyu na MTANDAO wake walifanya vurugu za kukipasua chama vipande-vipande. Walianza kujipanga kimya-kimya tokea mwaka 1995 hadi 2005, wakitumia mbinu chafu kama Rushwa, Mauaji, Ngono, Vitisho, Ahadi, Ushirikina na Propaganda. Watanzania walipuuza hii michezo ambayo ilifanywa na vibaraka wa MTANDAO walioko kwenye taasisi nyeti za dola, asasi za kiraia, taasisi za kidini na sekta binafsi.

Kipindi hiki BWANA huyu hakufanikiwa kuvuruga tu uchaguzi ndani ya chama, bali aina mbinu hizi alizihamishia hadi kwenye utawala wake ambao tulishuhudia nchi ikiendeshwa kama genge la YAKUZA. Siasa za chuki na makundi, rushwa iliyokithiri, uzembe kazini na siasa za kichawa zilianza na huyu BWANA. Watanzania kwasababu ni watu wakupuuza haya hatupendi kuyasikiliza au kuyajadili.

Mwaka 2015, BWANA huyu na MTANDAO wake waliamua kuvuruga kwa maksudi uchaguzi wa mgombea wa Uraisi. Hapa Afrika Mashariki, CHAMA ni moja ya taasisi kubwa zenye watu wenye akili na weledi. Wengi wao waliomba ridhaa kugombea Uraisi wa nchi, lakini MTANDAO ulioaanza 1995 ukawavuruga mchakato mzima. Mgombea aliyepatikana alikuwa ni wa SHINIKIZO LA WASTAAFU na BAHATI MBAYA.

Ila mbali na hayo BWANA huyu hakukubali kushindwa, akaamua kuvuruga mchakato wa MAKAMU. Watanzania na tatizo lao la kupuuza mambo, wakiwemo WASTAAFU hawakujiuliza kwanini BWANA yule amependekeza hivi kuhusu MAKAMU. Mgombea alikuwa wa BAHATI MBAYA/SHINIKIZO lakini MAKAMU alikuwa yupo KIMKAKATI.

Mwaka 2021, BWANA huyu alifanikiwa tena kuvuruga mchakato ndani ya CHAMA kwasababu mwaka 2015 alifanikiwa kupenyeza Farasi Wa Troa (Trojan Horse) kwenye nafasi ya UMAKAMU. Jambo hili watanzania wengi kwasababu ni watu wanaopenda kupuuza mambo, wakiwemo WASTAAFU hawakuona uzito wake kipindi hicho walikuja kustuka tu BWANA na MTANDAO wake wanajirudisha kwenye USUKANI kinyemela.

Mwaka 2025, BWANA huyu na MTANDAO karudia kufanya yaleyale aliyoyafanya kwenye chaguzi zote za mgombe Uraisi tokea 1995, 2005 na 2015. Jinsi utaratibu ulivyovunjwa mwaka 2015, ndivyo utamaduni umevunjwa 2025 yeye akiwa kinara. MTANDAO utafanya hivi tena 2030 na 2040. Bahati mbaya kipindi hiki watanzania washafahamu kwamba UMAKAMU kumbe ni mkubwa, uwepo wa BALOZI ambaye alikuwa mwana-MTANDAO huko nyuma, imeonekana ni CHANGAMOTO kwa BWANA.

==================================================================

KWENYE ULIMWENGU WA SIASA, SIYO BAHATI MBAYA mtu mmoja kuwepo na kuwa na ushawishi kwenye chaguzi za nafasi ya URAISI kwa kipindi cha miaka isiyopungua 30. Mnaweza mkamuita MWANAMKAKATI, BORN-TOWN, MASTER-MIND, KING-MAKER lakini, jambo ambalo BWANA huyu amefanikiwa kulifanya hata KAISARI kule kwenye kaburi anaona WIVU. Kuwa muhusika mkuu (MAIN PROTAGONIST) kwenye kila CHAGUZI ndani ya CHAMA kuanzia mwaka 1995, 2005, 2015 na 2025, ni jambo ambalo inabidi wanazuoni walifanyie TAFITI.

KINACHOSHANGAZA: Mwaka 2015, wakati BWANA na MTANDAO wamevuruga mchakato mzima wa UCHAGUZI ndani ya CHAMA. Aliyependekezwa UMAKAMU kipindi hiki alitoka nje kupinga mchakato mzima. Lakini mwaka 2025, yeye naye amerudia kufanya kilekile ambacho alikipinga kwa nguvu mwaka 2015.

Tena zaidi CHAMA kimegawanyika kwasababu aliyeratibu mchakato wa kutoa FOMU MOJA KWA MGOMBEA mwaka 2020, kaibuka kupinga uharamu uliofanyika kwenye mchakato wa kumpata mgombea Uraisi mwaka 2025. Yeye naye akipewa nafasi ya kugombea nafasi za juu kupitia njia haramu atanyamaza kama BALOZI mwenzake alivyofanya mwaka 2025.

==================================================================
Anachokifanya BWANA na MTANDAO wake kilifanikiwa tu kufanywa na Dikteta Sani Abacha kule Nigeria ambaye alifanikiwa kuvuruga michakato ya siasa Nigeria tokea mwaka 1966-1998, ambapo alikuwa nyuma ya uhaini (MAIN PROTAGONIST) ulioingiza au kutoa madarakani MARAISI 10 akiwemo na yeye.

CHAMA kumuweka BALOZI Uraisi kupitia UMAKAMU ni kijidanganya tu. CHAMA kilimuweka TINGATINGA lakini bado LAANA YA MTANDAO haikukiacha CHAMA, SERIKALI na NCHI. Mkishavunja utaratibu ndani ya CHAMA msidhani mtaweza kupambana na watu kama BWANA na MTANDAO.

Mpaka leo hii siasa za Nigeria zimekuwa ngumu kwasababu ya Sani Abacha na mtandao aliouacha. Hivyo hata kama BWANA ataondoka, madhara ambayo MTANDAO wake umeuacha kwa zaidi ya miaka 30 yataendelea kuiumiza NCHI, CHAMA na SERIKALI kwa miaka mingi mbele.

===============================================================
KIUFUPI TULIPOFIKA: Ili kuisadia nchi hapa ilipofika ni kufanya UWENDAWAZIMU (Doing the unthinkable). Hatuna utofauti na koloni la wakoma (A Leppers' Colony) ambapo huwezi kutofautisha baina ya mtu aliye MZIMA na MGONJWA. Katika mazingira kama haya, njia ni moja tu, kufunga madirisha ya nyumba na KUPULIZA SUMU, kisha kufunga mlango.

SUMU itaua WATOTO UNAOWAPENDA, itaua WATOTO WASIO NA KOSA, itaua WAGENI WALIOHAMIA, itaua DADA WA KAZI, itaua PANYA, itaua CHAWA, itaua WANYAMA na itaharibu CHAKULA na nyumba haitakalika kwa muda, lakini UGONJWA utakuwa umetoka na hautaweza kusambaa zaidi.

HAKUNA NJIA NYINGINE NJE YA HII.
​
KAISARI = Nyerere
BWANA = Kikwete
BALOZI = Nchimbi
MRATIBU WA FOMU MOJA 2020: Pole Pole

Kifupi ccm kama CHAMA kimenasa kwenye mtandao wa uasi, ufisadi, dhuluma, laana!
Dawa ni KUJIFUNGIA NDANI na kupuliza sumu!
 
Back
Top Bottom