Laana ya mtandao na kuvurugika kwa chaguzi za chama: 1995-2025

Laana ya mtandao na kuvurugika kwa chaguzi za chama: 1995-2025

Ukimsikiliza ya polepole utajua namna na mambo yanavyoenda..

Sema hakika kila mwanzo huwa na mwisho wake na huenda mwaka huu kukawa na mabadiliko
 
Naam hakuna njia nyingine zaidi ya haya inabidi nchi wapewe chama pinzani ilikuwa hizo siasa za huyo master mind zilizopo ktk chama tawala

La sivyo kumuondoa master mind pekee na Head of state pekee haitoshi maana tayari Kuna wafuasi wao ambao wameshaiga falsafa zao na endapo wakiachwa wazitumie nchi itarudi kule kule ama zaidi ya kule

Ila Sasa swali la kujiuliza ninani wa KUMFUNGA PAKA KENGELE !!?
Huyu haina namna ila atokomezwe tu.
 
Umeongea ya kweli kabisa Malcom Lumumba

Ayatollah Kikwete ni replica ya Sani Abacha.

Kama Abacha alivyoivuruga Nigeria ndivyo Kikwete anavyoivuruga Tanzania. Na asipozuiwa kwa lazima nchi hii itaendelea kupambana na mabaki ya uzandiki wa Kikwete hata miaka 50 ijayo.

We are already a failed state sasa kama Nigeria. Ni suala la hatua kwa hatua tu kuelekea kujiona openly kama tumekuwa Failed State.
Kabisa , mzee ni mkosi kwa taifa, awajibishwe.
 
Kila siku nasema. Tungekuwa na TISS wenye akili nchi hii ingekuwa The Most developed country in Africa.

Kukosa kwao akili na kushindwa kuzuia hatari kwa wakati kunaligharimu na kutaligharimu hili Taifa milele.
Hao TISS wanatengenezwa na kufinyangwa wakiwa loyal kwa hilo lichama takataka unategemea watatenda uzalendo kweli?

TISS cabinet inatakiwa kuwa structured kuwa very independent. Yaani watu waliokunywa maji ya bendera na kulamba mchanga wa ardhi ya jamuhuri.

Waweke kiapo moyoni kuwa mtu yoyote atakae cheza na misingi ya jamuhuri anashughulikiwa haraka sana hata kama ni nani, kulinda heshima ya katiba na raia ndio priority.

Hao wavaa "Kaunda suti" sidhani kama wanatii kiapo cha uzalendo maana hadi sasa wangeshafanya maamuzi magumu.
 
Hata ikibidi kumwaga damu, yafanyike tu ila nchi na Watanzania wapone.
Ili wajukuu wasipatwe na hii laana maamuzi magumu ni muhimu. Taasisi zinazotakiwa kutenda majukumu yake zimekubali kuwekwa kwapani na kufanya uhovyo kinyume na utaratibu.
 

"Once is an accident. Twice is a coincidence. Thrice is a pattern"

Watanzania tumefika hapa kwasababu ni watu tunaopenda kupuuza mambo, kutokufikiria ipasavyo na kuendesha maisha yetu kimazoea. Binafsi huwa naamini kama tungekuwa hatupuuzi mambo kuna watu wasingediriki hata kuomba ridhaa ya kututawala. Hebu angalia huu mlolongo, halafu fikiria kama kuna bahati mbaya yoyote.

Mwaka 1995, uchaguzi wa mgombea Uraisi ndani ya CCM, huyu BWANA alikuwepo. Yeye na MTANDAO wake wakiwa vijana kabisa walifanya jaribio la kutaka wamsimike kuwa mgombea lakini wakazuiwa na kundi la wakubwa lililoongozwa na KAISARI. Kiukweli alishinda, lakini KAISARI alimdhibiti na kwasababu ni mjanja alikubali kushindwa.

Mwaka 2005, KAISARI hayupo. BWANA huyu na MTANDAO wake walifanya vurugu za kukipasua chama vipande-vipande. Walianza kujipanga kimya-kimya tokea mwaka 1995 hadi 2005, wakitumia mbinu chafu kama Rushwa, Mauaji, Ngono, Vitisho, Ahadi, Ushirikina na Propaganda. Watanzania walipuuza hii michezo ambayo ilifanywa na vibaraka wa MTANDAO walioko kwenye taasisi nyeti za dola, asasi za kiraia, taasisi za kidini na sekta binafsi.

Kipindi hiki BWANA huyu hakufanikiwa kuvuruga tu uchaguzi ndani ya chama, bali aina mbinu hizi alizihamishia hadi kwenye utawala wake ambao tulishuhudia nchi ikiendeshwa kama genge la YAKUZA. Siasa za chuki na makundi, rushwa iliyokithiri, uzembe kazini na siasa za kichawa zilianza na huyu BWANA. Watanzania kwasababu ni watu wakupuuza haya hatupendi kuyasikiliza au kuyajadili.

Mwaka 2015, BWANA huyu na MTANDAO wake waliamua kuvuruga kwa maksudi uchaguzi wa mgombea wa Uraisi. Hapa Afrika Mashariki, CHAMA ni moja ya taasisi kubwa zenye watu wenye akili na weledi. Wengi wao waliomba ridhaa kugombea Uraisi wa nchi, lakini MTANDAO ulioaanza 1995 ukawavuruga mchakato mzima. Mgombea aliyepatikana alikuwa ni wa SHINIKIZO LA WASTAAFU na BAHATI MBAYA.

Ila mbali na hayo BWANA huyu hakukubali kushindwa, akaamua kuvuruga mchakato wa MAKAMU. Watanzania na tatizo lao la kupuuza mambo, wakiwemo WASTAAFU hawakujiuliza kwanini BWANA yule amependekeza hivi kuhusu MAKAMU. Mgombea alikuwa wa BAHATI MBAYA/SHINIKIZO lakini MAKAMU alikuwa yupo KIMKAKATI.

Mwaka 2021, BWANA huyu alifanikiwa tena kuvuruga mchakato ndani ya CHAMA kwasababu mwaka 2015 alifanikiwa kupenyeza Farasi Wa Troa (Trojan Horse) kwenye nafasi ya UMAKAMU. Jambo hili watanzania wengi kwasababu ni watu wanaopenda kupuuza mambo, wakiwemo WASTAAFU hawakuona uzito wake kipindi hicho walikuja kustuka tu BWANA na MTANDAO wake wanajirudisha kwenye USUKANI kinyemela.

Mwaka 2025, BWANA huyu na MTANDAO karudia kufanya yaleyale aliyoyafanya kwenye chaguzi zote za mgombe Uraisi tokea 1995, 2005 na 2015. Jinsi utaratibu ulivyovunjwa mwaka 2015, ndivyo utamaduni umevunjwa 2025 yeye akiwa kinara. MTANDAO utafanya hivi tena 2030 na 2040. Bahati mbaya kipindi hiki watanzania washafahamu kwamba UMAKAMU kumbe ni mkubwa, uwepo wa BALOZI ambaye alikuwa mwana-MTANDAO huko nyuma, imeonekana ni CHANGAMOTO kwa BWANA.

==================================================================

KWENYE ULIMWENGU WA SIASA, SIYO BAHATI MBAYA mtu mmoja kuwepo na kuwa na ushawishi kwenye chaguzi za nafasi ya URAISI kwa kipindi cha miaka isiyopungua 30. Mnaweza mkamuita MWANAMKAKATI, BORN-TOWN, MASTER-MIND, KING-MAKER lakini, jambo ambalo BWANA huyu amefanikiwa kulifanya hata KAISARI kule kwenye kaburi anaona WIVU. Kuwa muhusika mkuu (MAIN PROTAGONIST) kwenye kila CHAGUZI ndani ya CHAMA kuanzia mwaka 1995, 2005, 2015 na 2025, ni jambo ambalo inabidi wanazuoni walifanyie TAFITI.

KINACHOSHANGAZA: Mwaka 2015, wakati BWANA na MTANDAO wamevuruga mchakato mzima wa UCHAGUZI ndani ya CHAMA. Aliyependekezwa UMAKAMU kipindi hiki alitoka nje kupinga mchakato mzima. Lakini mwaka 2025, yeye naye amerudia kufanya kilekile ambacho alikipinga kwa nguvu mwaka 2015.

Tena zaidi CHAMA kimegawanyika kwasababu aliyeratibu mchakato wa kutoa FOMU MOJA KWA MGOMBEA mwaka 2020, kaibuka kupinga uharamu uliofanyika kwenye mchakato wa kumpata mgombea Uraisi mwaka 2025. Yeye naye akipewa nafasi ya kugombea nafasi za juu kupitia njia haramu atanyamaza kama BALOZI mwenzake alivyofanya mwaka 2025.


==================================================================
Anachokifanya BWANA na MTANDAO wake kilifanikiwa tu kufanywa na Dikteta Sani Abacha kule Nigeria ambaye alifanikiwa kuvuruga michakato ya siasa Nigeria tokea mwaka 1966-1998, ambapo alikuwa nyuma ya uhaini (MAIN PROTAGONIST) ulioingiza au kutoa madarakani MARAISI 10 akiwemo na yeye.

CHAMA kumuweka BALOZI Uraisi kupitia UMAKAMU ni kijidanganya tu. CHAMA kilimuweka TINGATINGA lakini bado LAANA YA MTANDAO haikukiacha CHAMA, SERIKALI na NCHI. Mkishavunja utaratibu ndani ya CHAMA msidhani mtaweza kupambana na watu kama BWANA na MTANDAO.

Mpaka leo hii siasa za Nigeria zimekuwa ngumu kwasababu ya Sani Abacha na mtandao aliouacha. Hivyo hata kama BWANA ataondoka, madhara ambayo MTANDAO wake umeuacha kwa zaidi ya miaka 30 yataendelea kuiumiza NCHI, CHAMA na SERIKALI kwa miaka mingi mbele.

===============================================================
KIUFUPI TULIPOFIKA: Ili kuisadia nchi hapa ilipofika ni kufanya UWENDAWAZIMU (Doing the unthinkable). Hatuna utofauti na koloni la wakoma (A Leppers' Colony) ambapo huwezi kutofautisha baina ya mtu aliye MZIMA na MGONJWA. Katika mazingira kama haya, njia ni moja tu, kufunga madirisha ya nyumba na KUPULIZA SUMU, kisha kufunga mlango.

SUMU itaua WATOTO UNAOWAPENDA, itaua WATOTO WASIO NA KOSA, itaua WAGENI WALIOHAMIA, itaua DADA WA KAZI, itaua PANYA, itaua CHAWA, itaua WANYAMA na itaharibu CHAKULA na nyumba haitakalika kwa muda, lakini UGONJWA utakuwa umetoka na hautaweza kusambaa zaidi.

HAKUNA NJIA NYINGINE NJE YA HII.
​
Kwanini mnapenda kusema watanzania, tulipofika kwanini unajitoa. Usiseme wakapuuza sema tulipuuza. Habari za kujitoa sio nzuri kwa mwanaume.

Kuhusu mada upo sahihi, mfumo ukishaseti kuingia king ni kugusa tu.
 
Mkuu, Suluhisho la kweli ni kuimarisha utamaduni wa mchujo huru ndani ya chama kwa kuhakikisha kila mgombea anapita kwenye mchakato wa wazi na unaosimamiwa kwa uwazi.

Mfano tunaweza kujifunza kutoka Marekani ambapo primaries zinafanyika kwa uwazi mkubwa, zikihusisha wanachama wote na matokeo kutangazwa hadharani. Hii itasaidia kupunguza nguvu za mitandao ya kifisadi inayojipenyeza kimyakimya.

Njia nyingine ni kuunda kamati za uchunguzi wa wanachama watakaogombea nafasi za juu kwa kushirikisha wanachama wa kawaida na asasi za kiraia ili kujenga uhalali na kuzuia mtu mmoja au kikundi kidogo kulazimisha maamuzi. Ujerumani kupitia chama cha SPD kimefanikiwa kwa kutumia kura za maoni kwa wanachama wote kabla ya kumuidhinisha mgombea, jambo ambalo limeongeza uwazi na mshikamano wa ndani ya chama.

Teknolojia inaweza kutumika kuongeza uwazi na usalama wa kura. Estonia imepiga hatua kubwa kwa kutumia kura za mtandaoni zenye usalama wa blockchain, na mfumo kama huo unaweza kusaidia hata vyama vyetu kuhakikisha matokeo hayabadilishwi. Hii ikijumuishwa na elimu ya wanachama kuhusu haki zao na taratibu za uchaguzi ndani ya chama, kama ambavyo Afrika Kusini imekuwa ikifanya kupitia warsha na semina, inaweza kuondoa ujinga unaotumiwa na mitandao ya kifisadi.

Tunisia baada ya mapinduzi ya 2011 ilibadilisha katiba ya vyama na kuanzisha vikao vya wazi kwa wanachama wote, hali iliyosaidia kuongeza mshikamano na kupunguza nguvu za makundi ya kifisadi. Hatua kama hizi zinaweza kuondoa kabisa nguvu za “mtandao” na kujenga demokrasia ya kweli inayotegemea ushiriki wa wanachama wote.

Nimetoa tu suggestions japokuwa mimi sio mwanachama wala muumini wa hicho chama
Umeandika hoja nzito sana na za maana kupita maelezo.
 
SIASA ZA MTANDAO ZILIVYOUA JAMHURI YA RUMI YA KALE.

Dola la Rumi kabla ya kuwa Ufalme mkubwa duniani 44 BC, ilikuwa ni Jamhuri inayoongozwa kidemokrasia chini ya Seneti. Kabla ya hapo Rumi ilikuwa nchi ya kifalme, ambayo wafalme waliongoza kama MIUNGU WATU (Divine Right). Mwaka 509 BC, Warumi baada ya kuongozwa na Mfalme Dikteta Jehuri, Tarquinius Superbus, walijikusanya wakampindua na kumfukuza.

Warumi walitengeneza Jamhuri ya Kwanza (First Republic) duniani ambayo iliongozwa na kiongozi wa kuteuliwa (Consul), ambaye alikaa muda fulani kisha kuondoka. Utaratibu huu uliendelee kwa zaidi ya miaka 300 na Rumi ikafanikiwa mno. Ndani ya Seneti kulikuwa na makundi mawili, Optimates na Populares, ambayo ndiyo yalitoa wabunge wa majimbo.

Rumi lilikuwa ni taifa kubwa lililofanikiwa kwasababu, waliweza kuanzisha mfumo wa MERITOCRACY. Ambapo mtu aliyezaliwa tabaka la chini angeweza kufika tabaka la kutawala kama alikuwa na kipaji cha kijeshi, dini, sanaa au kuasiriwa (Adopted) na mtu wa tabaka la juu. Mfumo huu, uliweza kufanya warumi kuwa taifa lenye watu wenye uwezo mkubwa kiongozi.

MWANZO WA MATATIZO: Mwaka 60 BC, baada ya Jamhuri ya Rumi kufanikiwa kwa miaka mingi, kuna vijana watatu (Julius Ceaser, Gnaius Pompey na Marcus Crassus) walichipukia kwa nguvu kwenye siasa za nchi. Vijana hawa walikuwa hawana nguvu ya kushindana na wanasiasa wakongwe ndani ya Seneti ya Rumi ambao wengi walikuwa ni wanafalsafa nguli kama Cicero.

Hawa vijana wakaanzisha siasa za fitna na kuunda umoja wao uliotwa The First Roman Triumvirate, ambapo walikubaliana kuunganisha nguvu zao ili kuwala Rumi kihuni. Mtandao wa wao, The Triumvirate ulikuwa na nguvu kubwa kwasababu, Julius Ceaser alikuwa ni KUHANI MKUU WA RUMI (Pontifex Maximus), Gnaius Pompey alikuwa JENERALI ALIYESHINDA VITA (Roman Imperator), na Marcus Crassus akiwa TAJIRI MKUBWA (Richest Man In Rome).

Huu MTANDAO ulikuwa na nguvu kubwa mno na kuanza kuvuruga siasa za Rumi, kwa kutumia rushwa, ngono, utekaji, siasa za kuchafuana na uchawa kutishia watu. Hawa vijana watatu waliratibu makundi ya wahuni waliofanya fujo, kisha wao kuja kusawazisha na kuonekana wao ndiyo suluhu. Walifanikiwa kushika nchi, na Pompey akawa kiongozi mkuu (Consul).

Tatizo likatokea pale hawa vijana waliposhindwa kushirikishana madaraka (Power Sharing). Pompey alikuwa Consul na uwezo wake kijeshi ulikuwa mkubwa mno kuliko Ceaser na Crassus. Ceaser akaamua kuingiza nchi kwenye vita ili avunje rekodi ya Pompey pamoja na kulipa madeni ya watu aliyokopa wakati wa siasa chafu za Triumvirate.

Baada ya kuvunja sheria za nchi Ceaser alichukua vikosi vya kijeshi kinyume na Seneti na kuvamia BRITTANICA (Uingereza) ili tu kujenga jina kubwa kuliko Pompey. Alifanikiwa kuvamia GAUL (Ufaransa/Spain) na BRITTANICA na kupewa cheo cha JENERALI ALIYESHINDA VITA (Roman Imperator).

Crassus naye hakuwa nyuma, akachukua wanajeshi wasiopungua 40,000 akaenda kuvamia dola la Uajemi la Kiparthi (Parthian Empire) ili kufikia mafanikio ya kijeshi ya Ceaser na Pompey. Alitumia fedha zake binafsi kuendesha hii vita, lakini iliishia vibaya mno baada ya Warumi zaidi ya 40,000 kuuwawa kinyama, huku yeye pia akimwagiwa dhahabu iliyoyeyuka (Molten Gold) kichwani.

==========================================
Wakabaki Ceaser na Pompey, siasa zao zikaigawa Rumi.

Hapo zamani ili kuzuia uhaini, Seneti ya Rumi iliweka utaratibu kwamba kuna mipaka ndani ya nchi ambayo wanajeshi hawataki kuvuka na vikosi vyao na kuingia navyo Rumi. Ceaser baada ya kuona Pompey kama kiongozi wa nchi ameishawishi Seneti imuadhibu kwa kuanzisha vita, akaavusha vikosi vyake kwenye mpaka uitwao,The Rubbicon.

Rumi iligubikwa na Civil War kubwa kisa MTANDAO wa watu watatu, The Triumvirate ambao ulifundisha watu tabia za kutotii katiba na sheria, pamoja na kutumia mbinu yoyote ile kupata madaraka. Miaka 4, walipigana maelfu ya watu wakafa, na mwishowe Ceaser akaibuka mshindi.

MADHARA YA SIASA ZA MTANDAO: Ceaser alipoibuka mshindi alijigeuza Dikteta (Benevolent Dictator), jambo ambalo liliwakera Warumi wengi hasa wabunge wa majimbo. Chawa wake kama Mark Anthony wakaanza kupendekeza Ceaser awe mfalme kabisa, wakijifanya wanatania. Wabunge kama Cicero walikereka mno na hichi kitendo kwasababu kilivunja misingi ambayo ilidumu kwa miaka zaidi ya 300. Wazee na Wahenga wao, walilipia gharama kubwa kufukuza wafalme na kuanzisha Jamhuri, iweje Ceaser atake kujigeuza Mfalme ?

NJAMA YA KUIOKOA RUMI: Wabunge wa Rumi, wakiwemo marafiki wa karibu na Ceaser kama Brutus, waliamua kuiweka Jamhuri mbele kuliko uswahiba. Wakapanga njama ya kumuua Ceaser. Mwaka mmoja kabla, zilianza kutolewa nabii kutoka kwa waaaguzi mbalimbali waliomwambia Ceaser kwamba atakufa mwezi Machi (Beware of the Odes of March), lakini aliwapuuza.

Mwezi Machi ukafika baada ya mwaka kupita, Ceaser akamfuata yule mwanamke muaguzi na kumcheka huku akikashifu kwamba nimefika Machi na sijafa. Ceaser alikuwa ni BRILLIANT STRATEGIST, and AN EXCELLENT STATESMAN. Alikuwa anakubalika sana na makundi ya watu ndani ya nchi kwasababu alijionesha yeye ni mtu poa anayetaka kila mtu apate. Sifa yake kubwa ilikuwa ni kupenda kulala na wanawake wengi, wakampa jina The Bald Fornicator.

Siku hiyo, Ceaser anamkashifu Mwaguzi, huku akielekea bungeni ndiyo ulikuwa mwisho wake. Alivyoingia bungeni, wabunge wakatoa visu na kuanza kumchoma na kumuua. Alishangaa kumuona rafiki yake Brutus, ambaye aliamua kuiweka Jamhuri mbele. Ceaser akafa na huo ndiyo ukawa mwisho wake.

MATATIZO YA MTANDAO YANAENDELEA: Wabunge kwa kumuua Ceaser, walidhani wangemaliza matatizo kumbe madhara ya siasa za MTANDAO, The Triumvirate yalikuwa makubwa mno. Wanajeshi walifundishwa kupuuza wabunge na kutumia nguvu kupata chochote. Wafuasi wa Ceaser wakiongozwa na Mark Anthony wakaanza kampeni za kijeshi za kulipiza kisasi, ambazo zilisababisha Civil War nyingine ambayo iliwaua kina Brutus na Cicero.

Hata baada ya wapinzani wa Ceaser kuuawa, Rumi haikupona. Machawa wa Ceaser wenyewe nao wakageukana kila mtu akitaka kutawala Rumi. Mpwa wa Ceaser, Octavian, ambaye alikuja kuwa Kaisari wa kwanza wa Rumi (Roman Ceaser Augustus) alipambana na Mark Anthony na kumshinda.

Octavian baada ya kushinda vita, akaitisha Seneti na kuwaambia wachague wampe uongozi wa kudumu wa Rumi (Consul for Life) ambapo walikubali kwa woga. Mwishowe akajigeuza kuwa Mfalme (Emperor) na Jamhuri ya Rumi ikafa, likazaliwa dola la Rumi (Roman Empire). Kitu ambacho Warumi walikuwa wanakiogopa kwa miaka za ya 300, kikawatokea kisa siasa za MTANDAO wa watu watatu tu.

==============================================
Kuna mengi ya kujifunza hapa. Hakuna MKUBWA KULIKO NCHI, na hapa tulipofika hatuwezi kukwepa maswaibu ya MTANDAO uliojijenga nchini kwa miaka zaidi ya miongo mitatu.




Sic Semper Tyrannis ​
Hii ni in-depth knowledge na hii ndio JF threading inatakiwa kuwa. Shukurani kwa hili andiko la maana kabisa.
 
Kule Ukraine kuna sniper anavunja rekodi zake, nilisoma juzi aliweza kupiga targert kwa umbali wa 2.5 miles away.

Mnaonaje atafutwe atoe nafunzo kwa watanganyika ili tuache kuwa tunalalamika bila kuwa na solution ya tunacholalamikia.
 
Tiss walitakiwa watengeze vyama viwilli vyenye Nguvu vinavyopokezana Madaraka ingesandia sana
Hilo sio jukumu la TISS ,wao kazi yao ni kusimamia usalama wa taifa sio kupanga usalama ukae namna gani. Misingi ipo na inajulikana. Mtu anayetumia mamlaka vibaya anatakiwa kufuatiliwa na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Hivi mnahisi hao TISS ni malaika au wanafanya kazi zao kwa mujibu wa wanavyojiskia.
 
Heko kwa bandiko lako ndugu MALCOM LUMUMBA
Inawezekana huyu KING-MAKER sio hatari hivyo kama tunavyotaka kuaminishwa maana kuna vitu vilitokea hapo katikati hadi vikatoa picha ya kwamba yeye sio MASTERMIND wa mchezo mzima bali kuna wanufaika wengine kuliko yeye.
Mchakato wa mabadiliko ya katiba uliruhusiwa katika hatua za mwisho za utawala wa huyu Bwana na ilikuwa imebaki kidogo sana hiki kitabu kipitishwe na kuwa rasmi kabla ya kutupiliwa mbali dakika za lala salama. Wote tunajua ni kwa namna gani katiba ya Warioba ingeenda kuwa mwiba mchungu kwa wanamtandao na inawezekana ndio walishinikiza kipotezewe. Kama kweli huyu Born town angekuwa ana plan mbele ya muda, hili alitakiwa awe amelijua mapema na mchakato wa mabadiliko ya katiba wala usingepewa promo kwa namna yoyote ile ili kulinda maslahi yao sasa na mbeleni.

Kwa mtizamo wangu mimi, huyu jamaa anaweza kuwa ni vessel tu ya masterminds wengine wanaocheza hii game nyuma ya pazia na yeye anatumikishwa tu kufikia malengo. Kinachomponza ni kule kunufaika na yale mabaki yeye na familia yake.
ni kweli , yani ukicheki siku ile samia kampasia kijiti atie neno unaona kabisa mwamba alikuwa out of the loop kabisa akaona any way isiwe shida alisita sana ila saizi kila mtu anambebesha lawama zote.
 
Hao TISS wanatengenezwa na kufinyangwa wakiwa loyal kwa hilo lichama takataka unategemea watatenda uzalendo kweli?

TISS cabinet inatakiwa kuwa structured kuwa very independent. Yaani watu waliokunywa maji ya bendera na kulamba mchanga wa ardhi ya jamuhuri.

Waweke kiapo moyoni kuwa mtu yoyote atakae cheza na misingi ya jamuhuri anashughulikiwa haraka sana hata kama ni nani, kulinda heshima ya katiba na raia ndio priority.

Hao wavaa "Kaunda suti" sidhani kama wanatii kiapo cha uzalendo maana hadi sasa wangeshafanya maamuzi magumu.
wawe kama CAG ila wapewe meno kwa ajili ya Taifa
 
Napenda kusoma maandiko ya watu ambao si wazushi kama hii makala.

Nakumbuka 2015 alianza kwa kueleza kuwa mwaka huu mgombea mwenza lazima awe ni mwanamke. Watu wakapiga makofi. Baadaye wakasema yupo Amina; jamaa akamkataa kwa kigezo kuwa Amina aligombea Urais na ni hatari kwa mtu anayetaka cheo kuwa msaidizi. Akadakia si saa ngapi 100 yupo! Watu pwapwapwa. Ilikuwa rahisi kwake
Dah..aise...jpm kwanini hakukataa? Kwa hulka ya jpm why hakukataa ama kama alikua anajua huu mtandao na kinara wake kwanini hakushtuka kuhusu pandikizi Hilo la makamu kwa wakati ule
 
Sitaki kuamini unachokisema maana hakina ushahidi, kinabaki kuwa ni maoni yako binafsi.

Lakini kama mtu wa namna hiyo yupo basi tumpe Nchi maana inaonekana anaiweza vizuri. Ikiwa mtu huyo anaweza ku control angle zote kama unavyotaka kutuaminisha Why Asiwe kama Trump tukamchagua tena.

Mimi nawaza postively kwamba huyo mtu anatufaa sana. He is powerful, Able and Briliant.

Yangu ni hayo tu.
Hizo characteristics tatu ulizotaja ...zimeisaidia nini Tanzania Hadi wakati huu? Countrywise Economically + personal income ya kila mtanzania Iko vipi
 
Dah..aise...jpm kwanini hakukataa? Kwa hulka ya jpm why hakukataa ama kama alikua anajua huu mtandao na kinara wake kwanini hakushtuka kuhusu pandikizi Hilo la makamu kwa wakati ule
Wewe, angekataa asingefika mbali kwa vile yeye ni mgombea wa chama kumbuka, si mgombea binafsi. Ndo maana tunahangaika mageuzi ya mgombea binafsi ingawa vyama vyote hada Chadema hawataki kulisikia hilo.
 
​
"Once is an accident. Twice is a coincidence. Thrice is a pattern"
​
Watanzania tumefika hapa kwasababu ni watu tunaopenda kupuuza mambo, kutokufikiria ipasavyo na kuendesha maisha yetu kimazoea. Binafsi huwa naamini kama tungekuwa hatupuuzi mambo kuna watu wasingediriki hata kuomba ridhaa ya kututawala. Hebu angalia huu mlolongo, halafu fikiria kama kuna bahati mbaya yoyote.

Mwaka 1995, uchaguzi wa mgombea Uraisi ndani ya CCM, huyu BWANA alikuwepo. Yeye na MTANDAO wake wakiwa vijana kabisa walifanya jaribio la kutaka wamsimike kuwa mgombea lakini wakazuiwa na kundi la wakubwa lililoongozwa na KAISARI. Kiukweli alishinda, lakini KAISARI alimdhibiti na kwasababu ni mjanja alikubali kushindwa.

Mwaka 2005, KAISARI hayupo. BWANA huyu na MTANDAO wake walifanya vurugu za kukipasua chama vipande-vipande. Walianza kujipanga kimya-kimya tokea mwaka 1995 hadi 2005, wakitumia mbinu chafu kama Rushwa, Mauaji, Ngono, Vitisho, Ahadi, Ushirikina na Propaganda. Watanzania walipuuza hii michezo ambayo ilifanywa na vibaraka wa MTANDAO walioko kwenye taasisi nyeti za dola, asasi za kiraia, taasisi za kidini na sekta binafsi.

Kipindi hiki BWANA huyu hakufanikiwa kuvuruga tu uchaguzi ndani ya chama, bali aina mbinu hizi alizihamishia hadi kwenye utawala wake ambao tulishuhudia nchi ikiendeshwa kama genge la YAKUZA. Siasa za chuki na makundi, rushwa iliyokithiri, uzembe kazini na siasa za kichawa zilianza na huyu BWANA. Watanzania kwasababu ni watu wakupuuza haya hatupendi kuyasikiliza au kuyajadili.

Mwaka 2015, BWANA huyu na MTANDAO wake waliamua kuvuruga kwa maksudi uchaguzi wa mgombea wa Uraisi. Hapa Afrika Mashariki, CHAMA ni moja ya taasisi kubwa zenye watu wenye akili na weledi. Wengi wao waliomba ridhaa kugombea Uraisi wa nchi, lakini MTANDAO ulioaanza 1995 ukawavuruga mchakato mzima. Mgombea aliyepatikana alikuwa ni wa SHINIKIZO LA WASTAAFU na BAHATI MBAYA.

Ila mbali na hayo BWANA huyu hakukubali kushindwa, akaamua kuvuruga mchakato wa MAKAMU. Watanzania na tatizo lao la kupuuza mambo, wakiwemo WASTAAFU hawakujiuliza kwanini BWANA yule amependekeza hivi kuhusu MAKAMU. Mgombea alikuwa wa BAHATI MBAYA/SHINIKIZO lakini MAKAMU alikuwa yupo KIMKAKATI.

Mwaka 2021, BWANA huyu alifanikiwa tena kuvuruga mchakato ndani ya CHAMA kwasababu mwaka 2015 alifanikiwa kupenyeza Farasi Wa Troa (Trojan Horse) kwenye nafasi ya UMAKAMU. Jambo hili watanzania wengi kwasababu ni watu wanaopenda kupuuza mambo, wakiwemo WASTAAFU hawakuona uzito wake kipindi hicho walikuja kustuka tu BWANA na MTANDAO wake wanajirudisha kwenye USUKANI kinyemela.

Mwaka 2025, BWANA huyu na MTANDAO karudia kufanya yaleyale aliyoyafanya kwenye chaguzi zote za mgombe Uraisi tokea 1995, 2005 na 2015. Jinsi utaratibu ulivyovunjwa mwaka 2015, ndivyo utamaduni umevunjwa 2025 yeye akiwa kinara. MTANDAO utafanya hivi tena 2030 na 2040. Bahati mbaya kipindi hiki watanzania washafahamu kwamba UMAKAMU kumbe ni mkubwa, uwepo wa BALOZI ambaye alikuwa mwana-MTANDAO huko nyuma, imeonekana ni CHANGAMOTO kwa BWANA.

=======================

KWENYE ULIMWENGU WA SIASA, SIYO BAHATI MBAYA mtu mmoja kuwepo na kuwa na ushawishi kwenye chaguzi za nafasi ya URAISI kwa kipindi cha miaka isiyopungua 30. Mnaweza mkamuita MWANAMKAKATI, BORN-TOWN, MASTER-MIND, KING-MAKER lakini, jambo ambalo BWANA huyu amefanikiwa kulifanya hata KAISARI kule kwenye kaburi anaona WIVU. Kuwa muhusika mkuu (MAIN PROTAGONIST) kwenye kila CHAGUZI ndani ya CHAMA kuanzia mwaka 1995, 2005, 2015 na 2025, ni jambo ambalo inabidi wanazuoni walifanyie TAFITI.

KINACHOSHANGAZA: Mwaka 2015, wakati BWANA na MTANDAO wamevuruga mchakato mzima wa UCHAGUZI ndani ya CHAMA. Aliyependekezwa UMAKAMU kipindi hiki alitoka nje kupinga mchakato mzima. Lakini mwaka 2025, yeye naye amerudia kufanya kilekile ambacho alikipinga kwa nguvu mwaka 2015.

Tena zaidi CHAMA kimegawanyika kwasababu aliyeratibu mchakato wa kutoa FOMU MOJA KWA MGOMBEA mwaka 2020, kaibuka kupinga uharamu uliofanyika kwenye mchakato wa kumpata mgombea Uraisi mwaka 2025. Yeye naye akipewa nafasi ya kugombea nafasi za juu kupitia njia haramu atanyamaza kama BALOZI mwenzake alivyofanya mwaka 2025.

=========================

Anachokifanya BWANA na MTANDAO wake kilifanikiwa tu kufanywa na Dikteta Sani Abacha kule Nigeria ambaye alifanikiwa kuvuruga michakato ya siasa Nigeria tokea mwaka 1966-1998, ambapo alikuwa nyuma ya uhaini (MAIN PROTAGONIST) ulioingiza au kutoa madarakani MARAISI 10 akiwemo na yeye.

CHAMA kumuweka BALOZI Uraisi kupitia UMAKAMU ni kijidanganya tu. CHAMA kilimuweka TINGATINGA lakini bado LAANA YA MTANDAO haikukiacha CHAMA, SERIKALI na NCHI. Mkishavunja utaratibu ndani ya CHAMA msidhani mtaweza kupambana na watu kama BWANA na MTANDAO.

Mpaka leo hii siasa za Nigeria zimekuwa ngumu kwasababu ya Sani Abacha na mtandao aliouacha. Hivyo hata kama BWANA ataondoka, madhara ambayo MTANDAO wake umeuacha kwa zaidi ya miaka 30 yataendelea kuiumiza NCHI, CHAMA na SERIKALI kwa miaka mingi mbele.

===========================

KIUFUPI TULIPOFIKA: Ili kuisadia nchi hapa ilipofika ni kufanya UWENDAWAZIMU (Doing the unthinkable). Hatuna utofauti na koloni la wakoma (A Leppers' Colony) ambapo huwezi kutofautisha baina ya mtu aliye MZIMA na MGONJWA. Katika mazingira kama haya, njia ni moja tu, kufunga madirisha ya nyumba na KUPULIZA SUMU, kisha kufunga mlango.

SUMU itaua WATOTO UNAOWAPENDA, itaua WATOTO WASIO NA KOSA, itaua WAGENI WALIOHAMIA, itaua DADA WA KAZI, itaua PANYA, itaua CHAWA, itaua WANYAMA na itaharibu CHAKULA na nyumba haitakalika kwa muda, lakini UGONJWA utakuwa umetoka na hautaweza kusambaa zaidi.

HAKUNA NJIA NYINGINE NJE YA HII.
Ukute wewe ndo Polepole 💞💕
 
Back
Top Bottom