Ladies kama wewe utachukua hatua gani?

Kwa kweli watu walio mdanganya all this time na wanao mfanyia hivo ghafla ni adui zake. ni bora akate mahusiano nao kabla hawajampangia mengine. Aondoke na mwanae (wanae) wote. Huyo jamaa na Housegirl wake wanastailiana, asiwaingilii kati.
 
pole yake jamani .Hawa watu wabaya sana wangeweza hata kumzuru.Ila hapa tunajifunza wakina mama kutowaamini sana hawa wasaidizi wa ndani.
 
, aliyemvumilia
kipipi my dia si kwamba ninamkandamiza huyu Mke wa ndoa but najaribu kuielewa hii hadithi ambayo kwa kweli ilininyima usingizi jana. Niliposema nyodo nilikuwa ninaangalia tabia ya wanawake wengi ambao tunajisahau tukisha simika mizizi ndoani (umeolewa umezaa basi unajiona unastahili na saa nyingine hata hashma na upendo kwa mwenzio vinapungua kama si kwisha kabisa) huzaa madharau na ugomvi kila kukicha. Suala la kutafuta suluhu si tija, vipi kama suluhu ilitafutwa baada ya mama kuona kuwa sasa namwagwa?
umeuliza kama ni possible kwa mwanamke kumwonyesha nyodo mumewe wakati anampenda msichana wa kazi! Well si kitu cha ajabu hasa kama anajiona anaye msichana wa kazi ambaye ni mwaminifu kwake na anamlelea wanae vema na pengine anamfichia siri zake za kurudi usiku n.k. (Najaribu tu kusoma kwa nguvu nielewe; ni assumptions zangu tu)

Bado nashindwa kuelewa kwa nini mwanaume huyu afanye hivi kwani kwa njia aliyoitumia ni kama vile amaamua kwa makusudi kabisa kumchapa kibao cha maumivu mkewe kama vile mtu anayelipa kisasi kwa mtu aliyemkosea. Ni kama faru aliyejeruhiwa hapa otherwise angefanya hicho ulichokielezea mwishoni mwa post yako..yaani kimya kimya na maisha yakaendelea!

Hapo kwenye red hebu jaribu kupageuza pasomeke ameamua kujilipua kisa MWANAMKE anayemuheshimu, aliyemvumilia na aliyemwaminifu kwake!
 

...maisha kwa upande mwingine chukulia tu kama redio kasseti...


badala ya kubonyeza rewind > stop # buttons kila mara...
wewe jitie hamnazo bonyeza fast forward tu >>

mpaka hapo walipofikia, kama hakuna kero kubwa kubwa kwanini ajiondoe kwenye hiyo ndoa? too late... amekuwa anaishi na huyo mke mwenziwe miaka nenda rudi...hakuna u - turn itayosaidia kujifariji na "laiti ningejua...!"
 
huyo jamaa ni mzinzi kama wazinzi wengine tu hana lolote,ashukuru tu kwamba amezaa na huyo mama,ningemshauri aachane naye hana maana kwake hamuheshimu hata kidogo,lakini kikwazo hao viumbe wataenda wapi? basi inabidi mama uvumilie tu,ila aweke masharti asiingiliwe sana na huyo kiumbe H/g
 
Huyo mama amwambie mumewe akakae na hg huko alikomjengea huyo hg nyumba, amuache hapo ye na wanae apumue kwanza baba aendelee kutunza wanae na mkewe. Ila wapumzishe mahusiano mpaka akili ya huyo mama itakapotulia.
 
Jamani mwenzenu naumwa nachungulia kidogo na kutoka ..
 

Nimekuelewa dear! Lakini nikiiconsider hiyo paragraph yako ya mwisho naeza pata jibu kuwa h'gal kwa sasa ndie chaguo la mume i.e amebeba asilimia kubwa (ndo maana mume kajitosa), and if thats so......now what next??? (heheheee sijasahau nakudai juice yangu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…