Ladies, let’s do the real talk...

Mi naona si vibaya kupendana na mtu sababu eti ana kila kitu, cha msingi ni kwamba inabidi uwe ni upendo wa kweli na si sababu ya mali. Na kuhusu contribution yako mtaanzia pale alipofikia utamshauri ni jinsi gani mtaendeleza hizo mali zake/zenu na mkafika mbali zaidi,pia mtaanza familia utamlelea watoto nk hizo ni contributions pia.

Ila for me sijui ila napenda nianze na mtu ambaye tutaanza from the scratch tufight na kufikia malengo pamoja, hii itacreate bonge moja la bond/ love story mapito ya hapa na pale ambayo hata tutakuja kusimulia wanetu, ila hizi ready made mmh unaweza ambiwa hukuja na chochote humu ndani so utatoka kama ulivokuja.🙄

Note:kuanza na mtu from the scratch haimaanishi hatoweza kukufanyia chochote kibaya akiamua, kuna ambao akipata anaona siyo type yake anatafuta pisi kali nyingine, so tupendaneni tu pasi na kujali kuna mali or not.
 

UPENDO wa kweli ndio silaha ya ndoa.......hata kama mmeanza pamoja.......bila UPENDO wa kweli ni bure.....Upendo jamani.....Upendo tuu....
 
Uko sahh mpenz nakuunga mkono
 
..mimi kama nina mali naoa mwanamke ili anizalie watoto tu...yanini kuhangaika kutafta mwanamke mwenye pesa/mali.....nikipata demu hata golikipa poa tu..ilimradi ananipenda...analea family na kunizalia watoto...hiyo ndio kazi ya mke....mimi kazi yangu kutafta mali....
Hamna furaha kwangu nikiwa na mwanamke asiyejua kulea family...hata kama ana PhD na kazi ya pesa ndefu..
 
Ladies, ni wanaume wachache sana uwakute wana kila kitu na bado wataku treat right, tumeanza from the scratch na my current man na raqha ya kupendwa na kuheshimiwa naiona lol'.
DJ shikilia hapo hapo

Jamaa alikuwa ana treat left sio?
 
Kikubwa kupendana tu haijalishi ana mali au hana mali. Unasema naenda kucontribute nini? Yeye hadi anakuja kunitaka atakuwa anahitaji nini? Mpaka akataka mahusiano basi kuna kitu ameona kinapungua katika maisha yake, hicho ndio nitakachocontribute
Unakuwaga na akili saa zingine we mtoto
 
Ah wapi kwenye kuchepuka wanaume nafsi hazijawahi kuwasuta hata siku moja ndiyo maana hamuachi! Zingekuwa zinawasuta mngeacha!
 
Ah wapi kwenye kuchepuka wanaume nafsi hazijawahi kuwasuta hata siku moja ndiyo maana hamuachi! Zingekuwa zinawasuta mngeacha!
Hivi kuna tofauti ya kuchepuka huku nafsi inakusuta na kuchepuka huku unachekelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…