Laana ya mtandao na kuvurugika kwa chaguzi za chama: 1995-2025

SIASA ZA MTANDAO ZILIVYOUA JAMHURI YA RUMI YA KALE.

Dola la Rumi kabla ya kuwa Ufalme mkubwa duniani 44 BC, ilikuwa ni Jamhuri inayoongozwa kidemokrasia chini ya Seneti. Kabla ya hapo Rumi ilikuwa nchi ya kifalme, ambayo wafalme waliongoza kama MIUNGU WATU (Divine Right). Mwaka 509 BC, Warumi baada ya kuongozwa na Mfalme Dikteta Jehuri, Tarquinius Superbus, walijikusanya wakampindua na kumfukuza.

Warumi walitengeneza Jamhuri ya Kwanza (First Republic) duniani ambayo iliongozwa na kiongozi wa kuteuliwa (Consul), ambaye alikaa muda fulani kisha kuondoka. Utaratibu huu uliendelee kwa zaidi ya miaka 300 na Rumi ikafanikiwa mno. Ndani ya Seneti kulikuwa na makundi mawili, Optimates na Populares, ambayo ndiyo yalitoa wabunge wa majimbo.

Rumi lilikuwa ni taifa kubwa lililofanikiwa kwasababu, waliweza kuanzisha mfumo wa MERITOCRACY. Ambapo mtu aliyezaliwa tabaka la chini angeweza kufika tabaka la kutawala kama alikuwa na kipaji cha kijeshi, dini, sanaa au kuasiriwa (Adopted) na mtu wa tabaka la juu. Mfumo huu, uliweza kufanya warumi kuwa taifa lenye watu wenye uwezo mkubwa kiongozi.

MWANZO WA MATATIZO: Mwaka 60 BC, baada ya Jamhuri ya Rumi kufanikiwa kwa miaka mingi, kuna vijana watatu (Julius Ceaser, Gnaius Pompey na Marcus Crassus) walichipukia kwa nguvu kwenye siasa za nchi. Vijana hawa walikuwa hawana nguvu ya kushindana na wanasiasa wakongwe ndani ya Seneti ya Rumi ambao wengi walikuwa ni wanafalsafa nguli kama Cicero.

Hawa vijana wakaanzisha siasa za fitna na kuunda umoja wao uliotwa The First Roman Triumvirate, ambapo walikubaliana kuunganisha nguvu zao ili kuwala Rumi kihuni. Mtandao wa wao, The Triumvirate ulikuwa na nguvu kubwa kwasababu, Julius Ceaser alikuwa ni KUHANI MKUU WA RUMI (Pontifex Maximus), Gnaius Pompey alikuwa JENERALI ALIYESHINDA VITA (Roman Imperator), na Marcus Crassus akiwa TAJIRI MKUBWA (Richest Man In Rome).

Huu MTANDAO ulikuwa na nguvu kubwa mno na kuanza kuvuruga siasa za Rumi, kwa kutumia rushwa, ngono, utekaji, siasa za kuchafuana na uchawa kutishia watu. Hawa vijana watatu waliratibu makundi ya wahuni waliofanya fujo, kisha wao kuja kusawazisha na kuonekana wao ndiyo suluhu. Walifanikiwa kushika nchi, na Pompey akawa kiongozi mkuu (Consul).

Tatizo likatokea pale hawa vijana waliposhindwa kushirikishana madaraka (Power Sharing). Pompey alikuwa Consul na uwezo wake kijeshi ulikuwa mkubwa mno kuliko Ceaser na Crassus. Ceaser akaamua kuingiza nchi kwenye vita ili avunje rekodi ya Pompey pamoja na kulipa madeni ya watu aliyokopa wakati wa siasa chafu za Triumvirate.

Baada ya kuvunja sheria za nchi Ceaser alichukua vikosi vya kijeshi kinyume na Seneti na kuvamia BRITTANICA (Uingereza) ili tu kujenga jina kubwa kuliko Pompey. Alifanikiwa kuvamia GAUL (Ufaransa/Spain) na BRITTANICA na kupewa cheo cha JENERALI ALIYESHINDA VITA (Roman Imperator).

Crassus naye hakuwa nyuma, akachukua wanajeshi wasiopungua 40,000 akaenda kuvamia dola la Uajemi la Kiparthi (Parthian Empire) ili kufikia mafanikio ya kijeshi ya Ceaser na Pompey. Alitumia fedha zake binafsi kuendesha hii vita, lakini iliishia vibaya mno baada ya Warumi zaidi ya 40,000 kuuwawa kinyama, huku yeye pia akimwagiwa dhahabu iliyoyeyuka (Molten Gold) kichwani.

==========================================
Wakabaki Ceaser na Pompey, siasa zao zikaigawa Rumi.

Hapo zamani ili kuzuia uhaini, Seneti ya Rumi iliweka utaratibu kwamba kuna mipaka ndani ya nchi ambayo wanajeshi hawataki kuvuka na vikosi vyao na kuingia navyo Rumi. Ceaser baada ya kuona Pompey kama kiongozi wa nchi ameishawishi Seneti imuadhibu kwa kuanzisha vita, akaavusha vikosi vyake kwenye mpaka uitwao,The Rubbicon.

Rumi iligubikwa na Civil War kubwa kisa MTANDAO wa watu watatu, The Triumvirate ambao ulifundisha watu tabia za kutotii katiba na sheria, pamoja na kutumia mbinu yoyote ile kupata madaraka. Miaka 4, walipigana maelfu ya watu wakafa, na mwishowe Ceaser akaibuka mshindi.

MADHARA YA SIASA ZA MTANDAO: Ceaser alipoibuka mshindi alijigeuza Dikteta (Benevolent Dictator), jambo ambalo liliwakera Warumi wengi hasa wabunge wa majimbo. Chawa wake kama Mark Anthony wakaanza kupendekeza Ceaser awe mfalme kabisa, wakijifanya wanatania. Wabunge kama Cicero walikereka mno na hichi kitendo kwasababu kilivunja misingi ambayo ilidumu kwa miaka zaidi ya 300. Wazee na Wahenga wao, walilipia gharama kubwa kufukuza wafalme na kuanzisha Jamhuri, iweje Ceaser atake kujigeuza Mfalme ?

NJAMA YA KUIOKOA RUMI: Wabunge wa Rumi, wakiwemo marafiki wa karibu na Ceaser kama Brutus, waliamua kuiweka Jamhuri mbele kuliko uswahiba. Wakapanga njama ya kumuua Ceaser. Mwaka mmoja kabla, zilianza kutolewa nabii kutoka kwa waaaguzi mbalimbali waliomwambia Ceaser kwamba atakufa mwezi Machi (Beware of the Odes of March), lakini aliwapuuza.

Mwezi Machi ukafika baada ya mwaka kupita, Ceaser akamfuata yule mwanamke muaguzi na kumcheka huku akikashifu kwamba nimefika Machi na sijafa. Ceaser alikuwa ni BRILLIANT STRATEGIST, and AN EXCELLENT STATESMAN. Alikuwa anakubalika sana na makundi ya watu ndani ya nchi kwasababu alijionesha yeye ni mtu poa anayetaka kila mtu apate. Sifa yake kubwa ilikuwa ni kupenda kulala na wanawake wengi, wakampa jina The Bald Fornicator.

Siku hiyo, Ceaser anamkashifu Mwaguzi, huku akielekea bungeni ndiyo ulikuwa mwisho wake. Alivyoingia bungeni, wabunge wakatoa visu na kuanza kumchoma na kumuua. Alishangaa kumuona rafiki yake Brutus, ambaye aliamua kuiweka Jamhuri mbele. Ceaser akafa na huo ndiyo ukawa mwisho wake.

MATATIZO YA MTANDAO YANAENDELEA: Wabunge kwa kumuua Ceaser, walidhani wangemaliza matatizo kumbe madhara ya siasa za MTANDAO, The Triumvirate yalikuwa makubwa mno. Wanajeshi walifundishwa kupuuza wabunge na kutumia nguvu kupata chochote. Wafuasi wa Ceaser wakiongozwa na Mark Anthony wakaanza kampeni za kijeshi za kulipiza kisasi, ambazo zilisababisha Civil War nyingine ambayo iliwaua kina Brutus na Cicero.

Hata baada ya wapinzani wa Ceaser kuuawa, Rumi haikupona. Machawa wa Ceaser wenyewe nao wakageukana kila mtu akitaka kutawala Rumi. Mpwa wa Ceaser, Octavian, ambaye alikuja kuwa Kaisari wa kwanza wa Rumi (Roman Ceaser Augustus) alipambana na Mark Anthony na kumshinda.

Octavian baada ya kushinda vita, akaitisha Seneti na kuwaambia wachague wampe uongozi wa kudumu wa Rumi (Consul for Life) ambapo walikubali kwa woga. Mwishowe akajigeuza kuwa Mfalme (Emperor) na Jamhuri ya Rumi ikafa, likazaliwa dola la Rumi (Roman Empire). Kitu ambacho Warumi walikuwa wanakiogopa kwa miaka za ya 300, kikawatokea kisa siasa za MTANDAO wa watu watatu tu.

==============================================
Kuna mengi ya kujifunza hapa. Hakuna MKUBWA KULIKO NCHI, na hapa tulipofika hatuwezi kukwepa maswaibu ya MTANDAO uliojijenga nchini kwa miaka zaidi ya miongo mitatu.




Sic Semper Tyrannis ​
 
Mko nchi gani mbona hamridhiki na matunda ya ardhi yenu.

Mimi siwezi kuipinga nchi yangu nakula, nakunywa, napata hela, naona fursa, naoa, nazalisha, napenda, napenda, nafanya miamala, nalala. sijaona kosa la mfumo nimeridhika na maisha hayahaya
Aisee!!
 
Napenda kusoma maandiko ya watu ambao si wazushi kama hii makala.

Nakumbuka 2015 alianza kwa kueleza kuwa mwaka huu mgombea mwenza lazima awe ni mwanamke. Watu wakapiga makofi. Baadaye wakasema yupo Amina; jamaa akamkataa kwa kigezo kuwa Amina aligombea Urais na ni hatari kwa mtu anayetaka cheo kuwa msaidizi. Akadakia si saa ngapi 100 yupo! Watu pwapwapwa. Ilikuwa rahisi kwake
 
The State ilitakiwa watengeze chama Chao viwe vyama viwilli vyenye Nguvu au waungane na Mlugaluga watakua wamechomoa waya
 
Mko nchi gani mbona hamridhiki na matunda ya ardhi yenu.

Mimi siwezi kuipinga nchi yangu nakula, nakunywa, napata hela, naona fursa, naoa, nazalisha, napenda, napenda, nafanya miamala, nalala. sijaona kosa la mfumo nimeridhika na maisha hayahaya
Wewe ni iron boy. Mambo ya golden boys yapo juu ya uwezo wako.
 
Kikwete ikishindikana kudhibitiwa mwaka huu, narudia mwaka huu, Hii nchi inazama mazima na haitakaa iinuke tena!!

Kosa nikuona JK ndio shida, ,shida sio JK jamani shida ni kikundi cha watu waliojaa Kila mahala na kuendesha mtandao wa kihalifu aka State capture, utekaji huu haujafanywa na mtu mmoja bali ni kikundi cha watu wengi ambao ni kama serikali ya kificho yenye Kila kitu kuanzia RAIS nk

Haka kakikundi kametengenezwa kuishi milele, na kuna succession plan ipo juu ya hii nchi kupitia hao wahuni.

ndani ya mitaa ya Damascus-Syria.
 
Hizo porojo tu na ingekuwa vizuri uandikie riwaya km kuna la kujifunza kweli ndani yake. Kugombea uongozi ni haki yake na kukubalika kwa wajumbe na wananchi ni haki yake, usiilalie mlango wazi bahati ya mwenzako, siasa ni ushawishi, ni mvuto, mzee wa watu alikuwa na mvuto km Barrack Obama sasa unataka kushindana na maumbile ya mwenyenzi Mungu?

Hata kesho we huwezi kusimama na JK mbele za watu ukashinda kwa jambo lolote, ana ushawisi. Ht km siue yeye Magu asingekaribia urais wa JMT. Hata hivyo Kikwete alifanya mambo makubwa sana hasa ktk kujenga miundo mbinu mwenye macho haambiwi tazama.
 
Wewe unaongelea ishu za chama wakati mjadala unahusu nchi na taifa...

Tunataka mfumo mpya na imara wa kikatiba ambao utavifunga mpaka vyama vya siasa kutoa watu wema na waadilifu kushika dhamana ya kuongoza nchi...

Tunatakiwa kufanya kama huyu mdau gefa alivyosema hapaπŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

...Reset Mode, na New installation ndio option....!
 
Hicho chama ndicho kimetoa viongozi wa taifa na kutufikisha hapa tulipo
 
Kivunjwe chama Cha CCM, viundwe vyama vitatu tuu kweny nchi ambavyo vitakuwa na ushirki wa siasa, sio vyma vingi kiasi hiki
 
Na mbowe wa Retired nina amini ni sehemu ya mfumo wa watoto wa mjini
 
Sitaki kuamini unachokisema maana hakina ushahidi, kinabaki kuwa ni maoni yako binafsi.

Lakini kama mtu wa namna hiyo yupo basi tumpe Nchi maana inaonekana anaiweza vizuri. Ikiwa mtu huyo anaweza ku control angle zote kama unavyotaka kutuaminisha Why Asiwe kama Trump tukamchagua tena.

Mimi nawaza postively kwamba huyo mtu anatufaa sana. He is powerful, Able and Briliant.

Yangu ni hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…