Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyodo?? Walitafuta suluhu wapi mambo yakashindikana? Ivi is it possible mwanamke kumfanyia mumewe nyodo alafu ampende h'gal kiasi hicho na kumuachia uhuru wote huo??(may b)! Mwisho wa siku mi nasema ni bora kujiengua. Huyo mwanamke hapendwi, believe me u...! Yaani mwanaume anafikia hatua ya kujilipua kisa h'gal?! Huyo anakuwa ameshajua kabisa reaction itakuwa ni negative na hivo ameshaamua vyovyote na iwe hata uamue kuondoka kwake poa tu! Hata kama mwanamke alianza nyodo h'gal akiwa ameshazaa, mie bado nashawishika kusema hilo lilikuwa limepangwa tu, we unadhani hiyo siri ingetunzwa mpaka lini?? Au kwa nini asingemhamisha huyo h'gal kimya kimya ili awe anaenda kupata faraja kwa uhuru? Jamani akufukuzae hakwambii tokaa...............!
Salam MMU membaz miss u big T.
Naanza na mkasa unaonishangaza !
Huyu jamaa ,Kabla hajaoa alienda kijijini kwao na kuleta binti mrembo akiwa ni mfanyakazi wake wa ndani
Amekaa nae muda mrefu huku binti akishuhudia pilika za jamaa wakati akileta girlfriends zake Na kufanya utambulisho mzuri tu kuwa ni msichana wake wa kazi na vile vile anamchukulia kama ndugu yake.
Muda wa kuoa ulifika jamaa kaoa na kuleta mke ndani ya nyumba wamekuwa na mahusiano mazuri tu kati ya mke/ mme na binti wa kazi.
Mama mwenye nyumba mungu amemjaalia watoto wawili.
Mara binti wa kazi nae alibeba mimba kisha alimleta jamaa na kumtambulisha kwa dada na shemeji kama ndo baba mwenye ujauzito
walimpokea vyema na kumuuliza nini hatma yao ,jamaa alisema atamuoa mambo yakikaa vizuri
Alienda kwao kujifungua na kukaa miezi sita kisha kurudi kuendelea na ajira yake kama kawaida.
Alifanya vema sana ktk kazi zake za ndani na kumuheshimu sana mke wa jamaa
Mama alimpenda sana na kumchukulia kama ndugu wa mmewe na wake pia,pia baba wa mtoto alikuwa anakuja mara kwa mara kumuona mwanae.
Jamaa baada ya mtoto wa H/G kutimiza miaka 3 Ndipo kaamua kuvunja ukimya kwa kuita ndugu na jamaa kuwatambulisha kwa binti wa kazi
bila kusita alisema huyo binti ana uhusiano nae toka kijijini na hata kabla hamjamuoa wife na mtoto ni wake na ameamua kumuoa kama mke wa pili
Na pia ameshamjengea nyumba anataka kumwamisha
Haya kina mama wenzangumlio kwenye ndoa na mnaotarajia kuingia kama wewe ungechukua maamuzi gani?
Hekima inahitajika hapa maana mama mwenzetu amechanganyikiwa.
Na nyie baadhi ya akina baba kwa nn mnafanya hivi lakini?
Mbona mnatuumiza sana !
Based on true.
, aliyemvumilia
kipipi my dia si kwamba ninamkandamiza huyu Mke wa ndoa but najaribu kuielewa hii hadithi ambayo kwa kweli ilininyima usingizi jana. Niliposema nyodo nilikuwa ninaangalia tabia ya wanawake wengi ambao tunajisahau tukisha simika mizizi ndoani (umeolewa umezaa basi unajiona unastahili na saa nyingine hata hashma na upendo kwa mwenzio vinapungua kama si kwisha kabisa) huzaa madharau na ugomvi kila kukicha. Suala la kutafuta suluhu si tija, vipi kama suluhu ilitafutwa baada ya mama kuona kuwa sasa namwagwa?
umeuliza kama ni possible kwa mwanamke kumwonyesha nyodo mumewe wakati anampenda msichana wa kazi! Well si kitu cha ajabu hasa kama anajiona anaye msichana wa kazi ambaye ni mwaminifu kwake na anamlelea wanae vema na pengine anamfichia siri zake za kurudi usiku n.k. (Najaribu tu kusoma kwa nguvu nielewe; ni assumptions zangu tu)
Bado nashindwa kuelewa kwa nini mwanaume huyu afanye hivi kwani kwa njia aliyoitumia ni kama vile amaamua kwa makusudi kabisa kumchapa kibao cha maumivu mkewe kama vile mtu anayelipa kisasi kwa mtu aliyemkosea. Ni kama faru aliyejeruhiwa hapa otherwise angefanya hicho ulichokielezea mwishoni mwa post yako..yaani kimya kimya na maisha yakaendelea!
Hapo kwenye red hebu jaribu kupageuza pasomeke ameamua kujilipua kisa MWANAMKE anayemuheshimu, aliyemvumilia na aliyemwaminifu kwake!
Jamani mwenzenu naumwa nachungulia kidogo na kutoka ..