Labda anitekenye

Labda anitekenye

Wachekeshaji wengi wa Tanzania hawajui kuchekesha. Angalau hizi skits zimekuja kuwaokoa. Kwenye skits ni hit-or-miss.

Bongo kwenye sanaa ya uigizaji / uchekeshaji hakuna quality bali quantity, tuna watu wengi wanaojiita wachekeshaji kushinda wachekeshaji wenyewe.

Ukifuatilia majukwaa kama Watu Baki, Cheka Tu: mada zao kwa 70% ni ngono. Uchekeshaji wao lazima wahusishe ngono, wanachowasilisha ni kama kimelenga aina fulani ya hadhara: watu wa hovyo.
Hii point!
 
Kuchekeshwa ni hisia.
1. Haijalishi mchekeshaji anatoka Taifa gani. Ni sawa na mtu aliyeuliza Kati ya King Majuto na Mr Bean nani mkali. Wengi wakacomment unafananisha mtu aliye 'mbele' na hapa bongo! Badala ya content
2. Uchekeshaji ni kama wimbo. Huu unakuvutia lkn ule haukuvutii.
3. Uchekeshaji haiendani na umaarufu wa mchekeshaji bali namna anavyokuchekesha. Ndio maana Kuna watu tunao mtaani wanachekesha vzr tu
 
Watu wanaoweza kunichekesha ni wachekeshaji wa Genre ya Black Comedy tofauti na hapo sicheki naona anaigiza utoto.
Baadhi ya muvi na series za black comedy ni
  • The Dictator
  • The boys (series)
  • You don't mess with the Zohan
  • Breaking Bad
  • Better Call saul
  • Game of thrones
Comedy ni hisia. Na si umaarufu wa msanii. Ni vile anavyokuchekesha tu bila kujali anatokea wapi
 
Ili ucheke inatakiwa uwe kwenye mkao wa kucheka. Ukisema ukaze hata Mr Bean hatoboi

Ikiwa unapiga stori na rafiki yako mnayeivana,akisema kitu kidogo ni rahisi wewe kucheka hasa ukijua kuwa kusudio lake ni wewe ufurahi. Tofauti na jambo hilo hilo akilisema msiyeivana
Huu ndio ukweli. Si jina la mchekeshaji wala umaarufu wake
 
Back
Top Bottom