Mkuu niliwahi kuongea na mchina mmoja miaka ya nyuma. Nilikuwa nasoma IT chuo nikiwa na miaka 30. Akanicheka kweli kweli akanimbia miaka zaidi ya 35 kufanya kazi za IT ufanisi unakuwa mdogo wa sababu mind yako inakuwa siyo sharp. Kitu ambacho nakubali ni kuwa kazi nyingi zinazohitaji kufikiria na ku-react kwa haraka kama kutusha ndege za kivita, udereva wa magari ya mashindano kama formula one, etc miaka 35 watu wanaanza kufikiria kustaafu. Hili ni suala la kitaalam kabisa.
Hii pia nimewahi kuisoma kwa mwana jf mmoja anaitwa Habib ni mtu Wa hadith nyingi, makala na machapisho, alikuwa akiongelea mambo ya mosad, shirika la kijasusi la Israel, anadai kwenye mambo ya tehema na habari za udukuzi wanachukua vijana wakiwa teenage, wanakuwa trained wanafanya kazi zao wakifika at 20's wanastaafu wanaajiriwa kwenye taasisi za kiraia kubwa kubwa such as Google huko na kwingineko
Ki-IT na Mimi pia nakubali mtoto Wa miaka 16 anaechemka vizuri kichwani anajua hisabati vizuri ukimsomesha kwa muda Wa miaka 7 tehama akifika miaka 23 asee atakuwa wamoto sana then anakufanyia kazi miaka 10 akiwa wamoto na akiendelea kuwa Wa moto zaidi kadiri anavyoendelea kufanya kazi
Lakini utu uzima kuwaza majukumu na nini kuna vitu vipya sana utatakiwa ujifunze ukiwa kazini ila wewe utakuwa unavipiga chini na pia utu uzima unakuja sana na u-technophobia kwetu sisi watu weusi unless ulikuwa unapenda mambo ya technology toka ukiwa kijana
Nimepita huko mashuleni nimeona siku hizi wana mifumo mbali mbali waliyopewa toka tamisemi kama prem, nahisi ni mfumo unaohifadhi taarifa za wanafunzi unafanya usajili kadhalika transfer kwa wanafunzi ila wakuu wengi Wa shule hawajui baadhi yao hata kufanya simple operation katika system hata kum transfer mwanafunzi na wamewaachia vijana, sio kwamba wame deligate power!, no hawajui na wanaogopa, sio wote ila wengi wao
Binafsi naona kwenye masuala ya technology vijana wetu wananza wakiwa watu wazima sana, kuanza Chuo (say) computer science ukiwa na miaka 22 binafsi naona ni miaka mingi sana hiyo katika technology field tena mingi mno
Kijana aanze akiwa 18 hivi naona ni nzuri zaidi