Ladies, let’s do the real talk...

Ladies, let’s do the real talk...

Mi naona si vibaya kupendana na mtu sababu eti ana kila kitu, cha msingi ni kwamba inabidi uwe ni upendo wa kweli na si sababu ya mali. Na kuhusu contribution yako mtaanzia pale alipofikia utamshauri ni jinsi gani mtaendeleza hizo mali zake/zenu na mkafika mbali zaidi,pia mtaanza familia utamlelea watoto nk hizo ni contributions pia.

Ila for me sijui ila napenda nianze na mtu ambaye tutaanza from the scratch tufight na kufikia malengo pamoja, hii itacreate bonge moja la bond/ love story mapito ya hapa na pale ambayo hata tutakuja kusimulia wanetu, ila hizi ready made mmh unaweza ambiwa hukuja na chochote humu ndani so utatoka kama ulivokuja.🙄

Note:kuanza na mtu from the scratch haimaanishi hatoweza kukufanyia chochote kibaya akiamua, kuna ambao akipata anaona siyo type yake anatafuta pisi kali nyingine, so tupendaneni tu pasi na kujali kuna mali or not.
 

Kiubinadamu: kila mtu anakuwa free na proud na ana uchungu na kitu ambacho amekitolea jasho. Ni nzuri zaidi kuanza na mtu kutoka chini; lakini pia sio lazima, na pia sio guarantee kwamba huko mbele atakuheshimu na kukutreat vizuri baada ya mambo kutiki. Sasa mtu kama alianza na mwingine chini wakafanikiwa ila wakashindwana; ndiyo kusema asioe au?

Mtu sahihi; regardless ana mali au hana mali ni mtu mwenye UTU. kuna wanaume hela hana na utu hana vile vile; leo utateseka na akizipata ndiyo utateseka zaidi. Tena mwanaume mwenye hela hadi akufuate ni kwamba wewe ndiye anayekuhitaji. Upendo wa maskini hauaminiki kwa kweli (hata mimi mwanamke maskini naweza kumkubalia mtu kisa tu hela). Inawezekama kabisa yupo na wewe kwa sababu ndiyo mtu ambaye he can afford at that time; ila dream woman wake ni mwingine kabisa. Akishapata hela ndiyo yale, sikutaki wewe sio type yangu. Au mwingine ndiyo ile tu nafsi inamsuta mmetoka mbali; basi utaendelea kuwa mke mtazamaji ila mkewe halisi atakuwa naye huko nje akizitumbua.

Na tusiwaseme tu mabinti kwamba wanapenda ready made; na wanaume wengi wa kiafrika wanazingua. Mtu unaanza naye chini huko mnapigika wee; siku nuru inaanza kuonekana unasema angalau sasa na mie ntaanza kuvaa na kanguo ka elfu 15; mwenzako ameshatafuta wa kuzitumia naye. Wewe ndani maisha yanabaki almost vile vile afu huko nje mwenzako anaspend tu. Ndiyo malipo yako hayo.

Kuna mdada humu alikuwa analalamika mumewe wameanzia huko chini, wakapambana wakaanzisha kampuni yao, sasa hivi imesimama maisha yamewanyookea. Lakini mume magari anapanda mwenyewe, mke anaenda ofisini na daladala. Yaani magari ya kwao lakini yeye anaishia kuyapigia picha kwa nje, kila kitu ni manyanyaso. Na usiseme mkewe alimnyanyasa zamani coz she did'nt. Na mtu akunyanyase afu akuvumilie miaka yote hiyo hadi mje mfanikiwe; obviously angeshamuacha au basi mshukuru tu alikupa mori ya kupambana. Ndiyo hayo wanawake wengi wanaishi kwa uchungu, anasubiri mume afilisike au agonjeke ndiyo anapata chance ya kulipiza. Na wanaume wakorofi uzeeni wanaisoma namba

Binti akikutana na mwanaume ana mali, akampenda na ana utu na anamuheshimu; kwa kweli aolewe tu. Usimkatae mtu kisa eti ana mali atakunyanyasa wakati mtu hajawahi hata kukudharau. Umaskini sio sifa wala sio kigezo cha kuja kuwa mume bora. So tusiwachukulie wanaume wote wenye mali kana kwamba hawafai na maskini wote ndiyo wanafaa. Kuna watu wana dharau zao za asili hata kama hana hela. Yaani hata muanze naye barabarani; kwake hutokuwa na hadhi wala heshima.

Kama mtu ana mali aombe tu apate mtu mwenye kujitambua; atakayekuwa na uchungu na mali za mumewe kwa sababu anajua ndiyo zitawasaidia watoto wao na wapendwa wao. Sio mtu ana akili ya ku-slay tu.
UPENDO wa kweli ndio silaha ya ndoa.......hata kama mmeanza pamoja.......bila UPENDO wa kweli ni bure.....Upendo jamani.....Upendo tuu....
 
A guy unamkuta ana nyumba, ana usafiri, ana biashara yake na kazi yenye kipato kizuri. All of this umekuta ameaccomplish mwenyewe bila ya wewe.

Then unakuwa attracted na this type of a guy na kumpa all of your attention na moyo ili muwe pamoja. But the problem inakuja kwenye swala moja?!

Unakwenda kuchangia nini katika maisha yake zaidi ya kutaka kutumia nae alichotafuta?!

If he in all well and good and you are broke as broke. Nambie hapa unakwenda kutoa what type of contribution ili tuite umekwenda fanya maisha na huyu brother?!

Ladies can I hear from you about this, guys you too can contribute.

On my side sijawahi kutamani that time of start katika mahusiano. The good thing nimeona thamani ya kuanza pamoja na hata hapa nilipofikia nashukuru sana MUNGU naona tofauti ya kuishi na mwanaume na kuwa na mwanaume.
Uko sahh mpenz nakuunga mkono
 
..mimi kama nina mali naoa mwanamke ili anizalie watoto tu...yanini kuhangaika kutafta mwanamke mwenye pesa/mali.....nikipata demu hata golikipa poa tu..ilimradi ananipenda...analea family na kunizalia watoto...hiyo ndio kazi ya mke....mimi kazi yangu kutafta mali....
Hamna furaha kwangu nikiwa na mwanamke asiyejua kulea family...hata kama ana PhD na kazi ya pesa ndefu..
 
Ladies, ni wanaume wachache sana uwakute wana kila kitu na bado wataku treat right, tumeanza from the scratch na my current man na raqha ya kupendwa na kuheshimiwa naiona lol'.
DJ shikilia hapo hapo

Jamaa alikuwa ana treat left sio?
 
Kikubwa kupendana tu haijalishi ana mali au hana mali. Unasema naenda kucontribute nini? Yeye hadi anakuja kunitaka atakuwa anahitaji nini? Mpaka akataka mahusiano basi kuna kitu ameona kinapungua katika maisha yake, hicho ndio nitakachocontribute
Unakuwaga na akili saa zingine we mtoto
 
Nina Mali niko vzr kiuchumi hatujaanza wote hamna kitu ume contribute nikikufuata of course you are the woman I want
Katika wengi niliokua nao [emoji16] umenipata vizuri hauko peke yako

Yule nilianza nae namuogopa sana tena nahemushimu na ukitaka Ku cheat kunakuwa na ka imani flani hivi nafsi inakusuta
Ah wapi kwenye kuchepuka wanaume nafsi hazijawahi kuwasuta hata siku moja ndiyo maana hamuachi! Zingekuwa zinawasuta mngeacha!
 
Ah wapi kwenye kuchepuka wanaume nafsi hazijawahi kuwasuta hata siku moja ndiyo maana hamuachi! Zingekuwa zinawasuta mngeacha!
Hivi kuna tofauti ya kuchepuka huku nafsi inakusuta na kuchepuka huku unachekelea?
 
Back
Top Bottom