Kaka Malcom, hizi nguvu tunazo tumia tungejitahidi kuzielekeza ktk mambo ya kweli na kuondoa dhana zisizo na ushahidi.
Makala ni ndefu nitajaribu changia ktk nukta za msingi kwa nitakavyoweza.
Nukta ya kwanza ya msingi ni CCM mtandao na rais wa awamu ya 4, kosa lake hapo ni kugombea 1995, kisha kuonekana tena ktk uchaguzi 2005 na ule 2015 na chaguzi za sasa. Kwanza fact zipo wazi na mwenyewe anajisemea uchaguzi wa mwaka 1995 hakuwa na nia, alifuatwa na kushawishiwa na vijana wenzake wa wakati huo, kisha akashindwa kuwakatalia akaingia ktk uchaguzi..na hapa kosa kubwa wanalo sakamwa nalo ni kuwa walipanga kuutaka urais nje ya utaratibu wa chama kwa wao kushawishiana! Lakini jambo hilo hakufanya kikwete na kina Lowasa peke yake. Jenerali ulimwengu, Mzee Warioba, Na Benjamini Mkapa walipanga na wao kuusaka urais kama vile kikwete na kina Lowasa walivyo fanya, tazama interview hapo chini kuanzia dk ya 30 hivi kwa hoja hii, ukiwezasikiliza yote kwa faida nyinginezo. Na hatima ikawa upande wa kina Mkapa wakashinda na wakapata urais! Shida ya kuwa kina Kikwete na wenzake ni hatari ina anzia wapi? kama wana makosa ya jinai wakamatwe si haya kupanga uongozi kila pande inapanga mgombea wake! Miaka imeenda Mkapa kamaliza urais wake, upande wa kina Kikwete ukashainda! na Kikwete akawa rais. Laiti dhana ya mtandao ingelikuwa na nguvu nadhani Kikwete asingekubali kumtoa swahiba wake ktk uwaziri mkuu, oka tuseme ilikua ni mkakati wa kumlinda Lowasa kisiasa, kama mtandao kweli una kwanini hajamuachia Lowasa kiti cha urais 2015?
Katika hoja yako, unaonesha Kikwete ali play role ktk uchaguzi wa 19995 bila mafanikio, na kisha akaja play role 2005 akashinda, na umamuhusisha tena na 2015! Unasahau 2015 kuwa alikuwa ndio rais na Mwenyekiti wa chama hivyo alikuwa hakwepeki ktk aamuzi hayo! Na nadhani hoja yako ni kwanini mtu huyohuyo katika chaguzi zote hizo za miaka tofauti? Lakini kwanini umseme kikwete peke yake? Mbona tunao viongozi wengi wamehusika ktk chaguzi za miaka tofauti kwasababu ya nafasi zao au kwakuwa wao walikuwa marais, Nakupa mifano kadhaa hapa la baadhi ya viongozi hao.
Mfano wa kwanza ni Mzee Warioba, alihusika ktk kupatikana kwa Mkpa kama mgombea urais mwaka 1995, sikiliza interview hapo chini. Pili kama umesikiliza press conference za Polepole Mzee Warioba pia alihusika kupatikana kwa Magufuli mwaka 2015 kwa mujibu wa Polepole. Je huyu nae ni mtu hatari kwa taifa kwakuwa nahausika kutupangia marais kwa kuanzia kwa Mkapa kisha Magufuli?
Mfano wa Pili ni Hayati Mzee Mkapa, aliwania urais mwaka 1995 akashinda, kisha 2005 akahusika kupatika kwa rais Kikwete akiwa mwenyekiti wa chama, Ilipofika mwaka 2015, kwa mujibu wa Kabdendera katika kitabu chake, Rais Mkapa allitisha kikao cha siri na viongozi wa dini (akiwemo Mzee Pengo) na baadhi ya viongozi wastaafu na kutamka kuwa anapanga kumpendekeza au kumchagua JPM kama mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Hili hata Polepole amelisema pia ktk press conference kuwa JPM alipatikana kwa nguvu ya Mzee Mkapa. Je Mzee mkapa kwa hayo na yeye alikuwa mtu hatari kwa taifa? Hasa kwa kuzingatia jinsi utawala wa JPM ulivyo enda, je Na yeye wana mtandao wao ? au Hoja ni ipi hasa?
Twende na hilo la uteuzi wa Makmu wa rais, na kuwa Kikwete alipendeza SSH, kosa ni lipi hapo? Ktk uongozi mbona hayo ni mambo ya kawaida. Nakupa mfano, Kwa mujibu wa Mzee Kimitii, Rais Mkapa alitaka mteua yeye kama Waziri Mkuu lakini Mwl Nyerere akamkatalia kuwa asimpe Kimiti uwaziri Mkuu kwasababu ya kuwa na yeye ni mkatoliki. Je hayo hayafanani? Huoni pengine Kikwete aliona jicho la kisiasa kwa kutazama kuvutia kura za wanawake ktk uchaguzi ulikuwa unaonekana ni mgumu? Hoja ni ni hapo ktk mazingira ya uongozi na vika vya chama? Na kama SSH alikuwa tishio kwa JPM kwanini JPM hakumbadili ilipofika mwaka 2020? Maan alikuwa na nguvu zote za kufanya hayo!
Kuhusu kifo cha Rais JPM, mbona mambo ya afya za wagombewa ilikuwa mjdala toka 2015? CCM walianza mshambuli MZee LOwasa kuwa ana tatizo la afya na ikuli si wodi, wala hatutaki tupate msiba wa Rais sisi. Lowasa na wenzake including Mzee Sumaye wakajibu Kwani huyo JPM ni mzima? Unadhani walijibu bahati mbaya? hawakujua wanalo sema?
Siasa za fitna zitatukwamisha kama taifa
View: https://www.youtube.com/watch?v=O6Uena9vFMc&t=2128s