Hajazinguwa shafii nadhani kitenge au somebody pale wasafi au simba ana maslahi na chasambi ndo maana wamelivalia njuga hili kwasababu shafii alichokiongea ni masuala ya kawaida kibiashara hasa kwenye uwakala wa wachezaji
Unashindwa kuelewa wanaompinga Shaffih sio Wasafi wala Kitenge
Ni mawakala wa mchezaji na mchezaji mwenyewe.
Shaffih Dauda alikuwa anafosi kupata commission kwa kutaka Chasambi asajiliwe na timu kupitia foundation yake.
Shaffih Dauda alikuja na dili feki na akasimama kama middle man lakini management ya mchezaji ilikuwa smart kugundua ulafi wa jamaa.
Shaffih Dauda alimfata mchezaji na kumu approach kuwa kuna offa kutoka Ulaya ambako ni Israel.
Dogo akafikisha huo ujumbe wa management yake na management yake ikafanya mawasiliano na Shaffih Dauda kuwa wapo tayari ila tupe hiyo offer tujadili maslahi atayopata mchezaji.
Lakini Shaffih Dauda hakuweza ku prove hiyo offer kuwa ni real. Walipoona jamaa alikuwa ana test upepo kwa madai feki wakampiga chini waka stick kwenye dili ambalo limeletwa na Simba.
Sasa yeye alipoona wamemla kichwa kwenye mchongo wake wa Israel akaja kwenye media akiwa emotionally eti yuko disappointed kwa kitendo cha dogo kusajili Simba na kuacha kwenda Ulaya.
Alipokuja kuharibu ni kutaja mkataba alionunuliwa Simba kutoka Mtibwa ambapo kwa mujibu wa management ya mchezaji Shaffih Dauda ametoa maelezo ya uongo.
Na moja ya hoja ambayo hata mimi nimeizingatia kutoka upande wa management ya mchezaji ni kukanusha taarifa za uongo ambazo zingeachwa ziwe spread zingewesa kuleta madhara.
Kuna kasumba ya kusikia boss katoa milioni 200 ya usajili halafu uongozi wa Club unamleta mchezaji aliyesajiliwa kwa milioni 100 halafu kwenye ripoti wanaandika milioni 200
Kwa hiyo Shaffih Dauda kwa kitendo chake cha kudanganya kutaja thamani ya mkataba kinaweza kuleta taswira tofauti, boss aliyetoa hela ya usajili anaweza kudhania kuwa amepigwa kwasababu kiasi kikichotajwa na Shaffih Dauda hakifanani na kiasi alichoandikiwa kwenye ripoti.